Naombeni ushauri na tiba: Kifua kinabana sana wakati wa kulala

Pole mkuu, Dalili kama hizi pia huwapata watu wenye matatizo ya moyo hvo ukifanya X-ray kama kutakuwa hamna tatizo jarib na vipimo vya moyo kama Echo na ECG
 
Asante kwa uchambuzi wako na Mungu akubariki kwa msaada wako.
 
Sky Eclat,
Asante sana, naanza kama ifuatavyo,

1. Sigara nilivuta kwa muda wa wiki mbili hizi ni za madukani club sport, master sports n.k, pia bangi nilitumia mwaka 2014 baada ya kumaliza chuo, ila baada ya bangi kunikataa niliacha mwenyewe na kuamua kuachana na uvutaji wa aina yoyote mwaka huo huo. Nilikuwa nimeasi kanisani nikarudi kutubu, mpaka sasa situmii sigara ya aina yoyote tangia mwaka 2014.

2. Nafanya kazi mgodini. Mwanzoni nilikuwa naenda sehemu za kuchimba almasi na sehemu hizo zina vumbi sana, nimefanya kazi kama miezi 9. Baada ya hapo nikaacha na kurudishwa ofisini, ila nimeacha kazi na kifua kilikuwa kinanisumbua siku hadi siku.

Nakumbuka nilikuwa na desturi ya kunywa maji sana usiku, ili niwe macho kulingana na kazi niliyokuwa nafanya, ilifika sehemu nilipoacha tu kunywa maji kwa wingi ndio tatizo likanipata mpaka sasa tangia mwaka jana mwezi wa (11). Pia mimi tangia udogo wangu nilkuwa nikikimbia naenda na pumua kwa kasi mpaka sasa ni hivo hivo tu.

Mazingira ya mgodini kiukweli vumbi ni ya kutosha pia baridi lina msimu kuanzia mwezi wa sita huwa kali na kweli lilinisumbua sana, nilikuwa sipendi kuvaa makoti nikiogopa kusinzia kazini.

3. Umri wangu miaka (25).
 
COPD mara nyingi huwapata watu wa 50+ lakini mazingira ya mgodini ni risk factor.

Anza vipimo vya lung function kwanza.
 
COPD mara nyingi huwapata watu wa 50+ lakini mazingira ya mgodini ni risk factor.

Anza vipimo vya lung function kwanza.
Nakubaliana na wewe kwa asilimia mia akafanye chest X-ray na lung function test. It might be helpful katika kujua what's up with him, as far as Pneumoconiosis is concerned.

Pia uvutaji wa sigara huchochea sana kutokea kwa ugonjwa wa mapafu kuwa mazito (Emphysema) ugonjwa ambao ni among of COPDs.
 
Isije kuwa ni TB mkuu, maana ule ugonjwa una visanga sana pia siyo rahisi kuugundua unaweza kwenda hospital zote, tatizo nililogundua ni kuwa mahospital yetu mengi wanafanya kazi kwa mazoea sana na majibu mepesi mno. Kuna kipimo nimesahau baada ya kupima makohozi ukakosa jibu kuna kifaa inapimwa damu kiundani sana sijui then tatizo lako linakuwa lishajulikana.
 
Una tatizo la mzio yaani Allergy. Ingekuwa unakohoa continues ningeamini (angalau kabla ya vipimo) kuwa mapafu yamepata changamoto.
 
Dodoma kuna Dispensary moja ipo Majengo Sokoni, ni ya Wachina wanatibu vizuri sana. Kuna ndugu yangu alikuwa anasumbuliwa na tatizo kama lako, wana mashine nyingi za kutafuta tatizo na hatimaye kulitibu
 
ashomile, Nakushauri nenda kaanze tiba ya kinga ya TB sio dawa za TB bali kinga ya maambukizi ya TB utanipa mrejesho baada ya miezi 6
 
Sky Eclat, Antifungal, by the way hizi kazi zake ni muhimu. Mwadui kuna mgodi na kama ni mchimbaji inaweza kuhusiana na tatizo lake.
 
Hata kiasi cha kuanzia huwezi fahamu
Mkuu tuulize wote gharama humu tunaweza kupata msaada. Kwa wanaofanya kazi hospitali au walioguza ndugu na jamaa. Ukipata clinic nzuri ya respiratory diseases utanufaija sana.
 
Wengi hatuna uelewa wa COPD, kijijini kwetu wagonjwa wa kifua cha mshipa walipewa chai ya iliki. Iliwasaidia kutibu kifua. Baada ya kugundua kuwa iliki ni natural antibiotic, nikafahamu babu zetu walikuwa na maarifa sana. Ukipika maandazi ukiweka iliki ina inhibit fungal kwa muda mrefu kuliko maandazi yasiyo na iliki.
Asante sana, nimejifunza kitu. Kuanzia sasa hiriki hazitakosekana kwangu, nitatumia mara kwa mara kwa ajili ya afya yangu.
 
Mkuu tuulize wote gharama humu tunaweza kupata msaada. Kwa wanaofanya kazi hospitali au walioguza ndugu na jamaa. Ukipata clinic nzuri ya respiratory diseases utanufaija sana.
Haya maana kwa ushauri wako nilijua wewe ni daktari.
 
Dodoma kuna Dispensary moja ipo Majengo Sokoni, ni ya Wachina wanatibu vizuri sana. Kuna ndugu yangu alikuwa anasumbuliwa na tatizo kama lako, wana mashine nyingi za kutafuta tatizo na hatimaye kulitibu
Asante kwa ushauri wako na Mungu akubariki sana.
 
Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom