Naombeni ushauri wa namna ya kurudi Chuo baada ya kushindwa kuhudhuria kwa muda mrefu

Amon Lisa

JF-Expert Member
Nov 20, 2018
211
451
Nawasalimu wakubwa kwa wadogo.

Naandika kwa uchungu sana wakuu, kwanini maisha yamekuwa mateso kwangu hivi au nina mikosi na laana?

Mimi ni kijana wa miaka 22, jinsia Me.

Kitu ambacho nimemshukuru Mungu kunipa akili kiasi ya darasani ambayo kwa sasa ni bora upewe ya maisha.

Nilifanikiwa kufaulu level zangu vizuri, nilitokea shule za kata, Mungu ni mwema kwa ugumu nilifanikiwa kupata ufaulu mzuri O- level nikaenda kusoma A- level, moja ya shule za vipaji maalumu na Mungu hakunitupa nikapata kuchaguliwa University of Dar es salaam( UDSM).

Sasa sijui nimekosea wapi, tangu nimeanza mwaka wa pili ni mikosi tu, nilipata ajali nikapoteza uono kwa left eye, nilipata brain hemorrhage, Dah!

Sikuweza hata kujiandikisha na masomo ya mwaka wa pili, nilikuwa hospital tu. Mpaka September nikawa nimetengamaa kiasi.

Kinachoniumiza najua chuo sina kwakuwa sikutoa taarifa kipindi chote hicho.

Sasa hivi akili inanituma nikaombe chuo wanifikirie, sijui kama inawezekana.

Naombeni mnishauri ndugu zangu kwa michango yenu ya namna yoyote ile.

Ahsante.
 
Ukipata muda sikiliza ule wimbo wa harmonize unaitwa never give up.
Pole sana mkuu kwa maswahiba yaliyokukuta hizo changamoto zifanye kuwa fursa kwenye maisha yako. Nimewahi kusoma na bubu alikua hataki kuvaa uniform alisema yeye atavaa uniform ya gauni tu (joho).

Nikamuuliza kwanini hutaki kuvaa uniform? akasema kama wana jeuri wanaiongeleshe kwanini sijavaa uniform. Walimu hawawezi kumuongelesha kwa vitendo zaidi ya mwanafunzi anayemsaidia tu.
 
Pole sana mkuu. Mie siwezi kukushauri kitu cha maana kwa sababu shule nilikimbia kitambo hivyo sielewi taratibu zinavyoenda.

Lakini endapo una viambatisho vya hospitali vinavyoonyesha ulikua unaumwa, kwanini usiende kujaribu kuomba endapo unaweza sikilizwa? Hauna cha kupoteza kwa sasa, lakini ukifanikiwa utapata nafasi kuendelea na Chuo.
 
Nenda kwenye Idara au College husika zungumza nao uwe na ushahidi wa yale yaliyokukuta. Unaweza pia kuzungumza na Dean of Students huwa wana uzoefu wa kesi za aina hii. Watakuelekeza nini cha kufanya.

Kama milango imefungwa nenda TCU uone kama unaweza kuhamishia credit zako Chuo kingine ili uanze tena mwaka wa pili. kama hiyo ni ngumu fikiria uwezekano wa kujiunga na Open University.

Usikate tamaa. Huna mkosi wowote katika maisha watu hukumbana na mengi la msingi uwe na determination.
All the best.
 
Boss umesoma mwaka wa kwanza wote lakini hauna hata rafiki ambaye ungeweza kumwambia akuombee ruhusa chuo? Au ndugu yako ambaye angetoa taarifa Chuoni?

Mh boss kwakua siku hizi 'Mabrazamen' wamekua wengi kwenye menejimenti za vyuo naamini utafikiriwa.

Fight.
 
Back
Top Bottom