Naombeni ushauri wa biashara ya juice ya miwa, mtaji ni milioni 1-2

NEIMAA

Member
May 21, 2020
24
51
Habari za leo.

Naomba ushauri, nataka kufanya biashara ya juice ya miwa. Ni hivi sitaifanya mimi nitamuweka kijana afanye. Kwahiyo naomba ushauri juu ya hii biashara ikiwa itaweza kunilipa maana nachukua hela ya mkopo.

Nikiwa na maana kwamba biashara nitakayofanya naitegemea inipe rejesho. Mimi ni mwajiriwa ndio maana nasema nitahitaji nimuweke mtu. Naomba wadau mnishauri.

Nakaribisha mawazo yenu na ikiwa kuna mwenye biashara ambayo ni bora kuliko hii inayotumia mtaji mdogo na inalipa nitashukuru pia.

Nitashukuru kwa ushauri wenu najua mtanipa mawazo mazuri.

1621844734576.png

 
Mbona unamtishia mkuu,ingekuwa vizuri ungemshauri idea nyingine ya biashara kama iyo kwa upande wako unaona itamletea changamoto
Ukiona unataka kunzisha biashara fulani na huna kabisa idea nayo, na wala hujui sehemu sahihi ya kutafuta ideas, basi usianzishe. Na kama uking'ang'aniza kuanzisha, basi uwezekano wa kufeli ni mkubwa. Siku zote huwa nasema: ukitaka kuanzsiha biashara yoyote wewe ndiyo chanzo kikuu cha ideas za kuendesha ile biashara.

Kama utauliza basi utakuwa na kujazia tu hapa na pale. Na ili uwe chanzo cha ideas huna budi kufanya research ya kiwango cha juu kwenye biashara unayotakiwa kufanya. Na research kwa kiasi kikubwa hufanyika ''site''.

Ila watanzania tulivyo wavivu, tunataka tuanzishe biashara kwa kutumia uzoefu wa kusoma thread ya JF. Kumbuka: sikusema kuwa kuulizia ni kubaya, ila nimesema mawazo yako ndiyo yanabeba 90% ya mkakati wa biashara. Ni hayo tu.
 
kweli mkuu,kwani unataka kufanyia iyo biashara mkoa gani...ushapata location??ingawa sio mzoefu sana wa biashara,ukinijibu hayo maswali naweza pata cha kukushauri
Dar na kuna sehemu ambayo nimeitarget kwasababu kuna muingiliano mkubwa wa watu, sehemu ambayo naimani kwamba ni rahisi kuuza.
 
Ukiona unataka kunzisha biashara fulani na huna kabisa idea nayo, na wala hujui sehemu sahihi ya kutafuta ideas, basi usianzishe. Na kama uking'ang'aniza kuanzisha, basi uwezekano wa kufeli ni mkubwa. Siku zote huwa nasema: ukitaka kuanzsiha biashara yoyote wewe ndiyo chanzo kikuu cha ideas za kuendesha ile biashara. Kama utauliza basi utakuwa na kujazia tu hapa na pale. Na ili uwe chanzo cha ideas huna budi kufanya research ya kiwango cha juu kwenye biashara unayotakiwa kufanya. Na research kwa kiasi kikubwa hufanyika ''site''. Ila watanzania tulivyo wavivu, tunataka tuanzishe biashara kwa kutumia uzoefu wa kusoma thread ya JF. Kumbuka: sikusema kuwa kuulizia ni kubaya, ila nimesema mawazo yako ndiyo yanabeba 90% ya mkakati wa biashara. Ni hayo tu.
Si kwamba sina idea kabisa,ndio maana nimesema nataka kufanya biashara flani, ina maana naona kwamba ni kitu ambacho kinaweza kunipa hatua, ninapokuja hapa tupo watu wengi humu na tuna ufahamu na experience tofauti hasa kwa mm ambaye nimesema ni mwajiliwa.

Najua kabisa biashara ili ifanikiwe inahitaji usimamizi na ufatiliaji wa karibu sn, kwakuwa muda wangu si mkubwa wakuweza kuisimamia ndio maana natafuta biashara ambayo haitanihitaji kutoa macho yangu muda wote,napatana na kijana kwamba kila siku utanipatia kiasi fulani,mm ntamsimamia lkn si ktk ukaribu ambao angekuwa nao ambae yupo wakati wote.
 
Jaribu kuwekeza kwenye cryptocurrency trading baada ya kupata mafunzo online kwa miezi mitatu tu

Povu ruksa
 
Si kwamba sina idea kabisa,ndio maana nimesema nataka kufanya biashara flani, ina maana naona kwamba ni kitu ambacho kinaweza kunipa hatua, ninapokuja hapa tupo watu wengi humu na tuna ufahamu na experience tofauti hasa kwa mm ambaye nimesema ni mwajiliwa, najua kabisa biashara ili ifanikiwe inahitaji usimamizi na ufatiliaji wa karibu sn, kwakuwa muda wangu si mkubwa wakuweza kuisimamia ndio maana natafuta biashara ambayo haitanihitaji kutoa macho yangu muda wote,napatana na kijana kwamba kila siku utanipatia kiasi fulani,mm ntamsimamia lkn si ktk ukaribu ambao angekuwa nao ambae yupo wakati wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante. Lakini ulivyouliza inaonyesha kabisa huna abc za hiyo biashara. Na mimi nilikuwa nakupa tu angalizo. Kila la heri lakini ukifanikiwa kuanzisha kwa kutumia ideas utakazozipata hapa bila wewe ku-contribute kwa asilimia 90 basi haitakuchukuwa muda kugundua kwamba pengine mimi ndiyo nimekupa idea nzuri sana.
 
Ukiona unataka kunzisha biashara fulani na huna kabisa idea nayo, na wala hujui sehemu sahihi ya kutafuta ideas, basi usianzishe. Na kama uking'ang'aniza kuanzisha, basi uwezekano wa kufeli ni mkubwa. Siku zote huwa nasema: ukitaka kuanzsiha biashara yoyote wewe ndiyo chanzo kikuu cha ideas za kuendesha ile biashara. Kama utauliza basi utakuwa na kujazia tu hapa na pale. Na ili uwe chanzo cha ideas huna budi kufanya research ya kiwango cha juu kwenye biashara unayotakiwa kufanya. Na research kwa kiasi kikubwa hufanyika ''site''. Ila watanzania tulivyo wavivu, tunataka tuanzishe biashara kwa kutumia uzoefu wa kusoma thread ya JF. Kumbuka: sikusema kuwa kuulizia ni kubaya, ila nimesema mawazo yako ndiyo yanabeba 90% ya mkakati wa biashara. Ni hayo tu.


Siku zote kwenye jukwaa hizi unachoandika na mm ndo huwa nakisemea moyoni mwangy! Huku unakuja kujazilizia tu kama 10%! La sivyo utashindwa mapema sana!
 
Dar na kuna sehemu ambayo nimeitarget kwasababu kuna muingiliano mkubwa wa watu, sehemu ambayo naimani kwamba ni rahisi kuuza.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Dar mkuu nauhakika ni sehemu sahihi...cha msingi usirudi nyuma kama akili ishakutuma kufanya iyo biashara kinachotakiwa ni kuanza tu utekelezaji...make sure iyo sehemu kama kuna muingiliano wa watu,kwa pembeni ya biashara yako kama kuna nafasi weka hata mabenchi mawili na drafti/bao watu wawe wanacheza na draft/bao pembeni...iyo itakuongezea wateja...

But zingatia usafi usafi usafi mkuu....ukifanikiwa kufungua kama utakuwa interested usisite kuni alert pamoja na wadau wengine humu tunaweza kukushauri na vitu vingine unavyoweza kuviongezea kwenye biashara yako sababu wakati mwingine biashara moja inaweza zalisha biashara nyingine...kila la kheri mkuu.
 
Mie naogopa kukushauri watakuja manguli watasema hee na hii unaijua😆!..lakini kifupijuice ya miwa=popcorn ...! Sijui kama bado watu wanakimbilia miwa pale kariakoo gerezani dadek maisha haya!..imepoa!

Kidogo nitenguke kiuno kugombea miwa😇! Tena kama unamkabidhi mtu atauza atakuwa anakupa za glass kumi tu !
all the best
 
Mkuu kama vipi fikiria biashara ambayo utaweza kuwapa madogo wakuuzie mtaani wakati wewe ukiwa kibaruani kwako halafu usiku hesabu.
 
Siku zote kwenye jukwaa hizi unachoandika na mm ndo huwa nakisemea moyoni mwangy! Huku unakuja kujazilizia tu kama 10%! La sivyo utashindwa mapema sana!
Kweli kabisa mkuu. Wengi hawajui kuwa ''mtaji wa mawazo'' ni muhimu kuliko hata ''mtaji wa fedha''. Na mtaji wa mawazo kama ulivyo mtaji wa fedha chanzo chake ni wewe mwanzisha biashara mwenyewe.

Kama ambavyo huwezi kutegemea watu kwenye kupata mtaji wa fedha basi hata kwenye mtaji wa mawazo huwezi kuwategea.
 
Nenda maeneo ya rufiji karibu na MTO kodi eneo hapo ,kuna ile mbegu bora ya matikiti ,ukimwaga hapo mche 1 unatoa tikiti zaidi ya 200 Nina uhakika ukilima hekari angalau 2 utapata matikiti ya kutosha ukipekeka sokoni huko m 5 mpaka 7
 
Back
Top Bottom