Naombeni tufurahi pamoja, mungu kanibariki na mtoto wa kiume.

hongera sana mkuu, nisalimie familia!

Usijali mkuu nadhani wife atafurahi sana nikimwambia kuna salamamu kutoka JF, anaijua sana kwani mara nyingi ananiambia unafanya nini muda huo wote kwenye PC au CM?

Ikabidi nimweleze ukweli asije kudhani ninachart na wezi wa ndoa yake.
Kuanzia hapo akiniona nimetulia anajua niko huku.
Mara nyingi huwa nikipanda kule JOKES na MMU ananiomba achungulie au nimhadithie.

Na huwa sio mara moja kuniuliza vipi leo kuna jipya gani hujo JF?

Atafurahi sana kupata salamu zenu na hongera zenu.

Asanteni sana wadau.
 
Vipi kuhusu jina mkuu???
Chagua na umpe jina la kiubabe,we mwenyewe si unaona nchi yenyewe kila day problems?mara maandamano,mara mgomo,mara ufisadi,
Ebu chagua jina moja hapa mpe,nakuahidi utanikumbuka.
1.Bedui.
2.Kamanda.
3.Adui kuu.
4.Jemedary
Pia:
5.GAIDI
6.NDULI
7.KABURU
8.DICTATOR
 
Mkuu hiki sio kituko and I can not joke on this. This is the real life I live. Ujue watu tuna maisha ya JF, FB nk. But for today haya ndio maisha yangu halisi.
Narudia tena mkuu; Namshukuru sana Mungu, mke wangu amejifungua mtoto wa kiume as our first born.

...hongera...
Hospitali gani..?
 
another chadema leader is borned?

Mh! mkuu mbona mapema hivyo?
Na umejuaje kama mimi cdm? Anyway Mungu amemleta duniani tayari anajua where to place him.

(Naogopa kuweka siasa humu nitaharibu uzi wangu)
 
Hongera sana Dogo!

Angalizo:
Hapo ndiyo mwanzo wa familia.
Mlee mke wako ktk maadili yapendezayo Ulimwengu wa sasa na hata mtoto wetu ambalo ni Taifa la kesho umlee katika sifa impendezayo.

Hongera sana Bwana mdogo!
Msisahau kumtolea Bwana MUNGU wetu zaka impendeyo!

ANDIKO TAKATIFU LASEMA:
""Mlee mtoto katika njia ipendezayo naye hataiacha kwamwe na hata atakapokuwa mzee""
 
Hongera wa kurid , kazza buti .
Kuzaa si kazi ! Mkubwa ,
kazi ndiyo hii unaianza !
K u l e a B a b aa
 
Naungana na wewe katika furaha ya kupata mtoto
Mungu awape afya njema mama na mtoto...
 
Back
Top Bottom