Naombeni ushauri kuhusiana na biashara ya kuuza mafuta ya kujipaka (lotion/crem),spray na perfume.

Phdum

JF-Expert Member
Apr 15, 2019
807
1,664
Najua hili sio jukwaa la biashara ila kutokana na jukwaa kuwa active sana nimependa niweka uzi wangu hapa hivo naomba isipigwe kapuni na viongozi.
Husika na mada hapo juu napenda sana kuanza hii biashara ya kuuza mafuta,lotion pamoja na perfume kwani kwani ni moja ya mawazo niliokuwa nayo ikiwemo wazo la kuuza nafaka au kununua bajaji used na kuendesha mwenyewe ila hili wazo la kuuza mafuta naona imenitawala zaidi.
nina mtaji wa ml 1+ hapo ukitoa pesa ya shelves,frame n.k yaani hiy m1 ni mtaji nimeamua nitafuta dondoo chache kuhusiana na biashara hii Lakini changamoto niliyonayo ni kwamba sijawahi kufanya biashara yoyote ile kubwa yenye mtaji wa kuanzia elfu 50+.
Kupitia uzi huu ningependa kupata ushauri wa vitu vifuatavyo katika biashara hii.
1.mtaji hasa nilionao huo je unatosha?
2. Je katika biashara hii ni mafuta ya kupaka (lotion/cream) spray au perfume ni bidhaa ipi inauzika sana (najua kuwa kuuza bidhaa inategemeana na mazingira yako ya kibiashara lkn huwa lazima kuwepo kwa bidhaa zinazouzika bila kujali mazingira nadhani wazoefu wa biashara hii wanaweza kusaidia)
3.changamoto zake ni zipi?
4.ni chimbo gani kwa dar naweza kupata bidhaa kwa bei nafuu nikienda kufunga mzigo (kumbuka biashara yangu nimepanga kwenda kufanya kwenye wilaya moja ndani ya mkoa wa mororgoro) au kwa mororgoro mjini kuna chimbo la bei nafuu kufunga mzigo wazoefu naombeni ushauri.
5. Ukiachana na kuwa na Tin namba na leseni ya biashara kuna kitu nahitajika tena kuwa nacho ili nisije nikaingia kwenye misukosuko.
6. Pia unaweza hata kunishauri kuachana na wazo langu hili kulingana na uzoefu wako na kunipa wazo lingine au niboreshe vipi nikianza ili niwe tofauti na wengine.
7. Hili linawahusu wafanyabiashara wote ni namna gani unapanga bei ili mfanane wauzaji wote wa bidhaa inayofanana au inakuwaje bidhaa ile ile muuzaji wa kwanza bei iwe pungufu tofauti na muuzaji wa pili kwa maana kuna wateja wanaokuwa wanazunguka maduka kama 2 au 3 hivi kuulizia bei. Na utajuaje kama vitu vyako unauza bei sawa na wenzako. Naombeni mbinu inayotumika katika sehemu hii ya kutathmini bei.
Ahsanteni nakaribisha ushauri pamoja na kukosolewa nilipoenda tofauti kwenye wazo langu.
 
Mkuu wajuzi wanakuja mimi nawahi siti tuu
Najua hili sio jukwaa la biashara ila kutokana na jukwaa kuwa active sana nimependa niweka uzi wangu hapa hivo naomba isipigwe kapuni na viongozi.
Husika na mada hapo juu napenda sana kuanza hii biashara ya kuuza mafuta,lotion pamoja na perfume kwani kwani ni moja ya mawazo niliokuwa nayo ikiwemo wazo la kuuza nafaka au kununua bajaji used na kuendesha mwenyewe ila hili wazo la kuuza mafuta naona imenitawala zaidi.
nina mtaji wa ml 1+ hapo ukitoa pesa ya shelves,frame n.k yaani hiy m1 ni mtaji nimeamua nitafuta dondoo chache kuhusiana na biashara hii Lakini changamoto niliyonayo ni kwamba sijawahi kufanya biashara yoyote ile kubwa yenye mtaji wa kuanzia elfu 50+.
Kupitia uzi huu ningependa kupata ushauri wa vitu vifuatavyo katika biashara hii.
1.mtaji hasa nilionao huo je unatosha?
2. Je katika biashara hii ni mafuta ya kupaka (lotion/cream) spray au perfume ni bidhaa ipi inauzika sana (najua kuwa kuuza bidhaa inategemeana na mazingira yako ya kibiashara lkn huwa lazima kuwepo kwa bidhaa zinazouzika bila kujali mazingira nadhani wazoefu wa biashara hii wanaweza kusaidia)
3.changamoto zake ni zipi?
4.ni chimbo gani kwa dar naweza kupata bidhaa kwa bei nafuu nikienda kufunga mzigo (kumbuka biashara yangu nimepanga kwenda kufanya kwenye wilaya moja ndani ya mkoa wa mororgoro) au kwa mororgoro mjini kuna chimbo la bei nafuu kufunga mzigo wazoefu naombeni ushauri.
5. Ukiachana na kuwa na Tin namba na leseni ya biashara kuna kitu nahitajika tena kuwa nacho ili nisije nikaingia kwenye misukosuko.
6. Pia unaweza hata kunishauri kuachana na wazo langu hili kulingana na uzoefu wako na kunipa wazo lingine au niboreshe vipi nikianza ili niwe tofauti na wengine.

Ahsanteni nakaribisha ushauri pamoja na kukosolewa nilipoenda tofauti kwenye wazo langu.
 
Ushauri wangu kwako utakapoanza kufanya hiyo biashara pendelea sana kujua kipya kinachoingia mjini na ni kipi wadada wengi wanakipendelea.
 
kwanza nikupe hongera kwa kuwa nawazo hilo ila nakushauri kuwa angalia wadada sikuhizi wanapenda nini, na lotion au mafuta gani yanatakiwa kwao kisha anza biashara yako usifanye biashara bila kufanya utafiti wa hiyo biashara yako ifanyie utafiti kisha anza
 
Mwanzo mzuri wa biashara yoyote ni research kwanza...kuangalia jamii inayokuzunguka inahitaji nini, na nini kinauzika sana kwa wakati huo kulingana na mahitaji ya walengwa. Any ways ni Wazo zuri ila ikuzingatia haya pamoja na kuuliza wazoefu katika biashara hiyo wanaweza kukupa mawili matatu ya kukusaidia. Kila la kheri mkuu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom