Naombeni ushauri, usajili wa jina NECTA

mamanzara

JF-Expert Member
Oct 9, 2007
651
195
Wakuu kuna jambo limepitia kwangu na limenitatiza na hivyo naomba ushauri na maoni yenu.

Kuna kijana ambaye yuko kidato cha nne mwaka huu. Kijana huyo jina lake ni Ayubu Bakari Selemani na ndilo alilosajiliwa shule tangu darasa la kwanza. Jina la baba yake ni Bakari Selemani na mama yake ni Bahati Athumani.

Tatizo lilianzia kwenye usajili wa mitihani ya kidato cha pili. Matokeo yalipotoka yalitoka kwa jina la Ayubu Bahati Selemani, haieleweki nini kilitokea katika usajili huo. Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita wanafunzi wa kidato cha nne walitakiwa kujisajili kwa ajili ya mitihani ya NECTA na alipotaka kurekebisha jina lake, Mkuu wa Shule alikataa kwa kigezo kwamba haitawezekana kubadilisha jina kwa vile lilishakuwa kwenye mtandao hivyo akibadilisha anaweza asitambulike na hivyo asipate namba ya mtihani.

Tatizo ninaloliona mimi ni kwamba jina halisi la kijana ndilo lililoko kwenye cheti chake cha kuzaliwa na aliojisajili kwenye vitambulisho vya taifa na hata shule tangu awali mpaka sasa,kwa hiyo endapo cheti chake cha kidato cha nne kitatoka na jina tofauti itamsumbua katika safari yake ya kimasomo hapo baadae.

Kama ni kweli hili haliwezekani basi vile vile kwa maoni yangu nafikiri mtandao wa NECTA nao pia hauko sahihi kwa maana usajili wa mtoto shule ni Ayubu Bakari Selemani, ni vipi jina jipya likajitokeza ambalo haliko kokote na kwamba isiwezekane kulisahihisa hivyo libakie kwenye kumbukumbu za NECTA?? Hili mnalionaje?

Naomba ushauri/maoni yenu tafadhali.
 
lazima hilo jina la bahati alilitumia kwenye usahili kidato cha pili ndo maana limekuwa hvo mbaka usahili k4 wangelipata wapi? pole kwa tatizo
 
mkuu wa shule kambania tu.. uwezekano wa kubadilisha ulikuwepo tangu mapema,kwa sasa hawezi hivyo afanye kwanza necta..
matokeo yakitoka na kupata vyeti vyote ndio aende baraza kuomba kubadilisha jina kwenye vyeti.. inawezekana kabisa.
 
Angekua form3 angeenda mahakamani akaapa kukana jina la kwanza na kutambua jina la pili kisha anapeleka shule mkuu anatangaza ktk mbao na anaambatanisha ktk file megine zaid huko sjui (mimi nilifanya hivyo)nilipokuwa nasoma
 
mkuu wa shule kambania tu.. uwezekano wa kubadilisha ulikuwepo tangu mapema,kwa sasa hawezi hivyo afanye kwanza necta..
matokeo yakitoka na kupata vyeti vyote ndio aende baraza kuomba kubadilisha jina kwenye vyeti.. inawezekana kabisa.
Asante kwa ushauri Mkuu.
 
Back
Top Bottom