Naombeni ushauri wa kimawazo ili niweze kuwashauri wazazi wa mdogo wangu

Hazard CFC

JF-Expert Member
Apr 7, 2015
16,615
38,589
Dogo kamaliza form 4 kanyoosha 1 ya point 7.. dogo hataki tena kuendelea kuitumikia necta namaanisha hataki kuenda form 5 kusoma kwa kutumia mitaala ya necta, nataka kwenda international school of tanganyika (IST), uwezo wa kumpeleka huko wazazi wanao ila wanataka ushauri kwanza kabla hawajatimiza matakwa ya dogo.

Vipi wakuu wampeleke au dogo aendelee kupambana na necta?

IMG-20200114-WA0019.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wamsikilize msomaji yeye ndio anajua nini anataka ingawa sio vibaya pia kumpa ushauri kwanyinyi watu wake wa karibu maana ndio mnafahamu zaidi
 
Wamuche dogo akapige mtaala wa Cambridge....kama ameweza kunyoosha 1.7 necta, cambridge hawezi feli na huko ndo anapopataka atasoma vzr kwa sabab amependa mwny bila kulazimishwa
 
Kama wazazi wanampunga wa kumsomesha nashauri aachane na mitaala aende asomee maharifa zaidi kuanzia level ya diploma! Akasomee certified certificate either kwenye IT/ICT, Accounts, Medical, n.k kulingana na anachopenda atafanikiwa fasta
 
Mkuu mpelekeni akasome hapo IST upesi bila ya kupepesa macho, elimu na mitihani ya NECTA sehemu kubwa ni monotonous and repetitive ukiwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kukariri past papers utapata A zote 9. Mtaala unaotumiwa na IST na shule nyingine za kimataifa (save for normal english medium) utamfanya mtoto awe inquisitive and competitive.
 
Nimewaambia hvyo hvyo...huko necta ni elimu ya kukaririshwa unatoka ukiwa mweupe mnoo kichwani
Mkuu mpelekeni akasome hapo IST upesi bila ya kupepesa macho, elimu na mitihani ya NECTA sehemu kubwa ni monotonous and repetitive ukiwa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kukariri past papers utapata A zote 9. Mtaala unaotumiwa na IST na shule nyingine za kimataifa (save for normal english medium) utamfanya mtoto awe inquisitive and competitive.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja, aende akachome mafweza huko Tanganyika International School.

Mfumo wa bongo mbovu sana, unasota kusoma miaka mingi, ukimaliza unakuwa huwezi kutengeneza hata njiti ya kiberiti na ubaki jobless.
 
Back
Top Bottom