Naombeni ushauri, nimempa hela nusu na kiwanja kamuuzia mtu mwingine

Jamani naombeni ushauri
Kuna jamaa mmoja aliniuzia kiwanja mwaka jana mwezi wa kumi
Wakati tunauziana sikuwa na hela yote hivyo nilimlipa niliyokuwa nayo Tshilingi milioni moja jumla ilikuwa nimpe milioni moja na laki nane hivyo ikawa imebaki laki nane kumalizia tukakubaliana nimalizie baada ya mwezi mmoja lakini sikufanikiwa baadae nikaanza kuuguza nikaongea naye akasema basi ukipata utanipa aliondoka mwezi wa kumi na mbili simu ikawa haipatikani na Mimi nimeuguza mpaka mwezi wa pili kuelekea wa tatu
Sasa jana ndio nimeonana naye nikamwambia jamaa vipi akaniambia safi nikamwambia kuna mazao nataka niuze mwezi huu mwishoni nimalizie ile hela akasema iache maana kiwanja nilishauza kwa sababu niliona unanichelewesha kumaliza shida yangu nikamuuliza kwa hiyo hela niliyokuwa nimeilipia tunafanyaje kama umeuza ? Akasema nisubiri mwezi huu uishe kisha tuonane
Naomba ushauri wenu kama kuna anayejua sheria juu ya hilo kwamba inatakiwa iwaje anisaidie jamani
Naomba kuwasilisha
Sent using Jamii Forums mobile app
Kubali tu upewe pesa yako kesi iishe kimya kimya mkuu
 
Hahaha mmekutana wote HAMNA SUBIRA. Wewe ulipochelewa kumalizia pesa mliyokubaliana hakukusubiri na hakukutafuta kufahamu kulikoni, akauza.
Yeye kakwambia "subiria mwezi huu uishe ndio muonane" wewe umeshapanik unatafuta ushauri, kwanini usisubiri ukaona itakuaje?! Hajasema hakulipi na alichosema subiria mwisho wa mwezi huu, kama alikua na shida genuine na pesa zilimsaidia kupata ufumbuzi wa matatizo yake kwa pesa uliyompa na aliyopewa huko kwingine, atakulipa.
Inawezekan kule nako hakupewa zote naye anasubiria mwisho wa mwezi huu, ili akilipwa ahamishe deni. Hivyo kuwa na subira kwanza.
 
Rules of 'acceptance' in contract law zinasema introduction of a 'counter offer' makes the existing contract voidable

Kama makubaliano yalikuwa ulipe ndani ya mwezi na ukufanya ivyo umevunja mkataba kisheria, ata ungepiga simu ndani ya huo mwezi kabla siku azijaisha kuomba usogezewe siku tayari ushavunja mkataba (ana haki ya kuuza) utakiwi kubadili makubaliano mliyowekeana ata kwa mdomo.
 
KOSA NI LAKO MWENYEWE, KUUGULIWA KWAKO YEYE HAKUMUHUSU, HAYO NI MAMBO YA FAMILIA YAKO, ULIPASWA ULIPE DENI KADRI MLIVYOKUBALIANA..

Pia Umesema alikuongeza MUDA Lakini hata MUDA aliokuongezea bado pia hukuukamilisha na Wala hukuhangaika kumtafuta.
 
Mbaka hapo huyo jamaa ni tapeli anatakiwa akurudishie pesa zako
Kibinaadam kama yeye aliuza kwa kuwa alikuwa na matatizo, baaada ya kuuza tu kwa mtu mwingine angekupigia simu
Bwana mkubwa umeshindwa kunimaliza kwa wakati, kiwanja nimeuza kwa mtu mwingine hivyo basi njoo uchukue haki yako, yaani angetemesha mzigo lakini kinyume chake yeye alikaa kimya kana kwamba anakumudu kivyovyote vile
Ukijifanya mpole sana na ngumi atakupiga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HUYO NITAPELI MAANA KAMA UNGEPANDA MAZAO NAYO ANGEYAUZA?
JEE MLIANDIKIANA?KAMA AMEUZA ZAIDI YA PESA ALIYOKUUZIA WEWE ANGETAKIWA KISTAARABU AKURUDISHIE PESA ULIYOLIPA.KAMA MLIANDIKIANA ANATAKIWA AKAMATWE MAANA AMEUZA MALI YAKO.
 
daaaa, m naumiaga sana nikiona mtu analizwaaa, watu wamekua waajabu sana siku hizi, usimwamin mtu kbsaaaa,

hapo hakuna kingne ni tamaaa tuu, na pengne hata mwanzo hakua na nia mbaya ila tamaa ikamjia,
huyo nenda nae kibabe wala kinyongee, mdai kama kwa njia ya kawaida tuu, huku ukimsoma je ni mlipaji au sio, baada ya hapo ndio ubadilishe mbinu,

TAMAA MBAYA SANA,
Sidhani hapo kuna tamaa. Makubaliano ni makubaliona. Hii ni sawa na kukopa benki au taasisi yoyote. Mkikubaliana lazima makubaliano yaheshimike, hata kama. Kama makubaliano yamekikiukwa ni lazima haki itendeke. Kama makubaliano hayana masharti mengione zaidi ya muda, muda ukifika mwenye kiwanja anaweza kukiuza. Lakini mwenye kiwanja anatakiwa ajuwe anatakiwa kurudisha pesa ya mnunuzi.
 
Kesi kama hii ilishawahi kumtokea jamaa yangu, ushauri niliyompa nilimwambia atafute fundi waende nae site wapige msingi hata wa chumba kimoja, baada ya hapo yule aliouziwa mara ya pili ndio akaanza kuhaha na kumfosi jamaa aliemuuzia amlipe jamaa yangu au la sivyo amrudishie yeye pesa yake, haikuchukua hata wiki jamaa akalipwa pesa yake yote na gharama aliyotumia kujenga msingi.
 
Back
Top Bottom