LadyRed
JF-Expert Member
- Mar 19, 2016
- 9,636
- 11,446
U nailed it..asipoelewa hapa basi tenaKwa kifupi unaweza kuwa na viza lakini ukishia airport na kupanda ndege hiyo hiyo iliyokubeba kurudi nayo iwapo utatiliwa shaka,kwani kuna viswali huulizwa kabla hujagongewa muhuriwa kuruhusiwa kuingia,pia jua digrii yako ya Bongo hakuna anayeijua huko Marekani na mwisho hadi kuja kufanikiwa Marekani inachukua miaka, na Marekani si lelemama kama wengi tunavyodhani huku au tunavyoangalia kwenye FB ,na kwa hali ya mtawala wa sasa aliyepo kwenye jengo jeupe,sidhani kama ni jambo jema kupiga kambi Marekani na kwa sasa sijui hata nafasi za kusomea unesi kama zipo kama ilivyokuwa awali,kwa wengi ukiwa nesi angalau ndio unakuwa na maisha ya uhakika au uwe na skills za kufa mtu ndio mfumo ukuhitaji, na mwisho kaka bila makaratasi utaishia kuuza maji mitaani kwa pesa ndogo. Ni bora uende ukaangalie na urudi tu ,hapa Bongo ni peponi kulinganisha na huko unakotaka kuzamia,maisha si rahisi kama wengi tunavyodhani,Marekani hakuna cha mjomba wala kwenda kuchimba mhogo shambani,usipofanya kazi/kibarua jua hutakuwa na sehemu ya kulala wala kula,yes kila kitu kipo lakini kila kitu ni pesa.Nenda kajionee mwenyewe halafu uje utuambie hapa,lakini jua moja tu huko utaenda kupigika kweli kweli, na utaikumbuka Bongo.Nimeandika kwa uzoefu nilionao wa kuishi Marekani japo si kwa muda mrefu,ikabidi ni Uturn asap.