Naombeni ufafanuzi wa fedha ya ruzuku mashuleni maana kuna kutofautiana juu ya waraka huu, nahitaji

Doto1897

Member
Jun 12, 2011
14
0
MATUMIZI YA RUZUKU YA UENDESHAJI(CAPITATION GRANTS)

Serikali itaendelea kutuma 50% ya ruzuku mashuleni kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya kujifunzia na kufundishia. Utaratibu huu wa kupeleka sehemu ya fedha ya ruzuku ya uendeshaji moja kwa moja kutoka hazina kwenda shuleni unalenga kuondoa urasimu usio wa lazima ili kuimarisha ubora wa elimu itolewayo.

Kwa muongozo huu, inaelekezwa matumizi ya ruzuku ya uendeshaji inayotumwa moja kwa moja shuleni itumike yote kwa ununuzi wa vifaa vingine vya kufundishia na kujifunzia kwa asilimia mia moja(100%). Vifaa hivi ni pamoja na kemikali, vifaa vya maabara, tufe, vivunge vya sayansi, vivunge vya mwili wa binadamu na vifaa vinavyoendana na hivyo. Utaratibu wa ununuzi wa vifaa hivi utasimamiwa na Bodi za shule, na utazingatia kanuni na Taratibu za manunuzi ya umma, na utazingatia vipaumbele vya shule husika.
 
Back
Top Bottom