Naombeni ushauri juu ya namna ya kupanga bajeti na kuiishi!!!!

UMUNYU

JF-Expert Member
Jan 28, 2017
685
484
Kwa muda wa miaka minne nimekaa na tatizo hili sasa ninadhani ni wakati muafaka wa kuomba ushauri!!

Mimi ninafanya kazi inayoniingizia kwa mwezi sh.700,000/= tasilimu.Sijajenga nyumba ila nina uwanja.

Naombeni ushauri namna ya kupanga bajeti na kuiishi.Nipo jijini Mbeya.

Nimepanga ninalipa sh.100000/= kama kodi ya nyumba kwa mwezi.Kazi ninayofanya inaniacha huru jumamosi na jumapili tu.

Nina mke na watoto wawili.Ingawa siishi nao ila nina wadogo zangu 4 wananitegemea pamoja na mama yangu!Kwa miaka hiyo nimekuwa kama ninapigamarktime!

Bila kusonga mbele.NISAIDIENI NAMNA YA KUPANGA BAJETI NA KUIFUATA!!!!!
 
Mkuu kama una mke na watoto wawili hujajua jinsi ya kuendesha family kuna tatizo mahala

Ila jua tu maisha ni kujibana
Mkuu ninajitahidi kujibana lakini kila ninachohifadhi,mwezi hauishi na chenyewe kinaisha!!Sababu kubwa hata nihifadhi vipi shida hasa za wanafamilia zinatokea mara kwa mara!Labda sijui unamaanisha nini kwa hilo neno kuwa maisha ni kujibana!!!
 
Ni dalili kwamba gharama za maisha zimepanda, na wa kulaumiwa pekee ni Serikali iliyopo madarakani iliyoshindwa kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja ili kuhakikisha linaendana na ongezeko la bei za bidhaa na huduma mbalimbali..
Kweli,kwa sababu kwa hali ilivyo sasa maisha ni magumu na pesa haina thamani
 
Unaposema 'shida za wanafamilia haziishi' ndio kwenye jibu lako. Anzia hapo....usitegemee utazimaliza shida za watu wote,fanya yale yaliyo ya muhimu tu,shida zingine kataa...ishi kibahili sio unaishi kama Mother Theresa hutatoboa ndugu
 
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi!Kiukweli lazima nikiri kuwa ukiwa peke yako ndiyo ulisoma kwenye familiaa ni baraka lakini upande wa pili ni laana kwa muhusika!!!
 
Asante kwa ushauri nitaufanyia kazi!Kiukweli lazima nikiri kuwa ukiwa peke yako ndiyo ulisoma kwenye familiaa ni baraka lakini upande wa pili ni laana kwa muhusika!!!

I know that feel bro, ‘una mke na watoto wawili ila huishi nao’..... kama nimekuelewa vizuri ni kwamba una familia mbili.
Anzia kwenye kuishi na familia yako sehemu moja kama hakuna kikwazo, unapokuwa unaishi ‘kusepa’ kuna namna fulani ya kujisahau ni kama huna majukumu.... japo unakuwa unatuma mchele kwa mkeo na hata ndugu wanavyokuelezea shida zao wanachukulia tu ile uko kisela.
 
Wadogo zako wana umri gani?? Jibane uwawezeshe katika biashara (hata ndogo tu) itakayoweza kusupport maisha yao. That way hawato endelea kukutegemea wewe. Katika maisha lazima itafika point kila mtu atajitegemea kua chachu ya kuwafanya wadogo zako wajifunze kujitegemea. Pili kwanini usiishi na familia yako? Siku zote mji bora unajengwa na vichwa viwili ke na me, inaweza kua huendelei sababu hakuna mtu wa karibu zaidi anayeweza kukushauri.
 
Unataka budget for
Ujenzi?
Kusave?
Or

Incase of ujenzi unaweza anza kwa kununua vifaa. Mfano mawe,mchanga,cement, pesa ya fundi then unaashisha msingi .

Then
Tofali just kidogo kidogo
Cement again
Pesa fundi

Just kidogo kidogo.

Ok pia jaribu kupunguza matumizi yasiyo yalazima kwa familia eg ununuzi wa vimidoli,shopping za supermarket,kwenda kwenye viwanja vya kutulia.

Mama pia mpunguzie budget.
Mke mweleze lengo la kujibana .

Never save to to something.

Legend 700,000 ni pesa kubwa I know you can,you must and you will.
 
Sikukatishi tamaa mkuu, but laki 7 kwa mwezi na kwa muundo wa familia uliyonayo (wewe na familia yako apart, mother na wadogo zako kukutegemea, huo mshahara ni ngumu sana kukutosha. Jifunze kufanya chochote; liwe genge, kibanda cha soup, bodaboda, kilimo, etc. Kama uwanja wako uko pazuri waweza jaribu kufuga hata vikuku 10/20/50??? Hapa lengo sio kukutoa kimaisha, but kukuwezesha kupata experience ya kufanya kingine zaidi ya kazi yako ya ofisini.
 
Asante sana mkuu kwa ushauri wako,nitaufanyia kazi!Ila tatizo ni kuwa kiwanja changu kiko mkoa wa tatu toka nilipo kwa sasa.
 
Sikukatishi tamaa mkuu, but laki 7 kwa mwezi na kwa muundo wa familia uliyonayo (wewe na familia yako apart, mother na wadogo zako kukutegemea, huo mshahara ni ngumu sana kukutosha. Jifunze kufanya chochote; liwe genge, kibanda cha soup, bodaboda, kilimo, etc. Kama uwanja wako uko pazuri waweza jaribu kufuga hata vikuku 10/20/50??? Hapa lengo sio kukutoa kimaisha, but kukuwezesha kupata experience ya kufanya kingine zaidi ya kazi yako ya ofisini.
Nashukuru sana mkuu,nilijaribu kufungua genge!Lakini sikufichi ilikuwa kero upande wa watu wa kodi!Unajua wakusanya kodi wakiishajua kuwa mwenye genge hili ni mtumishi mahali fulani inakuwa kero.Ilibidi nilifunge!!Walinisumbua sana kwani nilikuwa nimeshaanza kuweka na duka pembeni yake
 
Mkuu kama una mke na watoto wawili hujajua jinsi ya kuendesha family kuna tatizo mahala

Ila jua tu maisha ni kujibana
laki Saba haijui aitumiaje? Tena mbeya kwenye vyakula kibao vya Bei POA aiseee.Anyway hiyo nyumba ya laki moja Hama upesi uko mwenyewe vyumba viko Hadi vya elfu 15.kale kwa mama nitilie kwa siku elfu Tano inatosha kula kwa mwezi kwako laki moja unusu chumba elfu 15
 
hebu weka bajeti yako yote kwanza,,,ndio tukashauri
Pango sh.100,000/=
Ada ya mtoto sh.50,000/= kwa mwezi
Akiba sh.200,000/=
Maji na umeme sh.50,000/=
Chakula sh.200,000/=
Mavazi sh.50,000/=
Matibabu (Bima ya afya)
Sadaka sh.30,000/=
Mengineyo sh.20,000/=
 
Kingine mwanamke kama ni mama wa nyumbani mtafutie kimradi chochote awe anakusaidia hela ya chumvi na sabuni harafu wewe utatue mambo makubwa makubwa
 
Back
Top Bottom