Naombeni ushauri kuhusu mahusiano haya ya mama yangu na huyu mwanaume

Russia_Norway

New Member
May 9, 2020
3
15
Habari zenu,

Nimekuja na ID mpya ili kuficha utambulisho wangu wa awali ni kuomba msaada wa ushauri.

Naombeni ushauri na njia za kutatua tatizo hili.Ipo hivi kwenye tumbo la Mama yetu tulikuwa watoto 7 hadi Leo hii tupo 4. Katika watoto 7 tumezaliwa na Baba tofautitofauti 4. Katika hao baba zetu kuna moja wao ndio tumekuliwa kwake toka tukiwa wadogo badaye miaka 6 iliyopita Mama alitengana Nate.

Mama ni mtumishi wa umma, hivyo alinunua kiwanja na kujenga nyumba ambapo watoto wote 4 tuliongozana nae na kwenda kuishi nae, maana haikuwezekana kukaa tena kwa huyo baba mlezi sababu katika wathili.4 tuliobaki kati yetu 1 tu ndio mwanae kwahiyo ikabidi wote sisi sote tuongozane na mama. Ikumbuke kuwa katika sisi watoto 4, mtoto 1 hamjui baba yake wengine 2 Baba yao alifariki na mtoto 1 baba take ndio huyo aliyetulea.

Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52, jambo linalotusumbua ni kuwa Mama yetu ana mwanaume mwingine ambaye ni mume wa mtu. Jamaa huyu huwa anakuja na kulala hapa nyumbani karibu kila siku; huwa anasitisha kuja pale ambapo kaka yetu mkubwa akija nyumbani.

Ndugu na marafiki wamejaribu kumshauri mama kuwa tayari umri umekwenda na ana vijana wakubwa anatakiwa kuacha mambo hayo pasipo mafanikio, haelezeki wala haambiwi chochote. Kwa sasa tumefunga chuo sababu ya hii CORONA nipo hapa home naona aibu kijiji kizima kinatuzungumza.

Kaka yangu mkubwa alijaribu kuongea na huyo bwana mwaka jana; kwa kweli jamaa alisitisha kama miezi 2 hivi pasipo kuonekana, badaye ratiba ikaanza kama kawaida nimemjulisha kaka atafute siku 3 nyumbani tusaidiane kutatua tatizo hili. Pia, kila tukimsuhi Mama kuacha hiyo tabia majibu anayotupa ni kuwa huu mji ni wake na hamna aliyemsaidia kujenga hivyo anafanya chochote atakacho.

Ndugu zangu wana JF, naombeni msaada wa mawazo namna ya kutatua tatizo hili.
 
Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52 ,Jambo linalotusumbua ni kuwa" Mama

Nyie watu wazima what are you doing at your mum's home she has her own life leave her alone she sacrificed for you and educated you that's enough go away at 52 she still needs a man to entertain her.......nyie siwelewi kabisa wengine tumeanza maisha at 18 na timefanikiwa mkbali tu, hayo ya mama wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hayo ni maisha yake binafsi japo ni kawaida kwa watoto kuumia kwa sababu huhisi nafasi ya baba yao inapokwa na mtu baki. Kujaribu kumshauri ni kama kuchochea tatizo la chuki baina yake na ninyi.
Ushauri wangu, tafuteni namna ya kujitegemea na yeye aendelee na maisha yake.
 
Nimewazaaaa nikashindwa cha kuwashauri. Sababu huwezi sema mtumie ndugu as kila mtu ana mjomba wake, shangazi yake, baba mkubwa&mdogo wake, babu yake, yaani vululu vululu.

Cha msingi hapo kaeni mbali na matendo ya mama yenu msije mkaingia kwenye laana zisizo za lazima. Kwa kuwa mmeshamshauri na hashauriki kaeni kimya. Kuweni busy na mambo yenu wala msiwaze hayo matendo ya mama yenu kwani mtajipa stress za buree.
Unforgetable
 
"Sisi sote miaka yetu ni 24+ na Mama yetu ni 52,Jambo linalotusumbua ni kuwa" Mama

Nyie watu wazima what are you doing at your mum's home......she has her own life leave her alone she sacrificed for you and educated you that's enough go away at 52 she still needs a man to entertain her.......nyie siwelewi kabisa wengine tumeanza maisha at 18 na timefanikiwa mkbali tu, hayo ya mama wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
Madogo bado wanasoma, kama umemsoma amesema yuko chuo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mama yenu hawezi kuishi bila mwanaume...
24+ muhame mkaishi kwenu, yupo hivyo miaka yote inaonekana tokea avunje sinia....mumuache mama afurahie mgegedo, vipi nyie??

Mnataka kugombea URITHI, baba wanne tofauti ni ishara mjitegemee...mtafute vyenu...hapo hamna chenu!

Everyday is Saturday.......................... :cool:
 
Ofcourse naungana na mama yenu...she is right .mie nasemaga haya mambo usijudge..mama inaonekana hawezi ishi alone...anahitaji faraja..sema anakosea kuleta hapo mwanaume wake bora muwaambie wajomba..ila sio nyie alafu malizeni kusoma muondoke hapo mmpe mama wa watu uhuru..life is too short to complain!..msihukumu msije mkahukumiwa!
 
Mama yenu hawezi kuishi bila mwanaume...
24+ muhame mkaishi kwenu, yupo hivyo miaka yote inaonekana tokea avunje sinia....mumuache mama afurahie mgegedo, vipi nyie??

Mnataka kugombea URITHI, baba wanne tofauti ni ishara mjitegemee...mtafute vyenu...hapo hamna chenu!

Everyday is Saturday.......................... :cool:


Case closed! Hawana hata haya!..nini 52!
 
Back
Top Bottom