Naombeni ushauri na tiba: Kifua kinabana sana wakati wa kulala

Mkuu dalili zote ulizosema hata mimi ninazo. Japokuwa za kwako ni kubwa kunizidi mimi. Dawa zote hizo hata mimi huwa nazitumia tu pindi ambapo siko poa.

Wadau hawa niliowaquote wanakuwa wana jibu kwako. Binafsi nina tatizo la Asthma, na huwa nakohoa usiku tu, na huwa napiga chafya haswa nikiingia kwenye mazingira yenye vumbi, au harufu/manukato makali.

Wakati mwingine hata baridi inaweza ku trigger Asthma. Na ugonjwa wa Asthma ni wa allergy tu. Kwa hiyo ukipima na ikibainika allergy yako (visababishi) utaambiwa uepukane navyo. Visababishi vinaweza kuwa manukato, vyakula, vumbi, baridi n.k
Ulishawahi kuvuta sigara? Ulifanya kazi katika mazingira ya hali ya air pollution? Una umri gani?

Kumbuka kifua kinahusika katika mfumo wa hewa. Hewa inayoingia mwilini ikiwa safi ni lazima itoke ikiwa chafu. Maana yake inasaidia kutoa uchafu mwilini.

Kama mzunguko wa hewa una matatizo husababisha matatizo kwenye mzunguko wa damu na moyo.

Kama mdau ISLETS alivyoeleza kuhusu pulmonary oedema. Ninamashaka kuwa unasumbuliwa na kufua cha mshipa (COPD) Chronic Obstruction Pulmonary Disease.

Nenda clinic wa check capacity ya mapafu yako ku exhale and inhale.

Mfumo wa hewa ukiwa na hitilafu hudhoofisha immune system ya mapafu ambayo ni imara sana.

Wagonjwa huhitaji uangalizi wa karibu wa daktari katika kutibu infections za kifua, dawa za kutanua mishipa ya hewa na steroids.
Hiyo mbona ni asthma. Kila unPobanwa tumia dawa. Nenda hospital watakupa dawa. Usafi wa nyumba muhimu sana. Kusiwe hata na vumbi kiduchu. Acha kutumia perfume au sabuni za unga. Lakini pia fanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Muone daktari mtaalamu wa moyo.

Pole sana
Unasema unakohoa bila makohozi halafu kwenye kupima ulipima makohozi, how?

Nenda kapime X Ray ya kifua utapata jibu. Kwa hizo dalili I guess something like Pulmonary Oedema (maji kwenye mapafu), ila vipimo ndio vitatoa majibu sahihi.
Pia huenda una mzio (allergy). Baadhi ya Madaktari huwa wanasahau kuihusisha allergy kwenye uchunguzi. Lakini nakuhakikishia yenyewe pekee inaweza kukutesa hadi ukalazwa ICU
 
Mkuu dalili zote ulizosema hata mimi ninazo. Japokuwa za kwako ni kubwa kunizidi mimi. Dawa zote hizo hata mimi huwa nazitumia tu pindi ambapo siko poa.

Wadau hawa niliowaquote wanakuwa wana jibu kwako. Binafsi nina tatizo la Asthma, na huwa nakohoa usiku tu, na huwa napiga chafya haswa nikiingia kwenye mazingira yenye vumbi, au harufu/manukato makali.

Wakati mwingine hata baridi inaweza ku trigger Asthma. Na ugonjwa wa Asthma ni wa allergy tu. Kwa hiyo ukipima na ikibainika allergy yako (visababishi) utaambiwa uepukane navyo. Visababishi vinaweza kuwa manukato, vyakula, vumbi, baridi n.k
Asthma isopokuwa controlled huwa COPD
 
Mkuu tumewahi kuwa na house girl mwenye tatizo kama hilo. Tulimpa kila aina ya matibabu ya kifua hakupona. Siku moja mama akaamua ampe dawa za minyoo. Hilo tatizo limebaki historia. Kunywa dawa za minyoo halafu urudi uje unishukuru
 
Asthma isopokuwa controlled huwa COPD
Nadhani ni COPD ndio inayomsumbua maana kuna post moja hapo juu amesema anafanya migodini shughuli zake kama nimesoma vizuri so nadhani akienda hospitali kubwa atapata ufumbuzi.

Hospital nyingi za mikoani kuna tatizo na huduma zinazotolewa, Mimi kuna rafiki wa ndugu yangu alifariki sababu tu madaktari walishindwa kumpa ushauri mapema wa kwenda hospitali kubwa alikuwa huko Shinyanga. Yeye aliangukiwa na mlango wa geti mgongoni, alipoenda hospital akapewa dawa za maumivu kumbe maskini alipata Spinal Injury.

Baada ya kama mwezi akapata paralysis ya upande mmoja ndipo madaktari wakashtuka wakampa referral aende Bugando kumbe maskini it was too late akafariki kabla hata hajasafirishwa, so suluhisho la ndugu yetu huyu ni kwenda hospital kubwa hizo ndogo ndogo watamzingusha tu bila matibabu ya maana
 
Mkuu mwili wangu ni wa mazoezi mara nyingi na huwa nacheza mafunzo ya muda yanayoendeshwa hapa mgodini ni kila wiki najitahidi mpaka Root much huwa nafanya kiukweli nikipiga mazoezi inanisaidia sana ila mpaka ninywe na chai yenye ndimu.
Hii probably ni COPD kama dada Sky Eclat alivyosema hapo juu.

So cha kufanya jitahidi uende hospital kubwa upate vipimo vya maana, kama unajiweza kidogo nenda Dodoma hospital moja inaitwa DCMC wale jamaa pale wako vizuri sana wanafanya kazi zao kwa uweledi mkubwa. Naamini ukipata tiba na vipimo sahihi tatizo lako ni dogo sana.
 
Ikiwa unakohoa wakati wa kulala, na kubanwa kifua wakati wa kulala, je unapolala pia unahisi kama hupumui vizuri?
Kama ni ndio tafuta hospitali kubwa ya maana tena Bugando. Inawezekana kabisa una tatizo la moyo.
 
Unasema unakohoa bila makohozi halafu kwenye kupima ulipima makohozi, how?

Nenda kapime X Ray ya kifua utapata jibu. Kwa hizo dalili I guess something like Pulmonary Oedema (maji kwenye mapafu), ila vipimo ndio vitatoa majibu sahihi.
Hii kitu sababu ameshapima pima sana...

Hapa madaktari wake wanashindwa kunyumbua ukali wa kikohozi, wakati gani? Na hii ya kifua kumuuma zaidi wakati amelala. Ni tatizo la moyo.
 
Japo si mtaalamu so far nimeona shauri mbili zilizo kwenda shule (Sky Eclat & tonito120). Muhusika pitia na zifanyie kazi.

Japo kibongo bongo madaktari wengi sijui ugumu wa kazi au mazingira si rafiki, unakuta mpaka mgonjwa umuulize hiki vipi unicheck? Wao Malaria na UTI ndio huwa mbio kukimbilia yaani ndio kama default.

Daktari lazima uwe na roho ya kiuchunguzi na udadisi, wagonjwa wengine hawawezi kufunguka mpaka wapewe hint na labda kwa mazoea ya tiba asili wanadhani labda Daktari ni kama sangoma atajua tu anaumwa nini kama kupiga ramli.
 
Sky Eclat,

Asante kwa shule ya hiriki. Ukimsoma vizuri mazingira anayofanyia kazi uwezekano wa COPD au Asthma ni mkubwa..
Pia dawa alizopewa kuna dawa za.Allergy, dawa ya kutuliza kikohozi (ndio ile alisema anapata nafuu maana anakunywa dawa ya kutuliza, kawaida alitakiwa wampe na dawa ya kukohoa hasa mchana ili makohozi yatoke yasibaki kwenye mapafu) na kuna Antibiotic, kuua Bacteria.

Na kwa kuwa Madaktari wengj hawana utalaamu sana wa COPD na hata hivyo dalili za Asthma na COPD zinafanana hivyo ni muhimu aende kwenye hospital kubwa wamfanyie uchunguzi wa kina.
 
Hii kitu sababu ameshapima pima sana. Hapa madaktari wake wanashindwa kunyumbua ukali wa kikohozi, wakati gani? Na hii ya kifua kumuuma zaidi wakat amelala. Ni tatizo la moyo.
Tatizo kuna magonjwa ya mapafu dalili zinafanana sana. Pamoja na kuchukua historia ya mgonjwa ni muhimu pia kuchukua vipimo vya awali. Kitu ambacho sijaelewa tatizo gani la moyo linaloweza sababisha kikohozi? Angina Pect. Ni maumivu ya kifua.
 
Labda itakusaidia, kama tatizo linakupata usiku. Angalia shuka au blanketi unalojifunika. Nilishawahi kupata shida kama hiyo kipindi fulani huko nyuma. Ilikuwa ni kifua kikali kinoma unakohoa ila hakuna makohozi. Unaenda hospitali hakuna tatizo, at last nilikuja kugundua blanketi ninalotumia manyoya yake yanatoa vumbi fulani hivi jepesi sana. Nilivyobadilisha tu na kifua kikakoma.
 
Baada ya kufahamu lung capacity ndiyo anaweza kuanza kutibiwa na Salbutamol na Prednisone. Antibiotics kama ana chest infection

Ndivyo ilitakiwa kwenda si kumrundikia mtu madawa hata hujui unamtibu nini. Madaktari wengine wanakera.
 
Nenda kafanye X Ray utakuwa na maji kwenye mapafu mkuu
Kifedha siko vizuri kwa sasa sababu hata pesa niliyokuwa nayo nillifanyia miradi ya kimaendeleo hivyo kama ntaendelea kuwa hai basi ngoja nipigane nikiamini Mungu atanisaidia niweze kwenda kwenye tiba.
 
Vladimirovich Putin,
Mkuu iko hivi, nikilala huwa nakohoa mwanzoni ila usingizi ukigusa tu basi sikohoi mpaka usiku mwingine wa kulala. Na hainichukui hata masaa mawili, ikizidi sana dakika 40 au 30 na sio mfululizo, unakohoa kidogo kidogo tu.
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom