Naombeni Ushauri kuhusu M-Pesa..Hela imetumwa kikakosa na imeshatolewa...

tete'a'tete

JF-Expert Member
Feb 10, 2010
472
62
Wakuu,

Hope muu wazima!

Nisaidieni jana kuna ndugu yangu alikuwa anatuma hela through M-pesa kutumia simu yake sasa akakosea namba ya mwisho bila kujua ikaenda kwa mtu mwingine na hiyo aliigundua ilipomrudishia message kwa sababu hakuweza kujua ni namba ipi aliikosea kwa hiyo hakuweza kutress ile namba wakati huo kumwomba aliyemtumia amrudishie hiyo hela, akawa anawatafuta Voda nao wakawa busy kama tujuavyo system yao ilivyoelemewa baada kama ya dakika kumi na mbili hivi akawapata kuwaelezea watatress wakakuta yule mtu ameshadraw zile pesa, basi voda msaada waliompa huyu ndugu yangu ni kumpa namba ya aliyedraw zile hela ili ampigie na asimwongeleshe kwa hasira maana anaweza akadestroy hiyo namba na mazungumzo yakawa hivi:

Ndugu yangu -- akapiga simu ikapokelewa akamwomba nimetuma hela kwako kimakosa samahani naomba unisaidie unirudishie nina shida kweli nilikuwa namtumia ndugu yangu yupo Kcmc mama yetu amelazwa anafanyia operation kesho.

Aliyedraw hela akamjibu... hizo hela kweli ziliingia na kwa sababu nilikuwa nategemea kutumiwa kiasi hichohicho tsh 150,000 za ada za mtoto wa shule kwa hiyo imebidi haraka nikazidraw na nimeshazitumia kumbuka hapo ni saa kumi na moja na nusu hivi na kosa lilitokea saa kumi na moja kamili hela alidrwa kumi na mona na dakika tisa. akamwambia sasa sina hela itabidi mpaka nitafute nikipata nitakutumia..

Ndugu akanielezea nikamwambia hebu nipe namba ya huyo mtu akanipa jibu likawa lilelile...

Sasa wakuu nataka kujua hii M-pesa inawalinda vipi wateja wao wakikosea kutuma hela kimakosa, na hao customer care kweli walishindwa kuwasiliana na huyu mtu arudishe hela ya mtu, eti wanamwambia asimtukane wala kumsemea vibaya..mpaka sasa ndugu yangu huyo hajarudishiwa cha hela wala nini je nimshauri vipi?? hayo ndio masahibu ya M-pesa yaliyotokea jana...
 
pole kwa yaliyompata ndugu yako,hapo usiwalaumu voda kwanza customer care yao wapo makini ingekuwa mtandao mwingne asingewapata kabisa,upande wa pili lawana kwa nduguyo vodacom uduma zao uwa zinakuwa na pini ya uthibitisho aipo kama ya tigo ambayo aina pin ya kukubali.swali huyo ndugu yako kwanini akuandika namba ya anaemtumia pembeni ili awe na uakika wakati wa kuinakili.pole sana ajifunze kufanya mambo kwa umakini asipend mazoea ndiyo yamepelekea watu kusaini mikataba mibovu katika nchi yetu
 
Pole sana ndugu! Mimi niliwahi kupata kadhia kama hiyo mwezi uliopita. Nilikosea namba na fedha zikaenda kwa mtu mwingine. Niseme mimi nilikuwa na bahati kwasababu baada ya kuhangaika sana kuwapata jamaa wa costumer service, niliunganishwa mara moja na wahusika wa mpesa na baada ya maswali machache waliniambia fedha zangu zitarudishwa muda mfupi. Hii nasema ni bahati tu. Kama zingekuwa zimechukuliwa nahisi tatizo lingekuwa kama hilo!
Mitandao itafute njia mbadala ya kufidia wateja wao kama vile kutoza kiasi fulani cha Bima kwa fedha zinazotumwa au kuwekwa kwenye akaunti zetu za mpesa/tigo/airtel etc.
 
Pole kwa tatizo..lakini sidhani km voda wana utaratibu huo..
 
In 9 minutes jamaa akawa kasha withdraw na kwenda kulipa ada.....jioni...shule zilikuwa wazi au bank? labda kama wanalipia kwa mpesa...ada....kwa headmaster ni karibu hapo hapo...but kuna utata mkubwa...na kama jamaa alikuwa anategemea kutumiwa ada muda ule lazima palikuwa na dead line mean lada kesho yake?

So ikawa ni fasta yeye akalipe...sasa yule aliye kuwa anamtegemea kumtumia mean hajatuma..mpaka sasa...mwisho naweza sema jamaa si mtu mzuri...yule aliye tumiwa kimakosa.
 
M-Pesa ni kama western union ukimtumia mtu akishazitoa ndo basi tena.
Unachoweza kufanya ni kumshitaki aliyepokea hiyo pesa kwa sababu Voda wana taarifa kamili kuhusu huyo mtu (Namba zote zipo registered) ila hawawezi kuzitoa bila maamuzi ya mahakama, ila gharama ya kesi inaweza ikazidi hiyo hela.
 
Kampuni zetu zingekuwa makini kungekuwa na namna wanavyoweza kuwafungulia mashitaka watu wa aina hiyo! Maana wao inawezekana kumnasa mtu huyo, kwa sababu mtandao wao lazima uoneshe huyo jamaa yuko wapi na amechukulia kwa agent gani!
 
Pole sana ndugu kwa yaliyowakuta.Nikweli kuwa ndugu yako alikosea namba ya mwisho kwa kutokuwa makini ama kwa kutingwa, siwezi kumlaumu kwa hilo ila lawama zangu ziko kwa wahudumu kwa wateja. Jibu walilo mpa nduguyo halikuwa sahihi asilani kwani kumtafuta mteja aliyepokea fedha kimakosa ni la kwao na si mteja aliyetuma fedha hizo as long as nimewajulisha juu ya tatizo hilo. Mteaja kuharibu namba si kikwazo kwani wao wanataarifa juu ya wateja wao na ndugu zao wa karibu. Mbona watu wengine wanapotumiwa fedha kimakosa wao kama kampuni huwatafuata wateja hao na kuwaambia kuwa wafike katika ofisi zao zilizoko karibu na eneo mteja huyo aliko? Yametukuta na walitusaidia kwa mtindo huo.
Ninawasiwasi na ujuzi wa baadhi ya wahudumu hao huenda wengine ni wageni na hawazijui baadhi ya taratibu.
 
Nenda kwenye ofisi za M-PESA tafuta mmojawao, mtangazie dau uone wanavyochangamka-heri nusu shari kuliko shari kamili!!!
 
Back
Top Bottom