Naombeni ushauri, mdogo wangu wa form four kapewa ujauzito

Bomandamo

JF-Expert Member
Aug 23, 2014
651
386
Habari zenu wanajukwaa, nina mdogo yupo form 4 katiwa mimba ndio amejifungua jana ila tokea mwezi wa tatu yupo nyumbani na hasomi

Atatakiwa kufanya mtihani kwa sababu alishajisajili kufanya ila mm naona atafeli tu, hapo sasa yupo hoi kwa sababu alijifungua kwa operation that means bado atakaa sana nyumbani

Nawaombeni wakuu mnijulishe kama kuna uwezekano wa kutengua huyo mtoto asifanye mtihani mwaka huu arudie tu form four mwakani na kama upo nifuate process gani ili niweze kufanikisha hili.

Mdogo wangu alikua wa kufaulu vizuri tu isingekua hili ila kwa sasa naona ataenda kufeli tu akirudi shule.

NB: Naamini hakuna asiye na mdogo wa kike hapa na wengine mna watoto kama mdogo wangu, hakuna aliyezaliwa mkamilifu, mtoto akishika mavi kwa mkono hatuukati huo mkono bali tunausafisha.. hii ni kwa baadhi wanaoongea kwa kashfa
 
Kwani aliyempa hiyo mimba amekataa kumuoa?, huyo mdogo wako ameisha onja mechi na amenogewa utapoteza hela yako tu
 
huyo mtoto amechagua lililojema kwake we msikilize sijui kama anashida na shule maana asingejiachia kiasi hicho

ule msemo wa WAKUBWA WANAFAIDI inabidi upigwe marufuku ikiwezekana wanyarwanda watumike
Usitake kumkatisha tamaa mleta mada. Alichagua lililo jema maana yake nini. Sasa labda mleta mada . Je binti alikuwa shule ya Serekali au ya binafsi kwani kama binafsi ni rahisi zaidi. Hongerah sana kwa kumtakia mdogo wako mema. Aidha mtafute huyo Fataki apate adhabu inayomstahili.
 
Habari zenu wanajukwaa, nina mdogo yupo form for katiwa mimba ndio amejifungua jana ila tokea mwezi wa tatu yupo nyumbani na hasomi

Atatakiwa kufanya mtihani kwa sababu alishajisajili kufanya ila mm naona atafeli tu, hapo sasa yupo hoi kwa sababu alijifungua kwa operation that means bado atakaa sana nyumbani

Nawaombeni wakuu mnijulishe kama kuna uwezekano wa kutengua huyo mtoto asifanye mtihani mwaka huu arudie tu form four mwakani na kama upo nifuate process gani ili niweze kufanikisha hili.

Mdogo wangu alikua wa kufaulu vizuri tu isingekua hili ila kwa sasa naona ataenda kufeli tu akirudi shule.
Kama yuko vizuri kichwani anaweza akajisomea nyumbani huku analea ili afanye mtihani.
 
Mabint wamekuwa vicheche wakipata mimba inaoneka ametiwa? Katiwaje? Imekuwa artificial insemination ya ng'ombe hiyo? Wasichana waache ucheche na ushamba vinginevyo ni lawama tu. Kila siku inahubiriwa kuhusu kinga lakini hawajali. Si bora kapata mimba kuliko HIV?
 
Dr Magufuli ana hiyo taarifaa? Aliyempiga mimba adakwe ndani ya 24hrs aswekwe ndani na alambe mvua ya miaka 30 jela baada kumaliza kifungo ahukumiwe kifungo cha maisha jela!! Huyo msichana zipo taratibu za kurudia class! Usipo pata ushauri hapa jaribu kuonana na mkuu wake wa shule atakupa utaratibu wa nn kifanyike
 
Usitake kumkatisha tamaa mleta mada. Alichagua lililo jema maana yake nini. Sasa labda mleta mada . Je binti alikuwa shule ya Serekali au ya binafsi kwani kama binafsi ni rahisi zaidi. Hongerah sana kwa kumtakia mdogo wako mema. Aidha mtafute huyo Fataki apate adhabu inayomstahili.

Alikua anasoma shule ya serikali
 
Je kama alibakwa? Tusimhukumu mtoto. Nenda shuleni, ongea na mwalimu mkuu wake atakushauri utafanya nini.
 
Dr Magufuli ana hiyo taarifaa? Aliyempiga mimba adakwe ndani ya 24hrs aswekwe ndani na alambe mvua ya miaka 30 jela baada kumaliza kifungo ahukumiwe kifungo cha maisha jela!! Huyo msichana zipo taratibu za kurudia class! Usipo pata ushauri hapa jaribu kuonana na mkuu wake wa shule atakupa utaratibu wa nn kifanyike

Asante sana mkuu maana unanitia moyo kidogo
 
....muache akae nyumbani km mwaka,baada ya hapo akipata nguvu unaweza mrudisha shule au akawa private candidate asome afanye mitihani.Ila ni vyema ukajua km kweli bado ana hamu ya kusoma,usije poteza pesa bure.

Pia unaweza kwenda shule yake aliyosoma,kupewa utaratibu mzima jinsi ya kufanya.
 
...too many kids inhere nowadays,better deal with them or leave them alone!
 
Dah! Inasikitisha sana mtoto unamgharamia Alf anaenda kufanya ujinga ujinga...... Hapo nenda Kwa mkuu wake wa shule atakupa maelezo vizuri... Baada ya hapo nenda hata kwenye ofisi za ustawi wa jamii, na badae police upate RB.... Tumtafute huyo fataki apigwe 30 kwanza sio vizuri kuwaharibia madogo mipango yao...
 
Anaomba ushauri, yalopita yashapita,mbona mwamshambulia mtoa mada? Kamwone mwl mkuu atakupa utaratibu wote wa kuahirisha masomo,akarudishwa form three next year akaanza form four, utakua amejielewa na huyo atafika mpaka university, mpeni moyo
 
Yafaa mwaka huu apumzike mwakani arudie form three hili aweze jiandaa vizuri na mtiani.Nyie mlivyo ona amebadilika kwanini amkumuliza hili ahairishe kufanya mtiani asiyoe ada ya mtiani au mlijua amenenepa mpaka alipojifungua ndio mnashtuka
 
Kiongozi, kama ni shule ya serikali na wanataarifa za ujauzito huo, mkuu wa shule hana msaada wowote. Jaribu kumwomba amruhusu huyo binti afanye mtihani ili aende sawa na matokeo yake ya form 2. Halafu atukwa na uwezo wa kufanya kama private candidate kwa kutumia hiyo index namba!!
 
Kwa uzoefu wangu mara nyingi watoto wanaopata mimba wanafanya vibaya wakienda kufanya Mithani, lakini pia kuna process za kufanya iwapo mtoto atahairisha kufanya mtihani hasa yule aliyesajiliwa ambayo inahusisha shule,afisa elimu wilaya na mkoa kwa hiyo kama una mpango wa kuhairisha mtihani anza kufanya mapema kabla mambo hayajaharibika. Hofu yangu ni hili suala la ujauzito na ule waraka wa kufukuza shule wanafunzi wanaojishusha na ngono/mapenzi shuleni na kupata mimba shuleni.Ingawa kuna harakati za wanaharakati kupigania wanopata mimba kuendelea na shule lakini bado tu kuna matamko ya kisiasa ya kutaka kuendelea na shule. Pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom