Naombeni ushauri vyakula gani vinasaidia kuongeza maziwa

farajamlenga

Member
Dec 8, 2017
47
125
Naomba kueleweshwa ni vyakula gani ambavyo nikila vitasaidia kuongeza maziwa

Ninamtoto wa miezi miwili na wiki moja, maziwa yangu yanatoka kidogo sana hivyo naona kama hayatoshi na mtoto hashibi, nimesha tumia sana uji uliowekwa pilipili manga pamoja na matetele ya maboga lakini hayajanisaidia

Pia naombeni ushauri ni maziwa gani yanayofaa kwa mtoto Mdogo ili niweze kumpa akifikisha miezi mitatu muda ambao Mimi itabidi nirudi kazini

Nashukuru wote mtakao nipa ushauri
 

La gioconda

JF-Expert Member
Nov 30, 2015
404
1,000
Supu ya samaki, uji wa lishe,supu ya utumbo changanya na viazi, juis ya karoti,mbogamboga,maziwa ya mtindi,pendelea kunywa maji kwa wingi kutafuna karanga au korosho,mchemsho wa nyama na ndizi bukoba
 

Norshad

JF-Expert Member
Jun 3, 2013
4,524
2,000
yatakuwa yapo mbali, mpe babayake ayavute karibu....yupo mdada hapo juu kisha kusaidia we fuata maelekezo
 

minji

JF-Expert Member
Sep 2, 2016
2,244
2,000
Unateseka nini kuna watu hawajui kama maji yanaongeza maziwa kwa kasi sana jitahid kula ushibe kunywa maji mengi kila muda utakuja sema ninanyonyesha ndivyo ninavyofanya sbb uji huwa unanichosha mapema kuna docta mmoja alinishauri sio sir sikuamin ila nilipojaribu nilikubali
 

Honey Faith

JF-Expert Member
Aug 21, 2013
15,802
2,000
Pika uji uwe unaweka pilipili manga yakutosha wanadai inavuta na kuongeza maziwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom