ntabudjo
Member
- Jun 1, 2016
- 70
- 64
Habarini za mwanzo wa wiki wana jamvi,
Kuna mwanamke nimekuwa nae kwenye mahusiano ya kimapenzi zaidi ya mwaka mmoja sasa ila ilipofikia mwezi wa pili mwaka huu siku ya valentine day alipigia simu asubuhi na kunihoji nitamuoa lini nikamwambia asuburi kama baada ya miaka mitatu kwa sababu bado sijajipanga vizuri kiuchumi.
Baada ya hapo akaniandikia sms ndefu ya ya kunisihi tuachana kwa sababu anaona nimeshindwa kumuoa nilikubali kwa sababu mara nyingi alikuwa akinisihi tuachane ninakataa ila niliumia sana baada ya hapo tulikaa kimya kifupi, sasa kuanzia wiki iliyopita ananipigia simu na kunitumia sms akinambia ananimiss sana na anajuta kuniacha kisha kuniambia turudiane na yuko tayari kunivumilia.
Sasa ndugu zangu niko kwenye dailema nashindwa kujua anataka nini na lengo lake kwangu ni lipi, nipeni ushauri.