Naombeni ufafanuzi kauli ya "Mshahara wa dhambi ni mauti"

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
42,268
105,487
Wakuu,
Nna maswali kadhaa najiuliza:-
1. Kama kweli mshahara WA dhambi ni mauti, Ina maana TULIOWAZIKA WOTE NI WATENDA DHAMBI

2. Kama kweli mshahara WA dhambi ni mauti, Kwaiyo WASIO NA DHAMBI HAWAFI?

3.Kama mshahara WA dhambi ni mauti, Je Zinazungumziwa dhambi aina zote ndo zinapelekea kifo au Kuna dhambi specific ambazo mtu akizifanya anaadhibiwa kwa kifo?

4. Dhambi zinazoongelewa kwenye huo msemo ni kitu gani hasa,

Je dhambi maana ake ni kuvunja TU zile AMRI 10 za Mungu au kuna AMRI nyingine zaidi ya zile 10?

Mbona inasekana pia kua
-ULAFI ni dhambi, Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo

-UCHOYO ni dhambi, Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo

-UBAHILI ni dhambi, Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo

-UNAFIKI ni dhambi,Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo.

NAOMBA KUULIZA PIA,
"uchawa" vipi, Hivi nao sio dhambi?

Nawasilisha🙏
 
Kiuhalisia Hakuna Dhambi.

Sin is an imaginary disease invented by religion founders to sell an imaginary cure.

It's like creating Virus to sell Anti-Virus.

Tukirudi kwenye mafundisho ya kidini,

Kama mshahara wa dhambi ni mauti, Mbona Shetani mwanzilishi wa dhambi yupo hai mpaka leo?

Kama kweli mshahara wa dhambi ni mauti, Baada ya shetani kutenda dhambi na kumuasi Mungu mbinguni angekufa.

Lakini Holaaaa, Shetani bado anadunda tu!!

Hivyo mshahara wa dhambi si mauti.

Hizo ni hadithi za biblia za kukupumbaza tu.

Uwe na dhambi, Usiwe na dhambi. Kifo kipo palepale.

Achana na vitisho uchwara vya hekaya za Biblia.
 
Mshahara wa dhambi ni mauti kweli japo sometimes naye Mungu anabidi akumbushwe kutimiza wajibu wake.

Ila sema hapa kidogo tu Sheikh Kishki alimchanganya Allah hakuwa specific hakusema Ramadhani ya mwaka gani.

Mauti si ile ya kimwili.Adamu aliambiwa atakufa kama atakula tunda.Lakini aliishi miaka 900 hivi.Mauti ni kujitenga na Mungu.
Amri ya kumpenda mwenzio kama nafsi yako imejumuisha mambo yote yasiyoingizwa katika amri kumi za Mungu.
Mwenye dhambi na asiye na dhambi wote wanapatwa na mauti kimwili lakini roho zinaendelea kuishi zikisubiri mishahara ya mauti au Uzima wa milele.Lakini Mungu ametupa nafasi ya kuchagua moshara tunayotaka
 
Najua unampango wa kuwa chawa mkuu ndiyo maana unauliza kama ni dhambi.

Ukiwa chawa huku unamalinda yako yote 20 yamenyooka vizuri mpaka chini sio dhambi kabisa mkuu japo kuwa kumkuta chawa ana malinda ni ngumu sana.
Ha ha ha......sio kweli bhana mkuu
 
Mauti inayozungumziwa hapo ni mateso ya jehanam milele! Pale ambapo utakuwa unateseka milele motoni kwa ajili ya dhambu zako! Kuna tofauti ya kifo na mauti kifo kinamfika kila mmoja uwe mtakatifu au mwenye dhambi ila mauti ni kwa wenye dhambi tu!

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.

Ufunuo 21:8
 
Wakuu,
Nna maswali kadhaa najiuliza:-
1. Kama kweli mshahara WA dhambi ni mauti, Ina maana TULIOWAZIKA WOTE NI WATENDA DHAMBI

2. Kama kweli mshahara WA dhambi ni mauti, Kwaiyo WASIO NA DHAMBI HAWAFI?

3.Kama mshahara WA dhambi ni mauti, Je Zinazungumziwa dhambi aina zote ndo zinapelekea kifo au Kuna dhambi specific ambazo mtu akizifanya anaadhibiwa kwa kifo?

4. Dhambi zinazoongelewa kwenye huo msemo ni kitu gani hasa,

Je dhambi maana ake ni kuvunja TU zile AMRI 10 za Mungu au kuna AMRI nyingine zaidi ya zile 10?

Mbona inasekana pia kua
-ULAFI ni dhambi, Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo

-UCHOYO ni dhambi, Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo

-UBAHILI ni dhambi, Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo

-UNAFIKI ni dhambi,Ila kwenye zile AMRI 10 za Mungu haimo.

NAOMBA KUULIZA PIA,
"uchawa" vipi, Hivi nao sio dhambi?

Nawasilisha🙏
Hehehe
 
Mfano ukiiba unaweza kufungwa au kuuawa(mauti),ukizini unapata magonjwa,laana gundu Nk yaani.umauti sio mpaka ufe kimwili.
 
Ina maana ubaya uliomfanyia mwenzako utakurudia. Mf. Umemrushia mwenzako jini, likakuta kinga na kurudi kukumaliza wewe. Kama hungerusha jini haungekufa.
 
Atoe ufafanuzi Sasa, mauti na kifo tofauti yake ni nini
Kwa kifupi;

Kifo ni kitendo cha nafsi/roho kutengana na mwili. Hii ina maana kuwa wote tuliowazika wamekufa. (Bila kujali wamekufa katika dhambi au la).

Kwa upande mwingine, mauti ni kitendo cha nafsi/roho kutengana na Mungu. Hii inatokea/itatokea baada ya kifo. Maana yake ni kuwa, dunia ikifika mwisho, wote waliokufa katika dhambi watatengana na Mungu (mauti) wakati wale wasiokufa katika dhambi wataungan na Mungu (uzima wa milele.

Asante
 
Back
Top Bottom