Naombeni ufafanuzi wa hili suala kuhusu kutenganisha 'siasa' na 'uongozi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni ufafanuzi wa hili suala kuhusu kutenganisha 'siasa' na 'uongozi'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MAHENDEKA, Jul 9, 2010.

 1. MAHENDEKA

  MAHENDEKA JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 257
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 45
  Serikali inaposema inajaribu kutenganisha siasa na uongozi ina maana gani?.Unapokuwa mwanasiasa ni lazima usiwe kiongozi? na mbona huku vyuoni tunakosoma kuna baadhi ya degree program mfano political science and public administration hazitenganishwi?mtu anayesoma hii anaandaliwa kuwa nani hasa?
   
 2. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  1. kutenganisha siasa na uongozi kwenye nchi shaglabaghala kama ya kwetu labda nadhani ni serikali kutoingilia sehemu za uzalishaji ambazo imebakiza hisa tu baada ya kugawa percent kubwa kwa mzungu au tapeli mwingine in the form of kigogo. Hivyo ni kusema sisi ni shareholders na atuna influence katika uongozi huo mfano NBC.-------------

  2. Kusoma political science aina maana wote watakuwa wanasiasa, kwanza wengi uishia kuwepo kwenye body za ushauri na jinsi ya ku-tackle social problems. Mara nyingi ndio wao ufanya ma-research na kuwapa wanasiasa mistari ya kubishana kwenye kutengeneza policies. Funny enough nchi za dunia ya kwanza wanasiasa wengi ni maloya na wachumi kuliko watu waliosoma first hand sayansi za jamii.-------------------

  Well kwenye nchi ambayo political parties bado kutujuza yafuatayo: political approach, spending prioprities, perspective itakayoleta maendeleo na plan itakayoleta mandeleo. Anybody can be anybody usistaajabu ukisikia fundi bomba kawa mmbunge wako. Kwani amna science bado katika siasa, so far ni ufisadi na jinsi ya kuumaliza ufisadi hata hao our beloved CHADEMA have yet to convince us wana mipango gani ya kutuletea mabadiliko realistically.
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mods paragraph tena mbona azikubali au?
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kutenganisha Siasa na Uongozi ina maana - Mbunge (Mwanasiasa) hawezi kushiriki ktk Uongozi wa serikali kwa mfano kuwa Waziri au Naibu Waziri - n.k..
   
 5. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  kaka

  hivi unaweza kuwa waziri bila ya kuwa mmbunge katika siasa zetu tulizo achiwa na mkolononi? au hata mmbunge, waziri, raisi na yeyote anaelitumikia taifa katika kutunga sera si ni mwanasiasa au labda mimi tafsiri yangu imepitwa na wakati?
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Yap!...nakubalina na wewe kabisa kwamba kulingana na watu wetu, mazingira yetu hii habari ya Mbunge kuwa mtunga sheria kisha yeye mwenyewe ndiye yupo jikoni huko wizarani sidhani kama inawezekana kutekelezeka pasipo kumpa madaraka makubwa rais ya Udikteta. Yaani mfumo mzima wa kiutawala kwa nchi zetu ni Kitendawili, wenzetu wanaweza kushika wadhifa hizi na chama kinakuwa responsible kwa makosa yoyote yanayofanyika chini ya wizara yoyote kwa sababu wanafuata itikadi fulani au laa kuna chombo kingine kinachopitisha sheria (approval) baada ya kujadiliwa na kupendekezwa na Bunge.

  Sisi kwa bahati mbaya woote ni maskini wa hali na mali na kila tunapokabidhiwa madaraka kitu cha kwanza ni kutoka!...kutoka ktk umaskini na kuitwa mheshimiwa ambao huja na hadhi fulani ya kimaisha na kujisikia..hapo ndipo siasa na ahadi zote zinashindwa kutekelezeka baada ya kukabidhiwa madaraka..

  Kama tutaweza kutenganisha siasa na Uongozi kwa aina fulani ya mfumoambao utawabana viongozi wetu nje ya siasa zetu za Majungu maana hatuna itikadi basi bila shaka tutakuwa tumejenga Upya sura ya Kiutawala ambayo itaweza kuwawajibisha viongozi wanaotumia siasa ktk utekelezaji wa kazi zao kama viongozi.
   
Loading...