Naombeni ushauri na tiba: Kifua kinabana sana wakati wa kulala

Uko sure hauna Asthma mkuu? Ninachojua ni kwamba wagonjwa wa Asthma hupata breathing difficulties wakati wa kulala.
 
ashomile, Inawezekana umeota kinyama kwenye ulimi karibu na koo hivi huleta kikohozi kikavu sana ambacho usiku huwa ni kero sana. Kina tabia ya kukulazimisha kusafisha mara kwa mara kabla ya kuongea, koo linakuwa kavu sana, na kupumua unapumua kwa shida
 
Hii kitu sababu ameshapima pima sana. Hapa madaktari wake wanashindwa kunyumbua ukali wa kikohozi, wakat gani? Na hii ya kifua kumuuma zaidi wakat amelala. Ni tatizo la moyo

Mkuu usiseme walishindwa kunyambua tatizo maana hatujui huwa anajieleza vipi hospitali. Binafsi huwa sina shaka na daktari yeyote aliye-spend miaka 6 kwenye shule ya medicine kwenye vitu vidogo kama hivi.

Tatizo ni tunaoumwa ndio huwa hatutaki kutafuta msaada kwenye hospitali kubwa.

Though mimi mwenyewe nimefikiria Pulmonary Oedema maana iko typical kabisa ambapo one of the commonest cause ni Cardiac failure (right sided one) ambayo inaweza ikawa ni matokeo ya cor pulmonale or other chronic lung diseases including COPD kama wadau wengine walivyosema hapo juu.

Najua kilichowakwamisha madaktari ni vifaa/diagnostic tools ndio maana wakaishia kucheki makohozi, lakini pia hali ya uchumi, mtu mwingine ukimwambia kupima X ray 10000 au 20000 anaona hela kubwa sana anaona bora kupewa dawa bila kupima, mwisho wa siku watu wanakuja kudhani madaktari walishindwa kumtibu kumbe sio.
 
Pole sana Nina wiki kifua kinanisumbua mpaka sauti inapotea nakunywa tangawizi na Limao ila kupitia huu izi nimejifunza mengi sana
 
Pole Sana mkuu.

Umejaribu kuangalia kama sio mazingira unayolala yanakuathiri? Labda vumbi, mto au godoro? Mfano ukisafiri hali inakuwa ile ile?

Ungeweza kutafuta Family Doctor ambae ni Physician atakayekuhoji na kuangalia connection ya ugonjwa na historia yako. Kuna mmoja mzuri sana ila yuko Dar.

Kila la kheri mkuu
 
King'asti, Mkuu haijarishi mazingira ninayokaa nimejaribu kwenda sehemu mbali na mgodini lakini hali ni ile ile
 
ashomile,

1. Mindset.
2. Attitude.

Ndugu pole sana. Ni muhimu ukawaza positively na sio negatively. Unasema “kama nitaendelea kuwa hai” nikwambie ndugu hakuna Daktari wala dawa yoyote itakayofanya kazi on a defeated attitude and mindset.

Katika situation yoyote, half the battle is your mindset, its fifty fifty, positive attitude and you are halfway towards victory, negative mindset and you are half way towards defeat. Change your mindset, and you just won half the battle.
The glass is half full, not half empty.

Kila la heri.
Cheer up.
 
Shukrani Daktari kwa maelezo yaliyoshiba. Pia kama ni mcheza mpira/mwanariadha wakati mwingine wanapata hitilafu hizo. Nakumbuka baba mdogo aliendesha baiskeli na kucheza mpira mwishowe akapatwa na kifua.

Sky Eclat
 
Mkuu kama bado tatizo linakusumbua jaribu kucheck allergy, na kama ungekuwa Dar kuna hospital inaitwa Ekenywa kuna maspecialist wa allergy binafsi nimewahi kuugua kikohozi kikavu kwa takribani mwaka mmoja na nusu hususani nikiwa kwenye mgandamizo wa hewa yaani mkusanyiko wa watu wengi au kwenye chumba chenye AC au hata ndani kwangu, niliteseka sana na nilitumia pesa nyingi hadi ilifika kipindi nihisi labda nina TB ya mifupa lakini nilipoenda kwenye hiyo hospital tajwa hapo juu nilikutwa na allergy na nilipewa dawa hadi sasa hivi namshukuru Mungu nipo vizuri.
 
gabana, Namshukuru Mungu nimepona kwa kweli tena sikutegemea wala sijaenda hospital kubwa ya aina yoyote, nimetumia limao nikachoka ndo kuachana nazo, nikaanza kunywa chai kila siku iendayo kwa Mungu yaani usiku na mchana nakunywa chai yenye viungo hivi: majani yaliyosagwa ya kisabato, mdarasini, hiriki na pilipili manga + sukari nikatumia bila kuchoka.

Nikaweka system ya kutafuna pilipili manga kila nilalapo yaani kifua kikinibana nilikuwa natafuna then kifua kinaachia na nikisinzia nasinzia poa. Imefika hatua nikaacha yote hayo, nina mwezi na sehemu situmii na huwa nalala bila shida

NOTE: KIFUA KAMA KINA KUBANA TUMIA PILIPILI MANGA , ILA SIJUI MADHARA YAKE WADAU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom