Naombeni ushauri: Je, nimuache binti niliyezaa naye ili niwe na binti niliyekuwa naye kwenye mahusiano tangu chuo?

Geredi

Member
Nov 18, 2020
42
19
Habari ya muda huu wanaJF

Mwaka 20×× nilipojiunga na Chuo kikuu nilibahatika kuwa na Binti katika mahusiano na tukadumu mpaka namaliza Chuo na kufikia hatua huyo Binti nilimtambulisha nyumbani Kwa wazazi.

Sasa shida inakuja hapa. Kwa Sasa Niko na almost 35+ yrs ila bado sijaoa Kwa kufunga Ndoa kabisa.

Nilipomaliza Chuo kimoja hapa Tz, mwaka huo huo nilipata offer ya kwenda kusoma China -China Agricultural University (CAU) ni Chuo kikubwa tu Kwa wanaokifahamu.

Nilipoenda huko Kwa muda wa miaka miwili nilikuwa nawasilina vyema kabisa na huyu Binti hadi narudi, ila bahati mbaya Kuna dada hivi nikawa nimelala nae na akashika Ujauzito now mtoto ana 1.5 yrs old. Katika Hilo nikaamua nimchukue huko kwao niishi nae hapa nilipo maana kwao wanahali mbaya kiuchumi na mazingira ya kwao kiujumla.

Binti wa mwanzo niliyekuwa nae Toka Niko Chuo Tz.. nikamwammbia "for now Niko na mtoto na nitamwoa huyu niliyezaa nae japo haikuwa matazamio yangu naomba unielewe mahusiano yetu yaishie hapa"

Huyu Binti hajataka kunielewa kabisa bado analazimisha nimrudie yeye akidai ya Kwamba atamlea mwanangu.

Sasa huyu niliyezaa nae nilimwambia kwamba Chuoni nilikuwa na mtu hivi na hivi ila Kwa Sasa hakuna kilichopo btn us, Sasa Kuna siku kaona sms za kitambo sana nilisahau kuzifuta zingine Whatsapp na picha baadhi tukiwa katika mikao ya tofauti kidogo mnaelewa ukipiga picha na mpenzi wako zinakuwaje.

Sasa huyu kamind sana anadai anaondoka na mtoto na nisimtafute Tena na akiondoka anabadili hadi line Kwa maana ya kwamba nisiwahi mwona hata mwanangu. Madai yake kwamba bado Niko na huyu Binti niliyekuwa nae Toka niko Chuoni miaka ya nyuma na bado nampenda, kitu ambacho Mimi nishakifutilia mbali japo kweli nilimtambulisha.

Nimwache aondoke kama anavyodai nimrudie huyu niliekaa nae muda mrefu kwenye uchumba, Au nitumie Busara gani hapo wanaJF maana imeshakuwa changamoto hakuna amani ndani na Mimi nampenda sana mwanangu sitaki akose malezi ya Baba na Mama.

Naombeni mawazo yenu.
 

Lovebird

JF-Expert Member
Sep 27, 2012
4,293
4,128
Kale ka wimbo ka shetani na mama mkweee wake wamenikalia; we kanyaga twende ushalikoroga huna budi kulinywaa.

Anyway mtoto wa mwenzio mwone ka mtoto wako, maamuzi ya mwisho ni yako na si vinginevyo.
 

Geredi

Member
Nov 18, 2020
42
19
Tumia akili kulishinda Hilo kwan kwa upande wangu naona kosa ni lako. Ukioa acha ujana, mapichapicha yako ya kale yafute vinginevyo utakuw umenogewa na papuchi za kale.
Kama umenielewa vyema, nimezaa nae ila sikuwahi zifahamu tabia zake hapo awali maan sikukaa muda sana nikawa naishi nae ndani kabsa, ana kiburi sana, Hana heshima Kwa mmewe na mambo mengine mengi ya ndani zaidi .. nafikiri unaelewa mke inabdi afanye Nini Kwa mmewe.

Hilo pia linanipa changamoto sana , na mtoto siwez mwacha alelewe na mama pekee utata wa maamuzi unakuwa hapo.
 

Me I and my self

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
3,570
7,354
Yani kwa ufupi ulibadili ladha kutoka cha zamani kuingia kipya.

Vijana usikae na mtu mkawa mnafanya mapenzi mnadanganyana eti uchumba mtachokana sana na mwisho wa siku mmoja akipata mpya huwa imeisha.
 

Humilis

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
750
732
Labda wa pili hukumpenda sana na uliamua kuwa nae tu kwa sababu ya kumuonea huruma hali ngumu kwao na kwa sababu ya mtoto.

Huyo wa mwanzo ni kama muelewa zaidi,maana kusamehe uliyomtendea na akakubali muanze upya si jambo rahisi.

Hiyo dalili ya kutaka kuondoka na mtoto kisa tu kaona mambo ya nyuma si nzuri,na ni kama ishara ambayo umeoneshwa ili ujue uhalisia wake.

Omba msamaha kwa wa kwanza,kwa uliyomtendea,aponye nafsi yake maana hujui ya BAADAE.Tengeneza na wa pili ili aone kuwa hakuna utofauti kati yenu kwa usalama wa mwanao.Kama unaweza kuweka distance kati yenu(na wa pili) ingefaa upate wakati wa kuyatafakari upya maamuzi uliyoyafanya bila kutafakari vya kutosha
...utapata jibu sahihi zaidi na utajua cha kufanya.
 

Liverpool VPN

JF-Expert Member
Aug 29, 2020
3,271
6,507
Habari ya muda huu wanajf.

Mwaka 20×× nilipojiunga na Chuo kikuu nilibahatika kuwa na Binti katika mahusiano na tukadumu mpaka namaliza Chuo na kufikia hatua huyo Binti nilimtambulisha nyumbani Kwa wazazi....
Anyway hayo ya ndoa MI HUWA HAYANIHISU.

Nina swali?

Ukiwa China unasoma Postgraduate unaweza kufanya Kazi?

Yaani unaweza kwenda kusoma halafu ukarudi na mpunga mwingii wa madili ya nje ya chuo na huku chuo masomo yakaenda vizuri?

#YNWA
 

Geredi

Member
Nov 18, 2020
42
19
Labda wa pili hukumpenda sana na uliamua kuwa nae tu kwa sababu ya kumuonea huruma hali ngumu kwao na kwa sababu ya mtoto.

Huyo wa mwanzo ni kama muelewa zaidi,maana kusamehe uliyomtendea na akakubali muanze upya si jambo rahisi.

Hiyo dalili ya kutaka kuondoka na mtoto kisa tu kaona mambo ya nyuma si nzuri,na ni kama ishara ambayo umeoneshwa ili ujue uhalisia wake.

Omba msamaha kwa wa kwanza,kwa uliyomtendea,aponye nafsi yake maana hujui ya BAADAE.Tengeneza na wa pili ili aone kuwa hakuna utofauti kati yenu kwa usalama wa mwanao.Kama unaweza kuweka distance kati yenu(na wa pili) ingefaa upate wakati wa kuyatafakari upya maamuzi uliyoyafanya bila kutafakari vya kutosha
...utapata jibu sahihi zaidi na utajua cha kufanya.
Asante Sana Kwa mawazo yako Bora nitayafanyia kazi ..
 

Geredi

Member
Nov 18, 2020
42
19
Waache wote, hudumia mtoto akifikisha umri wa kusoma ukamchukue uishi nae..
Maana
1. Wa kwanza unampenda ila huna bahati nae.
2. Wa mtoto huna upendo nae.
Yaani kama upo kichwani mwangu kabsa , sema tatizo linakuja wapi, anadai kwamba hatokaa nimwone Wala mtoto kumwona ndio itakuwa Mwish japo ukweni nakufahamu.. Kwa huyu Binti, anadai hata nyumbani hatokaa.
 

Geredi

Member
Nov 18, 2020
42
19
Anyway hayo ya ndoa MI HUWA HAYANIHISU.

Nina swali?

Ukiwa China unasoma Postgraduate unaweza kufanya Kazi?
Yaani unaweza kwenda kusoma halafu ukarudi na mpunga mwingii wa madili ya nje ya chuo na huku chuo masomo yakaenda vizuri??

#YNWA
Ndio it's guaranteed 80% kufanya hivo, Mimi nilikuwa multtask kbs muda wote busy, na muda wa kuwa shuleni apo ni mdogo tu sana sana research hizo ndio zinachukua muda wako.
 

Abbyrutha

Senior Member
May 29, 2019
170
240
Kama umenielewa vyema, nimezaa nae ila sikuwahi zifahamu tabia zake hapo awali maan sikukaa muda sana nikawa naishi nae ndani kabsa, ana kiburi sana, Hana heshima Kwa mmewe na mambo mengine mengi ya ndani zaidi .. nafikiri unaelewa mke inabdi afanye Nini Kwa mmewe

Hilo pia linanipa changamoto sana , na mtoto siwez mwacha alelewe na mama pekee utata wa maamuzi unakuwa hapo.
Unajuaje kama huyu wa chuo ana heshima na hana kiburi ukiishi nae?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

4 Reactions
Reply
Top Bottom