Naombeni tiba ya kisaikolojia: Mwenzenu nikipanda ndege huwa nawaza hatari tupu

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Samahani kwa nitakaowakwaza kwa ushamba wangu!

Mwenzenu nikipanda ndege ikiwa angani huwa naogopa ile mbaya, Hususani nikichungulia dirishani ndo kabisaa!

Vikianza Vile vihudumu vinapoelezea kuhusu maparachuti fastafasta tena kwa kingereza ....ladies and gentleman..... Huwa nasema huyu anasema nini, yaani itokee mbungi huku juu hivi vikarachuti ambavyo hata cjawahi kuvivaa ndo nivae wakati wa hatari vitasaidia kweli?

Kwanza huko angani kuelea tu ule upepo ni mtihani mkubwa KM 5 juu angani hadi ufike chini kuna mtu hapo? Balaa ufikie juu ya nguzo za umeme itakuwaje!?

Kiufupi huwa nateseka sana nikipanda ndege wakati mwingine huwa najuta kwanini nimeipanda nakuacha bus!

Kuna wakati inapokaribia kutua rubani huzima AC kusubiri kuruhusiwa kutua, basi hata kupumua huwa naona kama oksjen inapungua,

Nyie mnawezaje wenzangu! Tena comfortable kabisa huwa nawaona mnaneng'eneka kwenda hadi chooni!

Mnawezaje wenzangu? Samahan kwa hili jaman
 
Pole mkuu
Hiyo Ni shida ya kisaikolojia, Inaitwa fear of flying. Inawashika watu Wengi tu.

Yule Mwalimu wake sarafina kwenye movie ya sarafina, na yeye anafear of flying. Ni mMarekani alipewaga uraia na Raisi wa nchi fulani ya West Africa sikumbuki nchi gani lakini alishindwa kwenda sababu ya fear of flying.
 
Io ni kawaida kwa kila mtu ukipanda mara nying io hofu huondoka

Kuhusu maparashut ni uongo mtupu likitokea la kutokea hata ruban yeye atachowaza alishushegoma wapi maswala ya parashutbado japo kuna madesigner wapo mzigon wanatengeneza reacue system ndege ikizingua tu umarushwa nje na kiti chako parashut litafunguka lenyewe
 
Bora hiyo ila vipi likigoma unashuka kama mshale pyuuuuu
 
Back
Top Bottom