Naombeni ushauri kuhusu baba yangu ambaye ana tabia inayotupa mzigo watoto

kwisha

JF-Expert Member
Sep 9, 2021
1,666
4,365
Nina baba yangu ambaye kwasasa ana umri wa miaka 48, baba yangu huyu tunashindwa kumuelewa kama amerogwa au amejichanganya mwenyewe.

Mwaka 2009 alitupiwa pepo akaanza kutembea uchi mchana kweupe, lifanikiwa kupona akawa sawa na toka siku hiyo amekuwa muongo sana. Anaweza kudanganya watu kuwa anapesa akakopa pesa za watu huko mzigo wote anatupia kwetu sisi watoto wake.

Anaweza kwenda kuoa huko mwanamke mwingine akadanganya watu kuwa atakuja kuweka mahari, watu wanajikusanya yeye anakimbia, mzigo wote una letwa kwenye familia. Ni mtu ambaye tunaogopa kumuacha na mama yetu maana mda wote tunaona anaweza kumchoma kisu au kumuua.

Mama pamoja na ukubwa wake baba ana huwa mpiga kama mtoto mdogo tukiwa hatupo na kibaya hachagui kitu cha kupiga kuna kipindi alimpiga mama na chuma.

Alipelekwa jela huko mwenyewe anajua alifanya nini akaachiwa na siyo mara ya kwanza kupelekwa jela. Amekuwa akipelekwa jela kwa kesi za kumfunga miaka mingi lakini cha ajabu anaachiwa tena bila dhamana wala nini.

Siku hizi tume mfukuza nyumbani Maana amezaraulisha familia vya kutosha tu watu wana tutukana mitaani dada yangu mwezi huu alikuwa ana takiwa kuolewa lakini kwao na mchumba wake uyo walikataa eti mtoto wao hawezi kuoa katika familia yetu hii sababu ya tabia ya baba yetu, wanafikiri na sisi watoto tunazo tabia kama za baba

Tumejaribu kupeleka mahitaji yetu kwenye maombi lakini hakuna kinacho badirika watu tumefunga vifungo lakini wapi. Mpaka kuna kipindi nafikia hatua ya kukufuru kusema labda huyu Mungu hayupo kweli mbona hatusikilizi kilio chetu au tunaomba vibaya

Lakini nimefikiria kwa kina Nikaona nijiongeze nitafute waganga wa asili labda anaweza kunisaidia maana uku kwenye makanisa tuna poteza muda tu

Au kama kuna yeyote ambaye anaweza kunisaidia naomba msaada wenu.

Ndugu zangu, ndugu na jamaa sisi tumeshindwa.
 
Huyo ananekana ni mkorofi tu hasa ukiangalia hilo swala la kumpiga Bi. Mkubwa wenu. Uongo ni asili yake wala sio athari ya mapepo.

Miaka 48 sio Mzee, bado anajimudu kabisa. Ikiwa watoto mnajiweza mchukueni mama yenu na mjitenge moja kwa moja na huyo mzee. Ikimaanisha mnavunja nae nasaba zote kiasi hata akifanya mambo yake nyie yasiwahusu.

Akijihisi katengwa kabisa akili itamkaa sawa. Sasa hivi ana kiburi cha kuharibu akijua mpo na mtamuokoa.
 
Nina baba yangu ambaye kwasasa ana umri wa miaka 48, baba yangu huyu tunashindwa kumuelewa kama amerogwa au amejichanganya mwenyewe.

Mwaka 2009 alitupiwa pepo akaanza kutembea uchi mchana kweupe, lifanikiwa kupona akawa sawa na toka siku hiyo amekuwa muongo sana. Anaweza kudanganya watu kuwa anapesa akakopa pesa za watu huko mzigo wote anatupia kwetu sisi watoto wake.

Anaweza kwenda kuoa huko mwanamke mwingine akadanganya watu kuwa atakuja kuweka mahari, watu wanajikusanya yeye anakimbia, mzigo wote una letwa kwenye familia. Ni mtu ambaye tunaogopa kumuacha na mama yetu maana mda wote tunaona anaweza kumchoma kisu au kumuua.

Mama pamoja na ukubwa wake baba ana huwa mpiga kama mtoto mdogo tukiwa hatupo na kibaya hachagui kitu cha kupiga kuna kipindi alimpiga mama na chuma.

Alipelekwa jela huko mwenyewe anajua alifanya nini akaachiwa na siyo mara ya kwanza kupelekwa jela. Amekuwa akipelekwa jela kwa kesi za kumfunga miaka mingi lakini cha ajabu anaachiwa tena bila dhamana wala nini.

Siku hizi tume mfukuza nyumbani Maana amezaraulisha familia vya kutosha tu watu wana tutukana mitaani dada yangu mwezi huu alikuwa ana takiwa kuolewa lakini kwao na mchumba wake uyo walikataa eti mtoto wao hawezi kuoa katika familia yetu hii sababu ya tabia ya baba yetu, wanafikiri na sisi watoto tunazo tabia kama za baba

Tumejaribu kupeleka mahitaji yetu kwenye maombi lakini hakuna kinacho badirika watu tumefunga vifungo lakini wapi. Mpaka kuna kipindi nafikia hatua ya kukufuru kusema labda huyu Mungu hayupo kweli mbona hatusikilizi kilio chetu au tunaomba vibaya

Lakini nimefikiria kwa kina Nikaona nijiongeze nitafute waganga wa asili labda anaweza kunisaidia maana uku kwenye makanisa tuna poteza muda tu

Au kama kuna yeyote ambaye anaweza kunisaidia naomba msaada wenu.

Ndugu zangu, ndugu na jamaa sisi tumeshindwa.
Poleni sana
 
Check na watu wa hospital, ikishindikana check wabobezi kwenye tiba za kiroho. Pana watu wanayo elimu ya kuchungulia ulimwengu wako wa kiroho umekaa vipi na kuuweka SAwa, si ushirikina wala uchawi na sio kufuru . Elimu ni pana.
 
Back
Top Bottom