Habari wakuu..!!
Kifupi nina shida na uhitaji wa kupata mtaji wa kuendesha biashara yangu (operating capital). Nina kampuni changa ya microcredit activities (utoaji wa huduma za mikopo) ambayo nimeisajili na kuianzisha tangu mwaka 2011. Mwaka 2012 nilitarajia kuanza kutoa huduma lakini mambo hayakwenda kama nilivyotarajia kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu na imenichukua takribani mwaka sasa nimejaribu kuhangaika kupata mtaji niendelee na biashara hii. Nina ka nyumba ka urithi (ingawa mzazi bado yupo hai) ambacho Bi mkubwa (mama) alinishauri either nikaombee mkopo benki, ktk taasisi za kifedha au kwa mtu binafsi au kuiuza nipate mtaji, lakini nimejaribu kufuatilia njia hizo hadi sasa bilabila. Ktk taasisi za kifedha na mabenki wameniambia inatakiwa uzoefu wa kuendesha biashara hiyo usiopungua miezi sita hadi mwaka. Kuna threads ktk jukwaa la matangazo madogomadogo nilipost humu JF tangu miezi sita iliyopita kuhusu kuuza nyumba hiyo lakini sijafanikiwa kupata mteja hadi leo (hata wa kwenda kuiona tu sijampata). Mda unavyozidi kwenda akili inazidi kunipelekesha nikiwazua namna ya kufanikisha lengo langu. Nimeshachoma meli moto (nimeachana na kazi zangu za kuajiliwa tangu mwaka juzi) lakini changamoto ni nyingi mno. Ufupi naombeni ushauri nifanyeje kufanikisha mpango huu maana mwaka ndo huu unakatika na sijui hata niweke mikakati gani kwa ajili ya mwakani.
Natanguliza shukrani.