Duniahadaa
JF-Expert Member
- Oct 16, 2017
- 336
- 677
Mimi ni Muuguzi Mkunga katika hospitali moja ya wilaya katika Mkoa wa Dodoma. Ni mwanachama wa chama dume, chama pendwa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Ninatarajia kustafu kazi mwaka 2022 July 10 baada ya utumishi uliotukuka wa miaka 31.
Natarajia kupata mafao yangu ya Sh. milioni 100. Baada ya kupata mafao yangu, nilipangilia kwanza kujenga nyumba yangu ya kuishi kwa sh. 30 million, kulipia ada ya chuo kikuu wanangu wawili na zingine nijenge nyumba za kupanga ili zinisaidie kusukuma maisha. Pia nilitamani wazee wangu niwajenge pia kibanda kule kijijini. Sasa naambiwa kuna kikokotoo kinakahofanya nilipwe milioni 25 na zingine milioni 75 nitakuwa nalipwa kidogo kidogo kila mwezi hadi nife. Hii maana yake hata ile nyumba niliyopanga kuijenga ili inisitiri sitaweza achilia mbali uwekezaji niliopanga kuufanya.
Sasa nimesikia Chadema na Tundu Lissu wamekuja na sera inayokataa kikokotoo hiki. Je, nifanyaje mimi maana nimechanganyikiwa. Nimpigie Magu ile kwangu, kwa wanangu na kwa familia ya wazee wangu au NIASI CHAMA nimpe Kura Tundu Lissu ili mipango yangu itimie? Naombeni ushauri jamani.