Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Mmeamkaje wakuu?

Wakuu kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimebahatika kupata kamtaji kidogo Milioni 10. Naombeni mawazo yenu nifanye biashara gani ambayo inaweza kukuza mtaji wangu, umri wangu miaka 26 sina mke, karibu wakuu kwani ushauri wenu ndio mafanikio yangu.

Asante.
Ushauri utategemeana na namna ulivyoipata hiyo million kumi, Kama umeipata kwa mkupuo baada ya kuuza au zali, unastahili kuendeleza maada, Kama hiyo million kumi ni imeanza 01-10 wewe Leta mawazo ya biashara hapa upo vizuri
 
Wazo lilifaa mwaka 2005
Mimi ni muumini wa uwekezaji wa muda mrefu, kwa mfano ungeenda iringa njombe ukanunua shamba la miti ukapanda kisha ukafanya mambo mengine. Kwa miaka 15 ijayo naamini utakua unazungumza lugha nyingine.

Au biashara ya mbao haswa mbao ngumu. Huwa hazishuki thamani kamwe, ila utafiti juu ya biashara hii ni muhimu na taratibu zote vibali nk.

Hardware nayo inalipa sana nayo pia inahitaji utafiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fungua duka la reja reja
Fungua mgahawa wa chakula
Fungua stationery
Fungua duka la dawa
Fungua duka la spea za pikipiki
Fungua duka la nafaka.
 
Napenda kuokoa pesa (saving money) nimeweza kufikisha kiasi cha shiling milion 8. Sasa napata wakati mgumu ni biashara gani naweza kuifanya kwa mtaji huu wa pesa.

Nahitaji kuwekeza huko kwenye biashara . Naombeni msaada wenu tusaidieni wengine.

Ahsanteni

======
Michango ya wadau

Ukiwa huna pesa unajikuta una vitu vingi sana vya maana vinakuja kichwani right!? Ila ukishaipata sijui vinaendaga wap! Just kidding

Developing countries kwa maana nyiingine zinaitwa land of opportunity! Kuna opportunities kwenye kila sectar inayojaribu kuigusa! Shida kubwa ni ukosefu wa mtaji ila kwa ww sio changamoto tena yaan mtaji sio swala kwako!

8M ni pesa nyingi sana labda kwa harakaharaka nikuchambulie baadhi ya biashara unaweza kuzifanya kwa mtaji huo

1: biashara ya miti au mbao
Hii inaweza ukawa kmchuuzi ila inahitaji uwe na uhakika wa masoko au mlimaaji kabisa sema hii inahitaj uvumilivu kdg kwa watu wa maeneo ya iringa wanaweza kutoa ufafanuz kdg kwenye hilo l. Gharama ya ukuzaji wa hekari moja ya miti mkoani iringa mpk kufikia mavuno haizid 1M na ukivuna na kuuza miti kwa mti ni hadi @30000-@60000 inategemea na ukubwa na mda wa mti hekari moja inauwezo kuchukua miti mpk 600 so kwa hesabu ya harakaharaka apo minimum kwa hekar moja unaweza pata mpk sh 18M baada ya miaka sita mpk 10 na kwa uusaji wa mbao km unachanja mwenyewe inafika mpk mara mbili ya hiyo!

2: uuzaji wa nafaka na matunda!
Swala lililo wazi ni kwamba hamna siku ambayo tutaacha kula kwamba tumeshiba kwa maana nyingne hii ni fursa kubwa sana mikononi mwetu! Biashara hii ni ya msimu na mahitaji uzur ni kwamba karibia kila kipindi kina msimu wa tunda au nafaka husika. Apa inabidi ucheze na masoko usiwe bendera fata upepo kwa mfano msimu wa nanasi! ukinunua nanasi moja shamban ni 300-@500 ukipelekea dar ni 800-1000 sawa utapata faida ila ukijulisha na gharama za usafilishaji kwang haijkaa sawa vile ila ukipereka maeneo km tarime automatically bei inapanda mpk 1500-2000 kwa nanasi plus na gharama za kusafirishia kwa centa moja hazizid 1M nakuhakikishia unaweza tumia km 5M ukapata faida mpk 15M per one trip! Ukiachana na mananasi nikupe mfano mwingne wa mpunga wakat wa mavuno gunia moja la mpunga linakua 35K-45k inadepend na eneo iyo ni kwa bei ya morogoro then ukitafuta godown lako au lakukorisha ukautunza baada ya miez sita after mavuno automatically huwa unapanda kwa 85k mpk 90k unaweza pata faida mpk mara mbili

3:kilimo biashara cha matunda, mbogamboga na ufugaji wa kuku
Itaendelea .......!

NB: NILIVOTAJA HAPO HASA THOSE NUMBERS SIO COSTANT ZINABADILIKA MWAKA HADI MWAKA, MSIMU HADI MSIMU, ENEO NA ENEO AU SUPPLY AND DEMAND PIA.
Hapa ndio huwa changamoto mwenye pesa hajui biashara gani ya kufanya mwenye wazo la biashara hana mtaji wa kuanzia anyway! angalia ni kitu gani unachofikira kwa haraka na ukipendacho kufanya, biashara ziko nyingi depends na ww umefocus nini zaidi.Milion 8 ni nyingi kwenye biashara za kati lakini inaweza potea pia usipokuwa na malengo bora

IDEAS
1.Duka la nguo au vyombo
2.Kuuza matofali, kokoto na mchanga
3.Pub
4. Ufundi wa kushona nguo za kike na suti za kiume unanunua machine unaajiri mafundi wazuri.
5.Saloon ya kike au kiume standard kali tu
6.Car wash
1. Fresh Foods and Drinks (Branded)

- Hapa utaanzisha restaurant itayohusika na usindikaji wa vinywaji visivyokuwa na kemikali na chakula fresh (Ready to Serve). Ukiangazia sehemu za Drive - In au kufanya delivery within 20 KM. Let's say! John Bambo Sepia (Hii ni juice yenye mchanganyo wa Chenza, Banana, Zabibu na Tangawizi), John Bambo Fellah (Huu ni mchanganyo wa roasted Chicken, Tortillas na Vrille.

2. Clothingline (Branded)

- Utaanzisha mavazi vyema kutafuta wabunifu hata wawili base zaidi katika mavazi ya casual, commercial na business. Tengeneza partnership na watu wenye titles lakini hawana brand. Let's say! John Bambo x Marioo (Hizi ni tisheti, fulana, kofia na sports kits zinazoweza kuvaliwa sehemu yoyote), Hakikisha unalenga soko la kati na chini.

3. Digital Auth / SMM Agency / Multimedia Company (Branded)

- Hapa fungua agency itayohusika na masuala ya kidigitali, uchapaji na uendeshaji masuala kidigitali. Kupitia John Bambo Digital Agency utaweza kulipia packages tofauti kama taasisi, kampuni au mtu binafsi kuendeshwa kwa masuala yako kidigitali, matengenezo ya Billboards, Syncing Boards, Fleets and Co. Uchukuaji picha, video kutengeneza commercial ads and co. Unavyozidi kukua tanua wigo anza Production issues hadi Audiovisuals Company.
 
Napenda kuokoa pesa (saving money) nimeweza kufikisha kiasi cha shiling milion 8. Sasa napata wakati mgumu ni biashara gani naweza kuifanya kwa mtaji huu wa pesa.

Nahitaji kuwekeza huko kwenye biashara . Naomben msaada wenu tusaidien wengine.
Ahsanten

Ungeangalia kwanza unapenda nini kufanya biashara gani ukifanya utaifanya kwa moyo
 
Ungeangalia kwanza unapend nini kufanya biashara gani ukifanya utaifanya kwa moyo
Sawa ndugu nimekupata. Ila ninaamini kuna biashara ambayo naweza kunufaika nayo japo kwa mtaji kama wangu, nikiifanyia research na kuona inalipa nais ntaweza kubadilisha maisha kwa namna moja ama nyingine
 
Hapa ndio huwa changamoto mwenye pesa hajui biashara gani ya kufanya mwenye wazo la biashara hana mtaji wa kuanzia anyway! angalia ni kitu gani unachofikira kwa haraka na ukipendacho kufanya, biashara ziko nyingi depends na ww umefocus nini zaidi.Milion 8 ni nyingi kwenye biashara za kati lakini inaweza potea pia usipokuwa na malengo bora

IDEAS
1.Duka la nguo au vyombo
2.Kuuza matofali, kokoto na mchanga
3.Pub
4. Ufundi wa kushona nguo za kike na suti za kiume unanunua machine unaajiri mafundi wazuri.
5.Saloon ya kike au kiume standard kali tu
6.Car wash
 
Back
Top Bottom