Naombeni ushauri, nimempa hela nusu na kiwanja kamuuzia mtu mwingine

Emma mwa

Member
Aug 23, 2017
21
20
Jamani naombeni ushauri

Kuna jamaa mmoja aliniuzia kiwanja mwaka jana mwezi wa kumi

Wakati tunauziana sikuwa na hela yote hivyo nilimlipa niliyokuwa nayo Tshilingi milioni moja jumla ilikuwa nimpe milioni moja na laki nane hivyo ikawa imebaki laki nane kumalizia tukakubaliana nimalizie baada ya mwezi mmoja lakini sikufanikiwa baadae nikaanza kuuguza nikaongea naye akasema basi ukipata utanipa aliondoka mwezi wa kumi na mbili simu ikawa haipatikani na Mimi nimeuguza mpaka mwezi wa pili kuelekea wa tatu

Sasa jana ndio nimeonana naye nikamwambia jamaa vipi akaniambia safi nikamwambia kuna mazao nataka niuze mwezi huu mwishoni nimalizie ile hela akasema iache maana kiwanja nilishauza kwa sababu niliona unanichelewesha kumaliza shida yangu nikamuuliza kwa hiyo hela niliyokuwa nimeilipia tunafanyaje kama umeuza ? Akasema nisubiri mwezi huu uishe kisha tuonane

Naomba ushauri wenu kama kuna anayejua sheria juu ya hilo kwamba inatakiwa iwaje anisaidie jamani
Naomba kuwasilisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati mnauziana mliandikishana? Na masharti ya kumalizia deni lililobaki yalikuwaje kwenye mkataba pindi usipolipa kwa muda muliowekeana kummalizia? Mikataba mingi usipolipa kwa kipindi mlichokubaliana anakurudishia hela yako kwa kukata 30% ya usumbufu. Lakini yote lazima yawe yameandikwa kwenye mkataba. Kwa vyovyote vile ushahidi!!
 
Kama hamna maandishi, hauna cha kumfanya kwa kutumia sheria za duniani.
Hivyo usijisumbue akikataa nenda kasalimie wazee.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata kama maandishi yapo hayo maandishi si yatasema anatakiwa kumalizia laki nane ndani ya mwezi.

Na hajamalizia.

Akasogeza muda, kama mkataba haujasema juu ya muda wa malipo kuongezwa maandishia hayana msaada.
 
Hata kama umepitisha muda alitakiwa kukueleza kwasababu ameshachukua pesa nusu na hakutakiwa kuuza mpaka akurudishie pesa zako ulizotoa. Huyo amefanya dharau na uhuni ungalikua unamuweza ungalimpa vitasa kwanza ndio muende kwenye sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba, muuzaji atakuwa na haki ya kuuza kiwanja husika pasipo kutoa taarifa kwa mnunuzi endapo mnunuzi atashindwa kulipa malipo ya awamu ya pili kwa wakati na kusababisha usumbufu kwa muuzaji.

JE KIFUNGU KAMA HICHO MLIWEKA KATIKA MKATABA WENU WA MAUZIANO ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
daaaa, m naumiaga sana nikiona mtu analizwaaa, watu wamekua waajabu sana siku hizi, usimwamin mtu kbsaaaa,

hapo hakuna kingne ni tamaaa tuu, na pengne hata mwanzo hakua na nia mbaya ila tamaa ikamjia,
huyo nenda nae kibabe wala kinyongee, mdai kama kwa njia ya kawaida tuu, huku ukimsoma je ni mlipaji au sio, baada ya hapo ndio ubadilishe mbinu,

TAMAA MBAYA SANA,
 
Hapo sio tamaa mkuu, mwenye makossa ni huyo mnuuzi wa kiwanja aombe mungu jamaa awe mstaarabu amrudishie pesa yake, vinginevyo kisheria hana la kufanya , makubaliano lazima yaheshimiwe na pande zote
 
Hata kama umepitisha muda alitakiwa kukueleza kwasababu ameshachukua pesa nusu na hakutakiwa kuuza mpaka akurudishie pesa zako ulizotoa. Huyo amefanya dharau na uhuni ungalikua unamuweza ungalimpa vitasa kwanza ndio muende kwenye sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ww unafikiri hajamwambia ? mawasiliano yalikuwepo hapo , huwezi jua muuzaji naye alikuwa na shida gani na hiyo pesa
 
Wakati mnauziana mliandikishana? Na masharti ya kumalizia deni lililobaki yalikuwaje kwenye mkataba pindi usipolipa kwa muda muliowekeana kummalizia? Mikataba mingi usipolipa kwa kipindi mlichokubaliana anakurudishia hela yako kwa kukata 30% ya usumbufu. Lakini yote lazima yawe yameandikwa kwenye mkataba. Kwa vyovyote vile ushahidi!!
Masharti hatukuandikishiana nikichelewa kulipa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kama umepitisha muda alitakiwa kukueleza kwasababu ameshachukua pesa nusu na hakutakiwa kuuza mpaka akurudishie pesa zako ulizotoa. Huyo amefanya dharau na uhuni ungalikua unamuweza ungalimpa vitasa kwanza ndio muende kwenye sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
Anachojidai ni kwamba anafahamiana na baadhi ya viongozi wa askari kama OCD, OCS na askari wa vyeo vidogo na kuna ambao nao amewauzia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom