Naombeni ushauri wadau; nifanye biashara au nisomee fani nyingine?

mumak

JF-Expert Member
Oct 24, 2013
1,069
661
Mim ni muhitimu wa shahada ya ualimu mwaka 2017 ktk fani ya elimu BaED, sasa kutokana na changamoto za ajira nimewaza vitu vifuatavyo, Kusoma tena certificate ya fani nyingine.
Au
Kufanya biashara!,
Sasa najaribu kuwaza tu nikienda kusoma na pia na huko malengo yasipotimia itakuajee? Na je nikifanya biashara, je mtaji ukiyumba itakuaje? Sasa nipo dilema, naombeni ushauri wenu wadau.
 
Mim ni muhitimu wa shahada ya ualimu mwaka 2017 ktk fani ya elimu Baed,sasa kutokana na changamoto za ajira nimewaza vitu vifuatavyo,
Kusoma tena certificate ya fani nyingine
Au
Kufanya biashara!,
Sasa najalibu kuwa kuwaza tu nikienda kusoma na pia na huko malengo yasipo timia itakuajee? Na je nikifanya biashara je mtaji ukiyumba itakuaje?sasa nipo dilema,naombeni ushauri wenu wadau,
Duuuuh,
Nakushauri KASOME,,,,,,,
BIASHARA BILA "NDUMBA" haiendiiiii.
Utakuja kulia kilio cha SAMAKI.
 
Mim ni muhitimu wa shahada ya ualimu mwaka 2017 ktk fani ya elimu Baed,sasa kutokana na changamoto za ajira nimewaza vitu vifuatavyo,
Kusoma tena certificate ya fani nyingine
Au
Kufanya biashara!,
Sasa najalibu kuwa kuwaza tu nikienda kusoma na pia na huko malengo yasipo timia itakuajee? Na je nikifanya biashara je mtaji ukiyumba itakuaje?sasa nipo dilema,naombeni ushauri wenu wadau,
Naona una mawazo mazuri sana mkuu tatizo kubwa una wasiwasi pia hauna imani na vitu unavyopanga kuvifanya kwa ufupi unakata tamaa mapema kabwa hata ya kujaribu kitu unachotaka kukifanya kama ni mpira umeshafungwa nje ya uwanja kabla hata haujaingia uwanjani kucheza, kiufupi itakuaje zimekuwa nyingi, kama unaamua kufanya biashara au kusoma fanya kwa moyo mmoja na kwa imani, "no plan work for the first time" and "everything is hard before it's easy" , hata hiyo elimu uliyonayo ni kubwa sana kama ukiajiamini na ukiamua kifanya kitu.
 
Aise fanya biashara kwani kwa miaka kumi hii hakuna ajira kabisa
 
Mim ni muhitimu wa shahada ya ualimu mwaka 2017 ktk fani ya elimu Baed,sasa kutokana na changamoto za ajira nimewaza vitu vifuatavyo,
Kusoma tena certificate ya fani nyingine
Au
Kufanya biashara!,
Sasa najalibu kuwa kuwaza tu nikienda kusoma na pia na huko malengo yasipo timia itakuajee? Na je nikifanya biashara je mtaji ukiyumba itakuaje?sasa nipo dilema,naombeni ushauri wenu wadau,
Kwanini usome certificate? Why usiongeze hata masters ya fani nyingine?
 
Mkuu masomo gani ulichukua??
Ndugu yangu nilianza na diploma ya ualimu,nikaunga bacherol lakini ndo hivyo nilichukua masomo ya arts so nasota mtaani hata ukienda kuomba tempo wanawataka wa sayansi sasa maisha yamekua magumu sana kwangu na wala sijui mbele itakuaje kwakweli.
 
Naona una mawazo mazuri sana mkuu tatizo kubwa una wasiwasi pia hauna imani na vitu unavyopanga kuvifanya kwa ufupi unakata tamaa mapema kabwa hata ya kujaribu kitu unachotaka kukifanya kama ni mpira umeshafungwa nje ya uwanja kabla hata haujaingia uwanjani kucheza, kiufupi itakuaje zimekuwa nyingi, kama unaamua kufanya biashara au kusoma fanya kwa moyo mmoja na kwa imani, "no plan work for the first time" and "everything is hard before it's easy" , hata hiyo elimu uliyonayo ni kubwa sana kama ukiajiamini na ukiamua kifanya kitu.
Mkuu unalosema ni kweli tatizo historia yangu nilipotokea hadi nilipofika nimetokea mbali sana,kabla sijafikia hapa mkuu nilipomaliza shule sec matokeo yangu hayakua mazuri na kwa bahati mbya wazazi walishafaliki tangu nipo shule hivyo nikasoma kwa changamoto tu,nilipomaliza na kuona matokeo yangu sio mazuri nikatafuta kazi nikapata sehem nikawa nafanya kwa malengo huku narisit nashukuru nilirudia mtihani mara mbili nikapata credit,naikawa sina pesa na kule nilikokua nafanya niliacha ili nijiandae na mitihani,so baada ya hapo nikapata kazi sehem nyengine huku nikiwa na credit zangu nikafanya nilipopata msingi nikafungua biashara ya duka nikaachana na mambo ya kuajiriwa sasa nikaendelea na biasha huku najisomea private badae nikafanya mtihani wa A level nashukuru nikapata div yenye kuniruhusu kwenda chuo nikaomba diploma in sec edu sasa biasharanayo ikawa inayumba kutokana na kukosa msimamiz nikaifunga nikaenda kusoma nilipo maliza ilikua kipindi cha j.k mwishoni nikapata sup sasa na dip kurudia sup hadi mwaka unaofata nikaona bora niunge degree ndo nikamaliza kipindi cha mzee hapa na ndoto zangu zikawa zimeishia hapo baada ya kuona hamna mwalim mwenye masomo ya sanaa aliyeajiriwa na pia hata ukiangalia biashara nyingi zinakufa basi nimebaki njia panda wala sijui niende wapi nifanye nini jamii inanichukulia tofauti kwakuaniona nimepoteza mda shule hamna nilichopata.basi tu sijui nifanyaje.
 
Kama kweli unataka kwenda kusoma ushauri wangu,NENDA KASOME VYUO VYA FANI.mf.VETA.baada ya hapo jiajiri.
 
Biashara yyt kukata tamaa ni mwiko. Na changamoto hazikosekani, ukiwaza hasara sana ndio mwanzo wa anguko lako. Kaza roho songa mbele.
 
Hii elimu ya kumsubiri jiwe mtu akuamulie maisha yako, haina faida yoyote, utakufa kibudu na shahada zako…
 
Fani uliyosomea ni fani SAHIHI kabisa. Wakati sahihi ukifika, utapata ajira. By then biashara zako nazo zitakuwa zimestawi. Kwa sasa fanya biashara. Kama una mtaji usizamishe wote, weka kidogo kidogo. Utakuwa unaingeza kadri unavyopata uzoefu na faida inavyokuja.
 
Back
Top Bottom