Naombeni ushauri ya manunuzi ya gari

Bizzly

Member
May 3, 2010
79
21
Wataalamu naombeni ushauri. mimi kwa hela niliyo nayo siwezi agiza gari nje sana sana nitachukua showrooms au nitamvua mtu. sasa nishaurini ni vitu gani vya msingi natakiwa kuwa makini navyo hasa nitakapoamua kununua gari kutoka kwa mtu binafsi? na kama ni showroom ni zipi ambazo ziko fresh kiuaminifu na kigharama? asanteni kwa ushauri wenu.
 
Kama hela yako ni ndogo itabidi umvue mtu, za showroom ni ghali sana kuliko kuagiza nje.
 
Wataalamu naombeni ushauri. mimi kwa hela niliyo nayo siwezi agiza gari nje sana sana nitachukua showrooms au nitamvua mtu. sasa nishaurini ni vitu gani vya msingi natakiwa kuwa makini navyo hasa nitakapoamua kununua gari kutoka kwa mtu binafsi? na kama ni showroom ni zipi ambazo ziko fresh kiuaminifu na kigharama? asanteni kwa ushauri wenu.

Showroom wananunua nje wanaweka na faida yao ndio wanakuuzia mteja, sasa iweje ushindwe kuagiza ununue showroom na budget iwe tight? Hebu tuweke sawa.

Kununua gari kwa mtu ni risky, inategemea na mtu anayeuza na unavyomjua. Kwani itasaidia kujua matumizi yake yalivyokuwa na utunzaji wake, ukinunua kwa mtu usiyemjua inakuwa ngumu kidogo kuweza kufatilia kila kitu, inabidi uende na fundi wa uhakika mwenye uaminifu na kuipenda kazi yake akakuchekie kila kilicho muhimu kuangaliwa kwa kina ndio ufanye manunuzi.

Kama unataka kununua gari kwa mtu, njoo nikuuzie yangu. Nipm tutaongea vizuri. Ni Mazda MPV, 2002 model, ina 7 seats (kama noa, au kubwa zaidi), 2.0 auto engine. Consumption yake si mbaya (elf 50 naenda shamba moro na kurudi-kama 450km hv), vipuli vimejaa tabata vipya na used, ila kama una access ya kenya ndio rahisi zaidi. Ina new tyres na vitu kibao.

Karibu.
 
Back
Top Bottom