Rahul Pacquao
Senior Member
- Feb 9, 2013
- 148
- 180
- Thread starter
- #21
nimekuelewa mkuuUnaweza ukakuta kuna mtu kampata anamzuzua kichwa tu na ndo maana kaamua kufanya hayo, na kusahau kua kuna maisha tena huko mbele. Mwanamke akikamata pesa/kazi nzuri huwa mara nyingi inakua hivyo, japo sio wote, ila kibarua kikiota nyasi huwa wanachanganyikiwa na kujirudi kuanza kuomba msamaha.
Ndo maana nimemwambia mkuu asijitie mawazo wala presha, japo kweli ni jambo gumu, linauma sana, hasa ukiangalia ndio mtu uliemchagua uishi nae maisha yako yote na ndio mama wa mtoto wako ila kaamua kukugeuka.
Huyo mwanamke naamini atarudi kwa jamaa kumpigia magoti na kumwomba msamaha tu, apewe muda ayaone maisha yanavyokua.
Pia jamaa ndio anauwezo wa kumnyoosha huyo mwanamke kisheria kuliko maelezo, kama ataamua kumnyoosha kweli. (Ila si mshauri amnyooshe, amwache tu arukeruke na afanye analotaka, yeye apambane kupata ruhusa ya mahakama ya kumlea mtoto tu, halafu amwachie mungu amlipie maumivu aliompa)