Naombeni ushauri nahisi nilijidanganya kwa huyu Binti

theriogenology

JF-Expert Member
Oct 7, 2016
8,750
15,636
Wasalaam wana jf natumaini mko poa na weekend bila shaka imewaendea poa huko mlipo, nimekkuja mbele yenu naomba ushauri ambao utaweza kuniweka huru juu ya huyu mpenzi wangu tuliodumu takribani miaka 3 na miezi kadhaa….. binafsi mimi ni mwajiriwa (Dar es salaam) na mwenzangu bado ni mwanafunzi wa chuo (Mkoani) na Mungu akimjaalia mwaka huu pia atakuwa anahitimu masomo yake ya chuo…..

Kitu ambacho kimepelekea mimi kuja kuomba ushauri kwenu ni mwenendo wa tabia ya mwenzangu ya kupenda sana pesa na kuwa na matumizi mabaya ya fedha ingali yeye bado ni mwanafunzi kwa hesabu ya fasta fasta nishatumia zaidi ya takribani milioni saba na ushee kama si nane juu yake yeye because sometimes huwa namlipia ada na kumtumia pesa ya matumzi (Thou kwa hili la ada nishajua ya kuwa amekuwa akiniongopea kwa muda mrefu kuwa bodi ilimpa 20% lakni nimekuja gundua bodi inampa almost 60% baada ya kuanza kufanya uchunguzi wa chinichini mwaka huu)……..

Sasa ugomvi umeanza hivi kiukweli kuna pesa ambayo ninayo almost Tsh.15 million kwenye fixed akaunti, sasa huyu mpenzi wangu anapenda magari sana (Na huko chuo naskia anaendesha gari ya kifahari kwelikweli na sijui ni gari ya nani na pia naskia kapanga nje na wakati mimi aliniambia anakaa hostel inshort ni kuwa ana luxury life zuri tu chuo) kuna siku nilimtania nikamwambia nitanunua gari mwaka huu uwe unatumia so juzi nimekaa mahali Napata wine nikaona text yake iliyokuwa inasema “the year is approaching to an end “ Binafsi nikamjibu kuwa kwa sasa siwezi kununua gari labda mpaka mwakani na nikamwambia kwa sasa na save pesa kuna project moja nataka niianzishe na nikaongezea ya kwamba kama nikukusaidia nitakusaidia but si kama mwanzoni sasa hivi pesa imekuwa ngumu sana na ni vyema tuwe na matumizi mazuri ya pesa…..

Kumbe mwenzangu hakufurahishwa na lile jibu nililompa kaenda kuwaambia marafiki zake na akaongezea kuwa kwa sasa nimekuwa sitekelezi vitu ambavyo nimekuwa nikim promise, mfano juzi kati hapa kaniomba pesa nikamwambia sina na kumbuka mwanzoni mwa mwezi huu nilimtumia laki nne sasa nikawa najiuliza amezitumia vipi? Na wakati anakaa kwao?

Sasa hao marafiki zake baada ya kuomba ushauri kwao wakawa wamemwambia ya kuwa ni kawaida ya wanaume wa dar ndio tupo hivyo tunapenda kuchezea wasichana na kuwaachia “ Mpaka nakuja naandika uzi huu hapa JF tokea hiyo juzi mawasiliano yamepungua hapokei simu na leo nimejaribu kumpiga simu amepokea simu na bila salamu ameniambia anataka aniache nifanye mambo yangu ili niwe na amani maana kila analonishauri huwa sifanyi akakata simu…..

Na tukija katika suala zima la mapenzi amekuwa akinibania kula tunda na alinihakikishia kuwa yeye ni bikra na kweli nilihakikisha hilo kwasababu kila nilipokuwa kuwa najaribu kuitoa alikuwa akilalama kwa maumivu na hiyo ilipelekea mimi kumwacha kwa muda na nilivyohitaji tena kula tunda alikuwa ananizungusha sana na mwaka huu mwishoni aliniambia amebahatika kuitoa mwenyewe kwa kutumia sijui dildo alinitumia picha la hilo dude kwa kweli nilimlaumu sana why kafanya hivyo na nilivyomwambia anitumie picha zake nikakuta amebadilika kiumbo kifuani sikuona zile chuchu konzi zake bali maziwa yalikuwa yamekuwa makubwa sana na ameongezeka kimwili inshort amebadilika sana na amepoteza mvuto na hayuko kama alivyokuwa hapo awali…….

Mwisho ni kuwa Hilo gari hata kama ningelinunua alitaka yeye ndio akae nalo mpaka pale atakapo maliza chuo then ndio tuanze kulitumia wote?.... kuna mengi amenifanyia nimeshindwa andika kila kitu kwa hayo machache niliyoandika na imani wajuzi wa haya mambo watakuwa wamepata mwanga kidogo na najua fika humu ndani kuna watu wameona wengi katika mahusiano na imani kupitia wao watanipa ushauri ambao utaweza nisaidia kwa namna moja ama nyingine ili niweze kutatua hili tatizo linalonikabili kwa sasa….

Natanguliza shukrani zangu…..
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom