Naombeni ushauri na tiba: Kifua kinabana sana wakati wa kulala

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,621
2,425
Habari zenu wapendwa,

Natumai mwaendelea vema na kurudumu la maisha haya!! Ila mimi kijana mwenzenu maradhi yameuteka mwili wangu.

Historia ya ugonjwa wangu ulivyoanza.

Nimekuja hapa mbele yenu, nikiwa naeleza tatizo linalonisibu.

Tatizo langu: Kifua kinabana haswa muda wa kulala huwa nakohoa bila ya makohozi kutoka, tangia mwaka jana 2018 mwezi wa 11 nilipata hitilafu hii mpaka leo sijawahi pona .

Nimeenda mahospitalini kuanzia Mwadui hospital nimepima mpaka makohozi lakini hakuna, nikaenda Shinyanga Government Hospital sijawahi pata tiba zaidi ya doze, Cetrizen ,Sediton na Amplicox pekee hapa ndo huwa naanza kupata nafuu ila doze ikiisha huwa narudi katika hali yangu ya kukohoa.

Wapendwa nimemeza doze mpaka nikahisi mwili kuchoka kwa kutumia doze. Imefika sehemu nikajikatia tamaa, kinachonishangaza kwanini kabla sijalala kifua hakibani na kukohoa kohoa hakuna?

Nikawaza labda ni UKIMWI, nikaenda hospital kupima ugonjwa huo nikakutwa mzima sina kabisa.

Siku nyingine nikaenda kupima makohozi nikaambiwa niko salama kabisa.

Ila kila nikilala nakohoa mno haswa pale usingizi unapokuwa umenikaba kama mida hii.

Nikapata mke wa mshikaji ambaye tupo nae kwenye ajira, akaona hali niliyonayo akanishauri nitumie limao, mchaichai na sukari niwe nakunywa nitapata nafuu. Kwakweli ilinisaidia na mpaka sasa inanisaidia kibaya siwezi sinzia bila kunywa kikombe kimoja.

Wadau naombeni msaada wenu wa tiba niko Shinyanga hapa Mwadui kwa sasa nimekata tamaa kijana mwenzenu.

Ukiona mzima basi mshukuru Mungu pia kabla tatizo halijawa kubwa shughulika nalo mapema maaana likiwa kubwa zaidi yawezekana hata gharama za matibabu zikawa juu sana

Karibuni kwa ushauri na ikiwezekana tiba
Ni wenu mtiifu

Ashomile William

Maoni ya wadau:

Ulishawahi kuvuta sigara? Ulifanya kazi katika mazingira ya hali ya air pollution? Una umri gani?

Kumbuka kifua kinahusika katika mfumo wa hewa. Hewa inayoingia mwilini ikiwa safi ni lazima itoke ikiwa chafu. Maana yake inasaidia kutoa uchafu mwilini.

Kama mzunguko wa hewa una matatizo husababisha matatizo kwenye mzunguko wa damu na moyo.

Kama mdau ISLETS alivyoeleza kuhusu Pulmonary Oedema. Nina mashaka kuwa unasumbuliwa na Kifua Cha Mshipa (COPD) Chronic Obstruction Pulmonary Disease.

Nenda clinic wa check capacity ya mapafu yako ku exhale and inhale.

Mfumo wa hewa ukiwa na hitilafu hudhoofisha immune system ya mapafu ambayo ni imara sana.

Wagonjwa huhitaji uangalizi wa karibu wa daktari katika kutibu infections za kifua, dawa za kutanua mishipa ya hewa na steroids.

Dalili zinashabihiana sana na REFLUX LARYNGITS (Laryngealpharyngeal reflux disease). Ugonjwa huu hasa husababishwa na reflux (backflow) ya gastric content (GERD) specifically Pepsin.

Husababishwa na some weakness za milango ya juu na chini ya njia ya chakula (Esophugus) ikianzia kinywani hadi linapoanzia tumbo.

Tindikali hii huathiri kuta za njia hiyo na inaporuka kwenda kwenye Airway (Larynx) basi husababisha dalili za kikohozi kikavu hasa unapokuwa umelala flat kwani reflux hutegemea pia gravity. Pia unaweza kupata pumu, vimbe kwenye vocal cord, sauti kupotea na kurudi.

Lakini mwanzo kabisa mtu huweza kuhisi kama kuna kitu kinakaba kooni(globus sensation),kuwa na ute mwingi mzito kooni (excessive phlegm), kuwa mkavu sana kooni, kuhisi kama masikio yamejaa maji, kichefuchefu especially asubuhi, kiungulia na kuhisi kuna kitu kinaunguza kooni au kifuani (heartburn), kupaliwa mara kwa mara unapokuwa umelala usiku.

Hii ni topic pana ila nakushauri uonane na Daktari Bingwa wa ENT (Otorhinolaryngologist).

Bugando wapo kadhaa.

All the best

ashomile, Pole sana mkuu. Kwa ushauri wangu naomba uende pale Bugando (Kutoka Shinyanga sio mbali) ukacheck hitilafu kwenye mapafu. Bila shaka there is something wrong. Pia jitahidi sana kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku yatasaidia kufungua mapafu na kuondoa some invaders.

NB: Zingatia natural home remedies kama malimao, tangawizi, asali nk. Ni bora zaidi.
 
Hiyo mbona ni asthma. Kila unapobanwa tumia dawa. Nenda hospital watakupa dawa. Usafi wa nyumba muhimu sana. Kusiwe hata na vumbi kiduchu. Acha kutumia perfume au sabuni za unga. Lakini pia fanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo. Muone daktari mtaalamu wa moyo.

Pole sana

ashomile
 
Hata mimi nahisi ni COPD au Asthma. Muhimu uende.katika hospital kubwa wakucheck una tatizo lipi
Wengi hatuna uelewa wa COPD, kijijini kwetu wagonjwa wa kifua cha mshipa walipewa chai ya hiriki. Iliwasaidia kutibu kifua. Baada ya kugundua kuwa hiriki ni natural antibiotic, nikafahamu babu zetu walikuwa na maarifa sana. Ukipika maandazi ukiweka hiriki ina inhibit fungal kwa muda mrefu kuliko maandazi yasiyo na hiriki.
 
Dalili zinashabihiana sana na REFLUX LARYNGITS (Laryngealpharyngeal reflux disease). Ugonjwa huu hasa husababishwa na reflux (backflow) ya gastric content (GERD) specifically Pepsin.

Husababishwa na some weakness za milango ya juu na chini ya njia ya chakula (Esophugus) ikianzia kinywani hadi linapoanzia tumbo.

Tindikali hii huathiri kuta za njia hiyo na inaporuka kwenda kwenye Airway (Larynx) basi husababisha dalili za kikohozi kikavu hasa unapokuwa umelala flat kwani reflux hutegemea pia gravity. Pia unaweza kupata pumu, vimbe kwenye vocal cord, sauti kupotea na kurudi.

Lakini mwanzo kabisa mtu huweza kuhisi kama kuna kitu kinakaba kooni(globus sensation),kuwa na ute mwingi mzito kooni (excessive phlegm), kuwa mkavu sana kooni, kuhisi kama masikio yamejaa maji, kichefuchefu especially asubuhi, kiungulia na kuhisi kuna kitu kinaunguza kooni au kifuani (heartburn), kupaliwa mara kwa mara unapokuwa umelala usiku.

Hii ni topic pana ila nakushauri uonane na Daktari Bingwa wa ENT (Otorhinolaryngologist).

Bugando wapo kadhaa.

All the best
 
Kuna Daktari mmoja anatumia tiba mbadala yuko Arusha,amemsaidia mke wangu kwa tatizo kama lako. Kama wamhitaji naweza kukuelekeza namna ya kumpata. Pole sana naelewa hali unayopitia.
 
Unasema unakohoa bila makohozi halafu kwenye kupima ulipima makohozi, how?

Nenda kapime X Ray ya kifua utapata jibu. Kwa hizo dalili I guess something like Pulmonary Oedema (maji kwenye mapafu), ila vipimo ndio vitatoa majibu sahihi.
Hapa niliambiwa hata kama ni makavu kohoa hapa hapa na wakaniambia kesho tena asubuhi kohoa na uje nayo nikafanya hivyo lakini ugonjwa haukupatikana.
 
Pole sana mkuu. Kwa ushauri wangu naomba uende pale Bugando (Kutoka Shinyanga sio mbali) ukacheck hitilafu kwenye mapafu. Bila shaka there is something wrong. Pia jitahidi sana kufanya mazoezi angalau nusu saa kwa siku yatasaidia kufungua mapafu na kuondoa some invaders.

NB: Zingatia natural home remedies kama malimao, tangawizi, asali nk. Ni bora zaidi.
Mkuu mwili wangu ni wa mazoezi mara nyingi na huwa nacheza mafunzo ya muda yanayoendeshwa hapa mgodini ni kila wiki najitahidi mpaka Root much huwa nafanya kiukweli nikipiga mazoezi inanisaidia sana ila mpaka ninywe na chai yenye ndimu.
 
Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom