Naombeni ushauri, namna ya kumsahau mume wangu aliyefariki

shavada

Member
Oct 21, 2017
11
7
Naombeni ushauri namna ya kuepukana na hili tatizo,

Mume wangu alipata ajali na kufariki mwanzoni mwa mwaka huu huku akiniacha nikiwa na ujauzito wa miezi miwili, tangu kitokee kifo cha mume wangu nimekuwa na msongo wa mawazo, nimekuwa nikikosa usingizi muda mwingi usiku nakuwa macho, muda wote ninaokuwa macho nakuwa namfikiria tu marehemu mume wangu na hii hali huwa inanitokea hata mchana pia, usiku nikibahatisha kupata usingizi ninamuota pia.

Nimekuwa mtu wa kukosa furaha na kuwa na huzuni muda wote, muda mwingi nikiwa pekeyangu najikuta tu nalia, sipendi kukaa na watu au kuwa kwenye mkusanyiko wa watu wengi na pia najihisi hata utendaji kazi wangu kazini haupo sawa kwani nakuwa na hasira hata mtu akikosea kitu kidogo.

Nilifikiri labda nilijifungua tatizo hili litaisha kwakuwa mtoto atanifariji, namshukuru Mungu nilijifungua salama mwezi uliopita lakini mtoto amefanana sana na babake, kila ninapo mwona mtoto wangu namkumbuka baba yake nakuanza kufikiria vitu vingi na mawazo ndiyo yameongezeka zaidi.

Ninatamani kuwa na amani kama zamani ila nashindwa, naombeni ushauri namna ya kuepukana na hili tatizo na kama wapo hapa waliowahipatwa na tatizo hili naomba wanishauri jinsi walivyoweza kulimaliza.

Nashukuru kwa wote watakaonishauri
 
Mkuu me nakupa pole sana natumai utapata majibu ya kutatua tatizo lako na kukufariji pia..
Kila LA kheri
 
Pole sana dear either atafute washauri wa saikolojia wakusaidie ila jaribu kukaa na watu na kujichanganya pia. Niliona rafiki yangu Mme alianguka ghafla na kufariki wakijiandaa kwenda kanisani. Baada ya kuzika mdogo wake tumbo moja na Dada wa Mme wake walikuja kukaa nae. Aliachiwa watt wawili 7 and 5 years, but ilfka mahali alikuwa analalamika na mdogo wake na sisi kama marafiki Mara nyingi tulikuwa tunamtoa out, au tunamtembelea but ame recover now though ilichukua muda. Unahitaji sana support ya marafiki na familia
 
Pole kwa kufiwa na mumeo,
kifo ni faradhi sote tutakufa kutangulia tu ndio kugumu, yakubali yote kua ameshafariki hatorudi hutamuona tena kubali hayo. Fungua moyo wako usiukunje kwa majonzi ahadi yake ilifika na sote tuko njiani hatujui saa wala dakika. Penda sana kujikusanya na watu epuka kukaa peke yako muda ambao unaona ni vyema ukawa unajihusisha na watu mbadilishane mawazo mtoto wako ndio faraja yako atakua na kukupa furaha ambayo kwa sasa huioni

Muombe sana Mungu akupe subra, akupe tahfif na shifaa kipindi hiki kigumu na akujaalie moyo wa kuyaona ya kawaida hayo jitahidi najua unaweza please be strong!!
 
POLE SANA DADA

WAHENGA WANASEMA, UKITAKA KUJUA UCHUNGU WA KUFIWA BS AFE MUME/MKE ULIYEPENDANA SANA.


1. KUBALI HALI HALISI KUWA MUMEO AMEFARIKI NA KIFO NI SEHEMU YA MAISHA YA MWANADAMU YEYOTE.
2. JITAHIDI KUWA KARIBU NA MARAFIKI, NDUGU NA JAMAA, USIPENDE KUKAA PEKE YAKO IKIWEZEKANA HAMIA KWA WAZAZI WAKO AU NDUGU ZAKO UWE NAO KARIBU
3. KUWA KARIBU NA MUNGU NA UMWOMBEE MUMEO APUMZIKE KWA AMANI
4. JIAMINI KUWA BILA MUMEO KIMWILI, MAISHA YAPO. AMINI KUWA UPO NAYE KIROHO NA KWAMBA YALIYOTOKEA NI MIPANGO YA MUNGU NA WEWE SYO WA KWANZA

NB. SISITIZA KUJICHANGANYA NA WATU USIPENDE KUKAA PEKE YAKO
 
Mitihani tumeumbiwa binadamu, Vifo vya Wapendwa wetu ni moja ya mitihani ya duniani hivyo Pamoja na kutuachia Majonzi lakini inabidi ifike kipindi ukubali kuwa hilo jambo limetokea na ni lazima litokee kwa kila Mwanadamu.., unapokubali kuwa hilo jambo limetokea inakupelekea ww kuendelea na mapambano ya Maisha na hatimae kupunguza lile gap la changamoto za Maisha ambazo pia zinakusababishia Msongo wa Mawazo!!!
 
Pole sana dear either atafute washauri wa saikolojia wakusaidie ila jaribu kukaa na watu na kujichanganya pia. Niliona rafiki yangu Mme alianguka ghafla na kufariki wakijiandaa kwenda kanisani. Baada ya kuzika mdogo wake tumbo moja na Dada wa Mme wake walikuja kukaa nae. Aliachiwa watt wawili 7 and 5 years, but ilfka mahali alikuwa analalamika na mdogo wake na sisi kama marafiki Mara nyingi tulikuwa tunamtoa out, au tunamtembelea but ame recover now though ilichukua muda. Unahitaji sana support ya marafiki na familia
USHAURI MZURI
 
Pole mkuu...haya yote ni maisha...omba Mungu...uzuri tumeumbiwa kusahau..ipo siku utarudia hali yako ya zamani ukiwa na furaha tele..nakuombea pia
 
Nawashukuru sana wote mlionishauri na watakaoenelea kunishauri ushauri wote nitaufanyia kazi
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom