Naombeni ushauri nifanye nini ili nisipoteze hela zangu nilizowekeza Kenya

Asee,pole ndugu,kwani Kenya Wana simu nzuri au rahisi kushinda sisi?,mbona hapa kwetu zpo simu bomba tu au Kama ni kuagiza ungeagiza nje ya Afrika ndugu...
 
Wabongo some time kwa kupenda uzumgu wa kuiga ni tatizo ni simu gani ambayo bongo ungeitaka ukaikosa ukaipata kenya tu? Ukitaka kuagiza online bora uagize na kampuni kubwa kama Alibaba na zinginezo otherwise unapigwa tu
 
Sijaona sababu ya kumshambulia zaidi ya kutoa solution. Kumbuka kwa kesi kama hii kila upande Wana wasiwasi. Muuzaji anaogopa endapo atatuma simu na mnunuzi asilipe hiyo nusu itakuwaje?
Zamani kidogo, katika biashara za kimataifa, tatizo kama hili lilikuwa linamalizwa na benk za nchi zote mbili. Mnunuzi anaweka pesa benki na muuzaji anatuma mzigo. Mnunuzi akishapokea mzigo na kuridhika, pesa inaachiwa.
Kuna kitu kinaitwa letter of credit. Terms na condition zinaelezwa
 
Jf imekuwa ya ajabu sana,mtu anaomba ushauri kwa ajuaye lakini vilaza wanakazana kumwambia kapigwa. Kama hujui kitu kwa nini usipite kimya kimya, unaweza kuwa na la kujifunza pia.
 
Jf imekuwa ya ajabu sana,mtu anaomba ushauri kwa ajuaye lakini vilaza wanakazana kumwambia kapigwa. Kama hujui kitu kwa nini usipite kimya kimya, unaweza kuwa na la kujifunza pia.
Huo ni uhakika kapigwa...

Kama anabisha atuambie aliagiza kwa kampuni au jina la hilo duka huko Kenya.
 
Huo ni uhakika kapigwa...

Kama anabisha atuambie aliagiza kwa kampuni au jina la hilo duka huko Kenya.

Mkuu hata mtoa mada anaamini chances za kupigwa zipo nyingi tu,anachotaka hapa ni mtu ambaye alishawahi kukutana na hiyo issue. Sasa waswahili kawaida yetu kutwa kujifariji kwa matatizo ya wengine,kapigwa kapigwa......
 
Ok sawa, sio shida maadam nina mikono na afya nitapambana nitafute hela niliyoibiwa. Je kuna namna ya kufanya ili ku recover au kuzuia wengine wasiingie kwenye utapeli huu?
Waanike hao jamaa mtandaoni ili wajulikane.
 
Naombeni ushauri wa nini cha kufanya kwa haraka ili nisipoteze hela ambazo nimezituma kwa a Company in Kenya nimefanya manunuzi ya simu. Katika makubaliano ilikuwa kwamba nilipe advance/deposit ya 50% cost ya simu ili waweze kuituma na nikishaipokea hapa Dar nitalipa balance 50% iliyobaki. Sasa mimi nikafanya kama tulivyokubaliana nikapewa namba ya mpesa nikafanya international transfer na fedha ikapokelewa vizuri na huyu supplier.

Sasa baada ya muda kidogo ananiambia kuwa ili mzigo wangu upelekwe airport niweze kupokea leo Boss wake amemwambia ni lazima nilipe hela yote yaani 100% jambo ambalo limenishtua kwavile 1. Sio makubaliano yetu but 2. Siwezi kuwaamini tena, kama hiyo 50% niliyolipa advance wamebadili terms za biashara je nikimalizia balance nina uhakika gani kuwa nitatumiwa mzigo wangu? Huyu jamaa ananisisitiza nitume hela chap ili mzigo upakiwe kwenye ndege. Kwakweli nimeshtuka nimeamua kutokutuma mpaka wanieleze sababu za kubadilisha terms of business katikati ya process

Ambao mmeshafanya transactions hizi naomba ushauri wa haraka nifanye nini ili nipate either hela zangu au wanipe mzigo wangu kama tulivtokubaliana na ukishafika hapa Dar mimi nipo tayari kulipa balance cash. Maana hayo ndio yalikuwa makubaliano yetu. Nimejaribu kurudisha muamala kwa Mpesa naona mesg inakuja 'transaction failed'

Naomba ushauri wenu kwa haraka ili nisipoteze hela
Lete full details za hiyo kampuni na ni kiasi gani cha pesa umewatumia ili nikueleze uende wapi utapata msaada sahihi na pesa yako utaipata kama kweli ulideal na kampuni ambayo inatambulika Kenya, na siyo briefcase company.
 
Back
Top Bottom