Naombeni ushauri wenu katika hili suala jamani nisije kuingia kichwa kichwa

Nchi yenyewe ipo chini ya mwanamke kwa sasa. Kubali matokeo piga moyo konde, kama unampenda yajengeni.

Haya mambo hayana kanuni, na hakuna njia moja inayofaa kwa kila mahusiano. Kama umeridhika nae kama mke, weka ndani fanyeni maisha.

Angalizo. Mfunge ndoa mapema...kichwa chako nna mashaka nacho haukawii kubadili gear angani.
 
Nchi yenyewe ipo chini ya mwanamke kwa sasa. Kubali matokeo piga moyo konde, kama unampenda yajengeni.

Haya mambo hayana kanuni, na hakuna njia moja inayofaa kwa kila mahusiano. Kama umeridhika nae kama mke, weka ndani fanyeni maisha.

Angalizo. Mfunge ndoa mapema...kichwa chako nna mashaka nacho haukawii kubadili gear angani.

Na kweli kwenye hilo swala ameharakisha tufunge ndoa mapema, Me mwenyewe akili zangu kama ulivyosema Bro ila nitajitahidi nisiumize hisia zake
 
Habari zenu waungwana natumai mko poa Poleni sana na Majumuku ya kila siku,


Ndugu zangu mimi ni kijana wa Miaka 25, Nimezaliwa mkoa Wa Dar es Salaam, Kigamboni
Elimu yangu ni kidato cha nne, Nilipata max za kwenda chuo tu hivyo nikachagua kwenda chuo cha Procuremement And Supply kilichopo Chanika Dar Es Salaam (IPS)

Ila sikuweza kumaliza kutokana muingiliano wa mambo mengi plus sisi vijana hivyo nikaishia njiani, After that nikakaa tu kitaa nikawa napiga mishe za hapa na pale.

Nina ujuzi wa kuendesha Gari hivyo niliajiria sehemu kwa mtu binafsi kusambaza Vinywaji vya jumla mimi na mwanangu mmoja ambae tulikua wote kitaa. Sasa tulipga mishe kwa huyu Mama takribani kama Mwaka hivi na alikua anatulipa 70k kwa Mwezi.

Kwa muda huo nilikua siishi nyumbani kwa wazazi wangu niliamua kutoka kuishi kwa wana tu ili nipambane kivyangu ila siku za Weekends nilikua naenda nyumbani kusalimia.

Basi siku zikasonga tunapiga mishe kama kawaida mwisho wa mwezi kila mtu anapewa salary yake ingawaje alikua anatoa nusu nusu (Mama alikua mchachu kwenye kutoa hela huyu)

Lakini tulikua tunapata ila mtu hufanyi malengo kutokana na hela the way unavyoipokea (nusu nusu) hivyo hela ikawa haionekani inapoenda unajikuta mtu hela vuuuuup! Imeisha so baada kama ya mwaka mmoja kukata kila mtu ikabidi sasa tuanze kushauriana.

Kwamba tusepe kwa huyu Mama tukatafute mishe zingine au namna gani vipi, ila maamuzi yaliyotoka ni kukacha tu maana hamna kinachoeleweka basi bhana, Me nilikua na mwanangu mwingine huyu yeye nilisoma nae chuo, Tukayajenga tukaamua twende zenji kutafuta maisha maana tulipata tetesi kule kazi za Hotels wanalipa kidogo hela nzuri kuanzia 250k kwenda juu.

Basi huko ZNZ tukafikia kwa mshikaji ambe alikua anamfahamu yeye sema jamaa alikua ana mishe yake ila na yeye mambo mengi sio mtu wa kutulia sehemu moja leo yupo ZNZ mara Dar mara Mkoani so unakuta anatuacha pale hata Mwezi halafu hatuna mishe patamu hapo, Mtu unaamka asubuhi hujui pa kwenda upo ugenini na wala hujui unakula nini.

So ikabidi tukikaze kiume kama siku tatu zikapita yule jamaa yangu kumbe nikagundua alikua mtoto wa mama() alishindwa kula mlo mmoja kwa siku so akapiga simu kwako wakamtumia nauli akarudi Dar nikabaki mwenyewe jeshi la mtu mmoja.
Basi nikanza kuzurula bhana maana kiukweli me mzurulaji nikafika sehemu kuna Bar na ndo ilikua kama kijiwe watu watu wanakutana pale kula urojo yakheee

Huku na huko nikakutana na jamaa tukaanza stori mbili tatu kumbe jamaa asili yake ni M'bongo sema amekulia huku Zanzibar, Jamaa alikua Bodaboda so akawa ananiachia Day worker nikawa napata japo ya kula mishkaki ya kuku na maisha yanasonga

Ila kumbe jamaa nae Bodaboda alikua anafanya tu kwa muda ila alikua anaskilizia mishe ya Hotel so na mimi nikapata upenyo hapo nikajichomeka kwasababu ilikua ni kupelekwa tu na kuanza kufanya kazi hakuna kufanyiwa interview wala kupeleka CV yoyote ile.

Sasa kimbembe ni pale mtu unakabidhiwa Department halafu huna ujuzi nayo patamu hapo. Mimi bhana nikapewa kitengo cha Waiter kwasababu nilionekana kidogo nina Communication skills na Lugha ya kuombea maji tu inapanda, Yule mwenzangu yeye akawekwa Jikoni, Kupika pika, kukalangiza, Chef kama Chef (Ila kichwani hamna anachokijua)

Bahati nzuri upande wangu huku kulikua na mtoto mmoja hivi wa Kinyaturu yeye alikua ana ujuzi na mambo ya Restaurant, So nikajitoa ufahamu nikamchama kwamba me nimeletwa tu hapa ila hamna hata moja nalojua, Hata sahani sijui inashikwaje.

Bahati nzuri kale kabinti Lugha ilikua haipandi so yeye mwenyewe alikua anapata wakati mgumu kwenye kuongea na wale wazungu bhana ila ni Pisi kali, So hapo akaanza kunipa somo Hapo ni Asubuhi kabla wageni hawajatoka kwenye Rooms kuja kupata Breakfast, Basi akanifua pale dakika kadhaa na mimi namshukuru Mungu kichwa yangu hii ni nyepesi hivyo kuna baadhi ya tips nikawa nimekariri vizuri.

Sasa hapo kimbembe wageni wakaanza kuja kupata Breakfast akawa ananiambia mimi niende Daah!
Nikaona wooii kuumbuka huku, T angu nijifunze kingereza sijawahi kuongea na Mzungu face to face
Leo hii mimi sijui nitaongea matango pori gani sijui

Lakini nikafanikiwa bhana nikajingundua kumbe Kingereza kwangu kimelala tena ile SLANG weeuwee! Nikajiona sijui nani mwenyewe. Basi Mungu akasaidia na tukakawa tunapiga kazi fresh maisha yakaendelea Nakumbuka ilikua ni Mwaka 2019 mwishoni ndo nilianza kazi pale kwenye ile Hotel inaitwa ZAN PALM BOUTIQUE ipo MICHAMVI

Basi huku maisha ya mtaani kuna mtoto moja wa Kitanga akawa amenielewa bhana anaitwa Rahma
Alinitunuku Drama Boy na mimi nikasema fresh tu aikatai hiyo, Tukawa tunapunguziana uzito, Sasa bhana nikaja nikaja kupata nyepesi nyepesi kwamba kumbe yule Demu anaishi na jamaa yake ambae huyo jamaa yeye ameoa tayari sema huyo Rahma alikua kama ndo Mchepuko wake, Alimpangia chumba na mwamba matumizi yote anatoa na ukizingatia alikua amesha mzalisha yule demu.

Sema sasa yule demu Rahma alikua ameshamchoka mchizi kwasabu sometimes alikua hamjali demu anamjali tu mtoto wake basi kwaiyo demu akawa amechoka flani hivi kuishi na yule jamaa, Maana Siku za kawaida jamaa yupo kwake na mke wake ila kila Weekend ndo anakuja huku kwa mchepuko wake.

So demu alivyokutana na mimi nyamwezi akadata na mimi bhana maana vitu nilizokua nampa tofauti na yule jamaa yake mla urojo Demu akataka aachane na mchizi eti aje kuishi na mimi,

Aaah! Kidume ngashtuka nikaskutiiii nikaona mhh! Huku Zanzibar sina cha ndugu wala nini nikija kupigwa Kipara na hawa wapemba sijui ntaenda kusema nini nyumbani

Nikamkataa yule demu kiaina japo alinipenda kweli na mimi nilimuelewa kwa shoo zake za kitanga sema ndo hivyo ningekua mlimbukeni wa mapenzi Wapemba wangekula kichuri
So nikaamua nifanye maamuzi ya kiume tu nikapita hivi, Na kwakua ndo ulikua mwaka wa Corona 2020
Hivyo Hotels zote zikalazimika kufungwa watu wakarudi mtaani kuskilizia hali itakuaje na mimi ndo nikasepa kuja huku Dar.

Kwa sasa nipo Mbeya huku kuna biashara flani nilikua nafanya na wachina nilianza mwaka 2020 mwishoni,
Sema Corona nayo ilivyokuja hii Second Wave ndo imekua kali kuliko the first one so biashara imesimama kwa muda,
Sasa bhana katika kupita pita huku na huku (Hapa Mbeya sasa) Sehemu flani hivi panaitwa MBALIZI

Kuna sehemu kuna kijiwe cha Pooltable mimi huwa ni mchezaji wa hilo dude, Sasa pembeni yake kina Mgahawa wa chakula Kuna mdada flani nilimuona hapa kiukweli nikamuelewa, Hivyo nikaanza kwenda kula pale kwenye mgahawa wale kila siku ilimradi anizoee kama mteja wake kumbe mnyabi hapo nina mingo zangu

Kwenda kwenda weeeee! Mwisho wa siku tukazoeana nikawa napata chance ya kukaa nae pamoja na tunapiga story mbili tatu, Kwenye Story hapo kuna Drama zinaendeleea like making eyes contact with her, Looking at her Lips nini yani vitu flani hivi amazing

Basi tukabadilishana namba za simu bhana siku ikitokea sijaenda ananiuliza upo wapi sijakuona leo
Mnyamwezi nikiona hiyo meseji Najihisi kama nipo Mawinguni vile naelea
Basi siku ya siku ndo nikamfungukia bhana kwamba mimi kutoka kwenye kumoyo nimekumanya sana.

Doooh! kitumbua nikatia mchanga nikachezea cha mbavu, Aisee hamna siku mwananume nilikua Broken kama siku hiyo sikutaka hata kumuuliza marambili nilirudi Gheto Ndonga imekua nzito kinoma kwa stress Daah! Oya wee ogopa sana kama Manzi umemuelewa like really na akakuonesha all the signs halafu eti anakupa za uso daah!

Usiku sikulala usingizi hauji nikaamka nikaanza kuskiliza ile Album ya Aslay
Chozi linataka linitoke lakini hapana najikaza
Linataka litoke mara ya pili lakini hapana nikajikaza

Mara ya tatu nikajikaza mpaka mavi yakanibana nikaenda chooni kwanza kushusha mzigo kwanza kurudi huko ndo kidogo ikawa nafuu kwangu ndo nikapata usingizi nikalala.

Kesho yake nilivyoamka nikamvungia pale kazini kwake sijaenda na wala sms sijamtumia kutwa nzima, Nikatafuta kijiwe Cha PS4 nikaenda zangu pale kupoteza mawazo..

Siku ya kwanza..

Siku ya pili..

Siku ya Tatu yake sasa ilivyofika mida kama ya saa 12 jioni hivi (Bado nipo kwenye PS hapo tangu asubuhi) nikaskia sms kwa simu yangu sikutaka kujisumbua, nikaipuuzia
Mara naskia ya pili tena, Argh! Nikasema ngoja nicheki, Nakutana na meseji hii

"Samahani ile juzi nimekujibu vile"
"Ndo umenuna??"

Jamani wazee wenzangu hivi ukiona sms kama hiyo niambie we utajiskiaje
Yani kuna kafeeling flani hivi kanakuja kama vile umepokea uponyaji yani

Basi tukawasilana na mambo yakaenda sawa sawia mnyabi nikaanza kuishi kwa furaha tena,
Hivyo huyu mdada yeye Kwanza Kabila Ni Mrangi na amenizidi miaka minne ila kimuonekano bado binti na ni pisi ya kueleweka kama mnavyojua Warangi venye wanakua kwanza Mweupe

So mdada anataka nimuoe na halafu amenipa plani ya mimi na yeye tukafungue Restaurant nzuri pale Mbeya mjini ambavyo kwa hesabu za haraka tumepiga inagarimu kama 12milioni na ananiambia yeye anao uwezo wa kukopa mkopo Bank wakampa tukafungua hiyo biashara na hapa navyoandika uzi huu ashanitambulisha kwa kaka zake kama wawili hivi na yuko serious na swala la kuoana.

Sasa ushauri naomba kwenu ndugu zangu je?? Nimuoe halafu tuendelee kupambana na maisha wote tukishirikiana au itakua jau me nipambane kivyangu tu???

Ahsanteni sana kwa muda wenu nategemea ushauri wenu ndugu zanguni.
Ile huyu mrangi sijaona sehemu unapomsifia kuhusu kugegedana kama yule wa tanga...hili kwangu mie naona kama litakuwa tatizo.
 
Na kweli kwenye hilo swala ameharakisha tufunge ndoa mapema, Me mwenyewe akili zangu kama ulivyosema Bro ila nitajitahidi nisiumize hisia zake

Bora unajielewa man, ila kama unajua fika hauna mpango nae, usimpotezee muda na itakusaidia mbele ya safari.

Lakini ikiwa nafsi inamkubali kwamba ni wife material, sukuma ndani. Usiendelee kupoteza muda
 
Huyu anapenda kitonga ndo maana anapata wanawake waliokata tamaa. Fikria wewe huna mtoto ila unapenda uoe mwanamke aliyekwisha zaa na anakuzidi umri. Hivyo ni vya kunyonga, vyakuchinja huviwezi. Unapenda ile pesa mfungue restaurant ila jua hiyo pesa anaipata kutoka kwa jamaa anayemkula tu. Wewe ni mchepuko wa binti wa kirangi .

Ushauri wangu, tafuta binti unayemzidi umri na asiwe amezaa uoe
 
Back
Top Bottom