Naombeni ushauri kuhusu kusoma Masters

Mwalimu unasoma Master degree ili iweje wakati hakuna muundo huo kwenye kazi yako hio ya vilaza.

Pambana kivingine hata usome Master degree bado wewe unabaki kuwa kilaza uliekosa fani nono na kukimbilia kwenye mteremko.
Acha dharau na kashfa boss... heshimu taaluma za wengine, hata wewe ulipita kwa mwalimu.
 
Sawa.. ila natamani sana kusoma master ili niwe kilaza mwenye uhafadhali.. pia vipi nikifanikiwa kupata hyo master hv siwezi hamia wizara kiongozi..? Nipe ushauri chief.
Masters ni ubobevu katika eneo husika,tunategemea muhusika ujue unataka kubobea kwenye nini!!!
 
Kwema wakuu..

Naombeni ushauri. Mimi ni mwalimu nilisoma BACHELOR OF EDUCATION (BED. Geography) natamani kusoma masters sasa sijui nisomee masters ya kitu gani naombeni ushauri.
Fanya Masters ya Education ukispecialize kwenye moja ya hizi areas
Education Research and Evaluation,
Curriculum Development,
Administration, Planning and Policy Studies
Quality Assurance
Cheki na prospectus za UDSM, OUT wanaprogramme nzuri za masters
 
Mwalimu unasoma Master degree ili iweje wakati hakuna muundo huo kwenye kazi yako hio ya vilaza.

Pambana kivingine hata usome Master degree bado wewe unabaki kuwa kilaza uliekosa fani nono na kukimbilia kwenye mteremko.
We ulifundishwa na vilaza mkuu?
 
Ulishakosea kusoma education undergraduate. Hapo masters haitakusaidia labda upate kazi kwa kutumia degree yako kwenye corporate then upate uzoefu wa hiyo kazi miaka kazaaa ndio then usome masters yake.

Hiyo Ada ya masters uliyonayo sasa hivi nenda nje ya nchi kasome short course yenye fani adimu.

Mfano unahodha wa meli.
Duh kakosea kusoma ualimu...?
 
Kwema wakuu..

Naombeni ushauri. Mimi ni mwalimu nilisoma BACHELOR OF EDUCATION (BED. Geography) natamani kusoma masters sasa sijui nisomee masters ya kitu gani naombeni ushauri.
Mkuu haya ni maamuzi mazuri soma tu elimu haimtupi mtu.

Mimi nna bachelor of arts with education niliongeza nikasoma masters of public administration nikaachana na kufundisha nikaingia kwenye NGOs kama program specialist.

Kama umeamua kusoma wewe kapige shule wewe una degree ya education (elimu) ni pana sana wewe haukusomea teaching.

Ukifika UN, USAID, UK Aid, World Bank, UNICEF, TCU, TIE, ubalozini na taasisi nyingine kibao utakuta walimu wapo uko wanafanya maisha.

Piga shule mkuu, ikiwezekana usome masters ya monitoring and evaluation inatolewa Open University.
 
Back
Top Bottom