Naombeni ushauri kwa huyu mdogo wangu wa kike mwenye matokeo haya kidato cha sita mwaka huu

Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au
namshaur aombe SUA kuna course nzuri tu atapata, lkn kwa course za afya ni ngumu kwa kulingana na guidebook ya TCU wanataka atleast C in chemistry
 
Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au
Kama uwezo upo awasiliane na Global Education Link wamtafutie chuo cha nje kama India hivi au China-inawezekana akapata afya. Anaweza pia akapata BSc (BLS)-Biotechnology and Laboratory Science . Kuna option ya afya ndani yake .
 
iyo BLS kwa hapa kwetu ipo
 
Kama uwezo upo awasiliane na Global Education Link wamtafutie chuo cha nje kama India hivi au China-inawezekana akapata afya. Anaweza pia akapata BSc (BLS)-Biotechnology and Laboratory Science . Kuna option ya afya ndani yake .

Ila tatizo ni kwamba hao watu wa BLS hawatakiwi kufanya kazi mahospitalini. Watu wa wizara ya afya wako strict sana hapo, wanawahitaji watu wa medical lab tu. Swali ni je huyo mwanafunzi atakua tayari kupambania nafasi chache TVLA, livestock research institutions, TFDA na viwandani ?
 
Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au
Kaka ata Mimi nmepata hivi napenda kusoma medical laboratory ila naomba TCU wameandika uwe na C ya chemia bios D na E ya physics daah nawaza kwel
Me pia nmepata hivyo naweza pata medical laboratory Bugando?

hongereni kwa kufaulu ila ni vyema mnavyo omba ushauri humu iko hivi kama huna C ya chemistry ila labda unayo ya BIOS unaweza ukapewa degree ila sio na huwezi kabisa kupata MEDICINE,PHARMACY,DDS (dental surgery) na program yoyote yenye point nane (8) utaweza pata nursing na sii kwa vyuo vya serikali labda kusiwe na competition na pia BMLS huwa ina competition sanaa kutokana na mawazo ya kila mwanafunzi anaemaliza PCB (ILA NAONA NURSING NI NZURI KIMASLAHI NA KUPATA KAZI) jaribuni nursing degree ST john huko dodoma au Bugando huko mwanza na kairuki huko dar es salaam kwa nursing usitake kupoteza muda wadongo zangu kwa kuweka medicine au pharmacy na usi apply kwa kufuata mkumbo angalia uhalisia ndio uapply na maanisha marks zako na kitu unachokitaka na namba iliyotolewa chuoni wanahitaji watu wangapi kuna vitu vingine pia njee ya afya jaribuni kuangalia SUA,UDOM,MZUMBE,ARDHI,ST JOSEPH,ST AGAUSTINE n.k.. mwaka jana wengi walikosa vyuo kisa kung'ang'ania jambo moja hasa PCB takers kwahiyo kuweni makini na kama umefaulu vizuri jaribuni pia vyuo vizuri ila kama huna uhkika na haujaperfome kwenye kile kiwango kinachohitajika usiapply chuo chenye competition jaribuni na vya private hasa kwa wanaotaka afya.
 
Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au

Mbali na kozi za afya ambazo "PCB wote Tanzania" ndio huwa wanazitaka at first place, kuna kozi nzuri sana za "natural sciences" ambazo huyo ndugu yetu anaweza akasoma na zikamsaidia huko mbeleni. Nimeambatanisha "UDSM undergraduate programs synopsis" ikiwa ni nyaraka yenye maelezo ya jina la kila kozi (degree), maelezo yake, malengo na mawanda ya ajira na kujiajiri baada ya kumaliza kozi husika. Naamini itasaidia kwa kiwango fulani kukupa japo ka mwanga. Kila la heri.
 
Attachments

  • UDSM UG Programmes Synopsis New Version 1.pdf
    1.2 MB · Views: 48
Msaada ndugu zangu kuna dogo wangu ana matokeo haya Phy-E Chem-D Bio-D anaweza kupata chuo kijana kama huyu?

Halafu programme gani za degree anaweza kupata kirahisi.
Naomba majibu wadau.
 
Msaada ndugu zangu kuna dogo wangu ana matokeo haya Phy-E Chem-D Bio-D anaweza kupata chuo kijana kama huyu?

Halafu programme gani za degree anaweza kupata kirahisi.
Naomba majibu wadau.

Rejea post number 32, lakini pia anaweza kupata kozi nzuri tu pale SUA, UDOM na kwingineko katika fani mbalimbali kama vile za kilimo, mifugo, chakula, misitu na nyuki, wanyamapori na uhifadhi, ualimu, teknolojia za maabara, uvuvi na viumbe maji, n.k
 
Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au

Dah kapata kama mm mwaka jana.. ila nkaangukia Urban and Regional Planning (Bsc.URP) Ardhi university..
 
Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au
Kama ni mzuri wa sura na umbile, mpeleke akasomee diploma ya katibu muhutasi... Huko ataenda ku husstle wakati ajira zenyewe mishahara mbuzi. Bora asome vitu rahisi aje apate mshahara huo huo, I tell you.
Kwenye afya kusoma ni hustle na mazingira ya kufanya kazi sio rafiki kabisa. Wakati akipata kazi ya ureceptionist anapigwa kiyoyozi, na kubofya bofya computer, mda wa kazi ukiisha huyoo anapanda kivitz chake kurudi nyumbani!
 
Amepata division two ya 11 ya PCB. phyc D, Chemistry D, Biology C. anapenda kusoma kozi ya afya. naombeni ushauri kama atapata au
ushauri wa humu wakati mwingine si sahihi maana wengine hawajasoma na waliosoma wanaweza kuwakatisha tamaa wenzao, Ni vyema upate copy ya kitambu ya TCU omba hata softcopy japo unaweza kukidownload pia, angalia humo kozi anazotaka na cutting points zake kama zinajitosheleza kusoma hizo kozi/ faculty, kama hujawahi kabisa kufabya applications basi uliza kwa mtu ikiwa na kitabu kabisa, kwa mtoto wa kike hizo marks bado ni nzuri tu changamoto ni competition maana wengi wamefaulu kama yeye au zaidi yake, hivyo asisahau pia kufanya application za diploma kwa hizo kozi za afya anazotaka
 
Kama ni mzuri wa sura na umbile, mpeleke akasomee diploma ya katibu muhutasi... Huko ataenda ku husstle wakati ajira zenyewe mishahara mbuzi. Bora asome vitu rahisi aje apate mshahara huo huo, I tell you.
Kwenye afya kusoma ni hustle na mazingira ya kufanya kazi sio rafiki kabisa. Wakati akipata kazi ya ureceptionist anapigwa kiyoyozi, na kubofya bofya computer, mda wa kazi ukiisha huyoo anapanda kivitz chake kurudi nyumbani!

Kwa mfano huyo binti angekua ni mwanao, ushauri huu ungekuwa applicable ? au ushauri wako ni "tailor made" kwa watoto wa wenzako tu pekee ?

Just a question
 
Kwa mfano huyo binti angekua ni mwanao, ushauri huu ungekuwa applicable ? au ushauri wako ni "tailor made" kwa watoto wa wenzako tu pekee ?

Just a question
Yep! Angekuwa mtoto wangu au hata mimi mwenyewe ningefanya hivi hivi. Kwani wewe unapenda mtoto wako afanye kazi ngumu kwa malipo kidogo?
Unajua kazi za wodini zilivyo? Wagonjwa wanatapika, wanaharisha, wananuka jasho hawajaoga, nk. Then unatakiwa kukesha wodini usiku kucha unawahudumia wakati kuna kazi rahisi mtoto wako anaweza kufanya kama kufanya kazi za ofisini za kuhifadhi nyaraka, kupokea simu na kuhudumia wageni wa ofisi? Kipi bora?
 
Back
Top Bottom