Naombeni ushauri wa haraka: Ndoa mwezi mmoja, mimba miezi miwili

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Habarini!

Niende kwenye mada.

Jamaa yangu wa mbali lakini niliye na uhusiano nae wa karibu kabisa kwa mambo mengi na msiri wangu mkuu alioa mwanzoni mwa mwezi uliopita, ilikuwa tarehe 2.

Leo asubuhi ya saa tano hivi alinijia nyumbani akiwa amefadhaika mno, nilistuka! Alichonieleza na ambacho nami kimenistua hadi kufikia kuomba msaada wa haraka humu ni kuwa ameenda na mke wake leo zahanati kumpima, baada ya kumuona hamuelewi elewi. Alimpima vipimo vyote, malaria na mimba. Kilichomshangaza ni kuwa mke ameonekana ana mimba ya mwezi mmoja na wiki tatu.

Alichonihoji: Je, atende lolote analoweza? (nafikiri mmenielewa hapa) Je, amwache? Akifanya hivyo aibu itakuwa ya nani hapa, mke au yeye? Awaite wazazi kusikia; watasemaje?

Kiufupi unaombwa msaada wa mawazo wa namna bora ya kulikabili jambo kama hili.

Mwenyewe jambo limenizidi maarifa, nilijifanya kumsihi atulie hadi nitakaporudi mizunguko yangu saa 2 usiku nitaongea naye kwa kirefu; ilifanya hivyo ili niweze kupata wasaa wa kuomba msaada humu wa kimawazo. Nimeileta humu hii mada sababu najua yeye hayupo humu.

Karibuni wadau!
 
anasema aliwahi lakini ni miezi kama 5 iliyopita, uchumba umedumu miezi 4.....hawajawahi kukutana katika kipindi hicho chote!
Simply hakuna kipimo kinachoweza kusema exactly umri wa mimba zaidi ultrasound inakadria tu afu pia dr atauliza mara ya mwisho period lini, Sasa hilo na kusema mimba ina mwezi na week tatu linahitaji evidance beyond dought .Busara inahitajika kufanya maamuzi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom