Naombeni Mwongozo Kuhusu Utaratibu wa Bajeti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni Mwongozo Kuhusu Utaratibu wa Bajeti

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gurudumu, Jul 20, 2011.

 1. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #1
  Jul 20, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Wapambanaji natumaini hasira za Jairogate zinapungua sasa. Hivyo naomba sasa mtulie mnipe Mwongozo wa kikatiba na kikanuni kuhusu bajeti ya serikali kwa muktadha wa bajeti ya Nishat na MadiniKwa kuwa sasa tunajua kwamba Kamati za Bunge zimekuwa zikihongwa kupitisha bajeti za serikali,Kwa kuwa Bajeti ya Nishati na Madini ilikutikana na kasoro za ujumlishaji na inasemekana bajeti zote zina kasoro hizo,Kwa kuwa Mkulo na Pinda walikwisha soma bajeti zao na kupitishwa na Bunge,Kwa kuwa bajeti ya Mkulo ilikuwa ni bajeti ya serikali nzima ikijumuisha ya Nishati,Kwa kuwa bajeti ya Pinda ilijumuisha halmashauri zote nchini ikiwa ni pamoja na idara za Nishati na Madini,Kwa kuwa bajeti ya Nishati na Madini imekataliwa hadi ikarekebishwe na kuongezwa kutoka kwenye bajeti za Wizara na idara zingine,JE?1. Baada ya marekebisho ya bajeti ya Nishati na Madini itabidi kurudia kujadili bajeti zilizopitishwa kabla hasa ya Mkulo na Pinda?2. Wabunge wetu wamepoteza sifa na uwezo wa kupitia bajeti za serikali hivyo watafutwe wataalamu ambao kazi yao ni kuchambua na kupitia bajeti za serikali?3. Wabunge wetu waendelee na upitishaji wa bajeti zilizobakia na bila kurekebisha zilizokwishapitishwa kana kwamba kurekebishwa kwa bajeti ya Nishati na Madini hakutaparaganya bajeti zingine?Naomeni majibu ya kikatiba na kikanuni
   
 2. F

  FJM JF-Expert Member

  #2
  Jul 20, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nchi imekuwa inaendeshwa kwa mazoea na sasa tuko kwenye dilema. Mbaya zaidi Spika wa sasa hata uwezo na wala hataki kujifunza. Inakuwaje bajeti ya serikali kuu (national budget) ipitishwe halafu ndio ministerial budget zijadiliwe/zipitishwe? Logic iko wapi hapa?
  Kwa nini watu wazima wasianze kujadili ministerial buget halafu ndio ije budget kuu? Na kwa upande mwingine sion mantiki ya kuwa looooong budget session. Sijui kama bunge letu linajuwa kuwa time is money! Miezi miwili na ushee mnaongelea budget?
   
Loading...