Naombeni ushauri mie, nimeaibika sijui nitauficha wapi uso wangu

Sijawahi kuona mpumbavu Kama wewe.
Simu ya mchepuko unaisave kwa jina la kike?
Huwezi kuishika kwa kichwa?
Halafu siku zote mchepuko anapewa pesa mkononi ku avoid records..
 
Mke wangu alichukua simu yangu na kufuta namba ya mpenzi wangu mwingine, namba ya Magreth na kuhifadhi namba yake ya kuwa anaitwa Magreth.
Sikujua kuwa kuna mtu alimwambia mke wangu kuhusu Magreth, kisha nikapokea SMS kutoka kwa Magreth akiomba pesa Sh.250,000.
Nilimkimbilia mke wangu kwa kuwa sikuwa na hiyo hela wakati huo na kumdanganya kuwa nahitaji Sh. 250,000 kwa dharura. Nilimwambia kuwa mdogo wangu Rutta anaumwa na anahitaji pesa haraka.
Mke wangu alinipa zile pesa na nikakimbilia kutuma kwenye akaunti namba iliyoandikwa kwenye ule ujumbe.

Nikiwa nimejipumzisha nyumbani baada ya kutoka kazini, niliendelea kuwaza iwapo Magreth alipokea pesa hizo.
Nilimtumia SMS ili kujua kama alikuwa amepokea pesa. Jibu lake lilikuwa, "Nipigie sasa."
Nilitoka nje nyuma ya nyumba kupiga simu.
Weeeeeeh!
Unaweza kufikiria uso wangu wa kutisha ulivyokuwa niliposikia sauti ya mke wangu badala ya Magreth!
Leo ni siku ya tatu bado nimesimama nje.
Sijui jinsi ya kurudi nyumbani kwangu !!!

Ushauri wowote tafadhali ...
Uongo njoo ukweli nenda. Mimi nikituma hela nina la ninayemtumia hutokea, inamaana jina la mkeo lilitokea! Haiwezekani hata ufanye nini, tungo za kitoto hizi.
 
Mkuu umeamua tu kutufurahisha wanabodi naona!

Dunia ya kijanja hii kuna mambo ya muhimu mbayo ni lazima mtumia simu uyafanye kwenye chombo chako kwanza kwa ajili ya usalama wa chombo hicho na wewe mwenyewe(password) kabla ya kuanza kukitumia.

Jambo jingine, dunia imejaa matapeli hii, wakati ukijiandaa, utatumaje pesa moja kwa moja kabla ya kuwasiliana naye kwanza kwa simu kujiridhisha?

Kama habari hii ni ya kweli basi matapeli wa kimtandao bado wana fursa kubwa sana ya kuendelea kuvuna bila jasho.

Rudi nyumbani kwa mkeo huku ukijichekeleza na ukamhonge zawadi atakuelewa na yataisha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijawahi kuona mpumbavu Kama wewe.
Simu ya mchepuko unaisave kwa jina la kike?
Huwezi kuishika kwa kichwa?
Halafu siku zote mchepuko anapewa pesa mkononi ku avoid records..
Acha uongo mkuu inamaana muda wote unakuwa na huo mchepuko? Ikitokea umesafiri na anahitaji hiduma yako utafanyaje?
 
Acha uongo mkuu inamaana muda wote unakuwa na huo mchepuko? Ikitokea umesafiri na anahitaji hiduma yako utafanyaje?
Itabidi tu anisubiri nirudi safari. Ukimtumia mchepuko pesa ukiwa safarini ndio anatumia hiyo pesa na ki benten kwa Uhuru zaidi. Tena anakupigia simu kabisa na kukudanganya Yuko kwa mama yake Mbagala. Kumbe anatumbuliwa buguruni
 
Hizi ndio zile script za Bongo movie.Jini anavuka barabara huku akiangalia magari kulia na kushoto.
Katika namba muhimu kuijua na kukariri ni namba ya wife.
Chai ikizidi utamu ongeza maji,sukari nyingi ni hatari kwa afya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom