Naombeni ushauri wa tiba wa ugomjwa huu

ashomile

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Messages
1,805
Points
2,000

ashomile

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2017
1,805 2,000
Pole sana.Mbona tatizo lako ni dogo sana.Wapo waliokuwa na makubwa kuliko yako lakini yamekwisha na sasa wanadunda kama kawaida.

Inaelekea hujafika kwa huyu mganga au daktari wa uhakika ambaye nataka nikuagizie anapatikana hapo Shinyanga karibu na hapo nyumbani kwako.

Hata mimi nikipata shida namwita ananisaidia sana.Usifikirie kuhusu fedha za matibabu na dawa.Gharama yako wewe ni kuamini atakalokuambia na kulifuata.Gharama nyingine anakulipia yeye.

Ni mganga mzuri na wa uhakika . huyu anaitwa Maombi.Kupitia Jina la Yesu Kristo.
Nenda kwenye kanisa lolote linalomubiri Kristo.Hapo watumishi watakuombea na huo utakuwa mwisho wa shida yako.Chukua hatua sasa utapokea uponyaji kupitia kanisa ni, mikutano ya kiroho na hata kupitia watumishi wa Mungu.Gharama ni bure.

Usidanganyike wa Ganga wa kienyeji hawana dawa yoyote usihangaike nao watakumaliza
Asante sana lakini naomba uamini mimi ni Msabato na huwa nasali sana pia naamini Mungu yupo , kuhusu maombi huwa naomba nikiamini siku moja nitarudi ktk afya yangu..ASANTE KWA USHAURI WAKO NA MUNGU AKUBARIKI MTUMISHI..
 

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Messages
22,735
Points
2,000

Miss Natafuta

JF-Expert Member
Joined Sep 16, 2015
22,735 2,000
Ulishawahi kuvuta sigara?
Ulifanya kazi katika mazingira ya hali ya air pollution?
Una umri gani?

Kumbuka kifua kinahusika katika mfumo wa hewa. Hewa inayoingia mwilini ikiwa safi ni lazima itoke ikiwa chafu. Maana yake inasaidia kutoa uchafu mwilini.

Kama mzunguko wa hewa una matatizo husababisha matatizo kwenye mzunguko wa damu na moyo.

Kama mdau ISLETS alivyoeleza kuhusu pulmonary oedema. Ninamashaka kuwa unasumbuliwa na kufua cha mshipa (COPD) Chronic Obstruction Pulmonary Disease.

Nenda clinic wa check capacity ya mapafu yako ku exhale and inhale.

Mfumo wa hewa ukiwa na hitilafu hudhoofisha immune system ya mapafu ambayo ni imara sana.

Wagonjwa huhitaji uangalizi wa karibu wa daktari katika kutibu infections za kifua, dawa za kutanua mishipa ya hewa na steroids.
Hivi ile ya kukatwa kilimi si inaponesha?
 

PTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
7,031
Points
2,000

PTER

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
7,031 2,000
Mkuu iko hivi, nikilala huwa nakhoa mwanzoni ila usingizi ukigusa tu basi sikohoi mpaka usiku mwingine wa kulala. na hainichukui hata masaa mawili , ikizidi sana dakika 40 au 30 na siyo mfululizo , unakohoa kidogo kidogo tu.
Inawezekana umeota kinyama kwenye ulimi karibu na koo hivi huleta kikoozi kikavu sana ambacho usiku huwa ni kero sana.

Kina tabia ya kukulazimisha kusafisha Mara kwa Mara kabla ya kuongea, koo linakuwa kavu sana, na kupumua unapumua kwa shida
 

ISLETS

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2012
Messages
8,195
Points
2,000

ISLETS

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2012
8,195 2,000
Hii kitu sababu ameshapima pima sana...
Hapa madaktar wake wanashindwa kunyumbua Ukali wa kikohozi , wakat gan?? Na hii ya kifua kumuuma zaidi wakat amelala .
Ni TATIZO LA MOYO...
Mkuu usiseme walishindwa kunyambua tatizo maana hatujui huwa anajieleza vipi hospitali. Binafsi huwa sina shaka na daktari yeyote aliye-spend miaka 6 kwenye shule ya medicine kwenye vitu vidogo kama hivi.
Tatizo ni tunaoumwa ndio huwa hatutaki kutafuta msaada kwenye hospitali kubwa.
Though mi mwenyewe nimefikilia Pulmonary oedema maana iko typical kabisa ambapo one of the commonest cause ni Cardiac failure(right sided one) ambayo inaweza ikawa ni matokeo ya cor pulmonale or other chronic lung diseases including COPD kama wadau wengine walivyosema hapo juu.
Najua kilichowakwamisha madaktari ni vifaa/diagnostic tools ndio maana wakaishia kucheki makohozi, lakini pia hali ya uchumi, mtu mwingine ukimwambia kupima Xray 10000 au 20000 anaona hela kubwa sana anaona bora kupewa dawa bila kupima, mwisho wa siku watu wanakuja kudhani madaktari walishindwa kumtibu kumbe sio.
 

Gitarijosenga

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2019
Messages
289
Points
250

Gitarijosenga

JF-Expert Member
Joined Aug 3, 2019
289 250
Habari zenu Wapendwa , Natumai Mwaendelea Vema Na Kurudumu La Maisha Haya Ila Mie Kijana Mwenzenu Maradha Yameuteka Mwili Wangu.

HISTORIA YA UGONJWA WANGU ULIVYOANZA ...>

Nimekuja hapa mbele yenu ,nikiwa naeleza tatizo linalonisibu.

Tatizo langu :Kifua kinabana haswa muda wa kulala huwa nakohoa bila ya makohozi kutoka , tangia mwaka jana 2018 mwezi wa 11 , nilipata hitilafu hii mpaka leo sijawahi pona ..


Nimeenda mahospitalini anzia Mwadui hospital nimepima mpaka makohozi lkn hkn , nikaenda shinyanga government hospital sijawahi pata tiba zaidi ya doze , cetrizen ,sediton na amplicox pekee hapa ndo huwa naanza kupata nafuu ila dozee ikiisha huwa narudi katika hali yangu ya kukuhoa ,wapendwa nimemeza doze mpaka nikahisi mwili kuchoka kwa kutumia doze ... Imefika sehemu nikajikatia tamaa , kinachonishangaza kwann kbl sijalala kifua hakibani na kukohoakohoa hakuna ???!

Nikawaza labda ni UKIMWI , nikaenda hospital kupima ugonjwa huo nikakutwa mzima sina kabisa ..

Siku nyingine nikaenda kupima makohozi nikaambiwa niko salama kbs .

Ila kila nikilala nakohoa mnoo haswa pale usingizi unapokuwa umenikaba kama mida hii.

Nikapata mke wa mshikaji ambaye tupo nae kwenye ajira , akaona khali niliyonayo akanishauri nitumie ..............>>>>

LIMAO , MCHAICHAI NA SUKARI NIWE NAKUNYWA NITAPATA NAFUU KWELI ILINISAIDIA NA MPAKA SASA INANISAIDIA KIBAYA SIWEZI SINZIA BILA KUNYWA KIKOMBE KIMOJA ..

WADAU MSAADA WENU WA TIBA NIKO SHINYANGA HAPA MWADUI KWA SASA ..
NIMEKATA TAMAA KIJANA MWENZENU.

UKIONA U MZIMA BASI MSHUKURU MUNGU,PIA KABLA TATIZO HALIJAWA KUBWA BASI SHUGHULIKA NALO MAPEMA MAANA LIKIWA KUBWA ZAIDI YAWEZEKANA HATA GHARAMA ZA MATIBABU ZIKAWA JUU SANA..

KARIBUNI KWA USHAURI NA IKIWEZEKANA TIBA..
NI WENU MTIIFU..
Ashomile.. William.
Iyo ni TB kijana anza dozi mapema
 

King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,687
Points
2,000

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,687 2,000
Pole Sana mkuu.
Umejaribu kuangalia kama sio mazingira unayolala yanakuathiri? Labda vumbi, mto au godoro? Mfano ukisafiri hali inakua ile ile?

Ungeweza kutafuta family Dr ambae ni physician atakaekuhoji na kuangalia connection ya ugonjwa na historia yako. Kuna mmoja mzuri Sana ila Yuko dar. Ukipenda kumuona uje pm nikupe namba Yake.


Kila la kheri mkuu
 

Forum statistics

Threads 1,356,693
Members 518,934
Posts 33,135,551
Top