Naombeni Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni Msaada

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Masanilo, Aug 27, 2009.

 1. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Niko kwenye mahusiano kwa muda mrefu sasa kama miaka 3 hivi na tunategemea kufunga Dec kama mambo yatakuwa salama. Siku za hapa karibuni nimehisi Mr wangu anatabia za kishoga. Ana rafiki yake wa muda mrefu huwa kila sehemu wanakuwa naye nimegundua huenda huyo ndiye anayefanya naye mchezo mbaya. Nimeongea naye hataki kuwa mkweli ila nimeisha ona hata meseji akimwita huyo rafikie wa kiume mpenzi. Jamani nifanyaje?
   
 2. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2009
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hapa naona kama hauna ushahidi wa kutosha wa kumtia hatiani huyu Mr. wako mtarajiwa. Fanya uchunguzi zaidi. Je kwako huwa ana rekebisha?
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  wanawake kuitana mpenzi ni kawaida ila sijawahi kuona wanaume wakiitana mpenzi.Kama Mr wako anamiwta mwanaume mwenzie mpenzi...inatia shaka.Chunguza kisha amua.Hata kama kwako yuko kamili...usisahau kuna wanaume wanaweza kotekote....usijikute kwenye triangle mbovu!
   
 4. K

  Keil JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hizo triangles ni nyingi sana na hasa kwenye jamii zetu ambako swala la ushoga bado linafichwa fichwa sana na hasa kwa upande wa wanaume wanaopenda kuwapanda wanaume wenzao. Ili kuficha hilo, wanaume wengi huwa wanaoa ili kuficha ushoga wao. Lakini lazima awe na "Aunt Dume" wa kumshughulikia. Ma-"Aunt Dume" wameshindwa kujificha na wengi wanajiweka wazi, wanaokera ni hao vidume wa ma-Aunt Dume ambao hawataki kujulikana na matokeo yake akina dada wanaishia kuingia kusiko.

  Ni vema mhusika ameshituka mapema, hivyo ana nafasi ya kuchunguza na kufanya maamuzi, kama atakubali ku-share mume na "Aunt Dume" au la, huo utakuwa ni uamuzi wake.

  Swali la kizushi: Kipi kina nafuu kati ya haya mawili, mume awe na "Aunt Dume" amemuweka kinyumba kwa siri ama awe na nyumba ndogo aliyoiweka kwa siri?
   
 5. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  duuuh,pole sana.mie kinachonifanya niwe na huakika ana matatizo ni reaction yake ulivyomgusia hilo swala.kama ingekuwa uongo angekuzibua bonge la bao kwanza kwa kumvunjia heshima.na je ulivyo muuliza kuhusu hio msg alijitetea vipi manake sio kawaida wanaume kuitana "mpenzi" hata siku moja.ushauri wangu wa mwisho mchunguze zaidi kabla ujafanya maamuzi makubwa ya ndoa kwani hilo swala litakuwa doa kubwa sana hapo baadae wakati mkiwa na familia yenu.
   
 6. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2009
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180

  Afu unategemea umbadilishe mkishaoana?
   
 7. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #7
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Kama ni kweli kumbuka una hatari ya kuambukizwa ukimwi hivyo it is up to you to protect yourself.
   
 8. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Tafadhali Mwamtama, mchunguze huyo mchumba kabla ya kuingia ndoani. Hilo la kumuita mpenzi mwanamume mwenzake hata mie naona kuna walakini, maana kwa wanawake si ajabu kuitana hivyo.
  Once again mchunguze huyo, uamue mapema kusuka au kunyoa.
   
 9. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  duu hapo mie hoi kabisa, yaani kumuuliza mpenzi wako swali kama hilo kweli ni ishu...kuna walakini mahali.
   
 10. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #10
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  ACHA WASIWASI WEWE BIBIE HUYO MCHUMBA WAKO SIO SHOGA WALA NINI SEMA KASEVU JINA LA KIMEO CHAKE CHA NJE KINACHOMPA MAMBO MATAMU KWA JINA LA RAFIKI YAKE UNAYEMFAHAMU WEWE ILI HATA UKIONA SIMU INAITA WEWE HUSIIPOKEE. SASA TATIZO WEWE UMEENDA BEYOND HADI KUSOMA MESEJI KWENYE SIMU YA MCHUMBAKO NDIO MAANA UMEONA HIYO MESSAGE UKAPATA KIWEWE.
  THEREFORE ENDELEA NA MIPANGO YA HARUSI KAMA KAWAIDA UTAVUNJA HIYO MIPANGO BAADAE UTAJUTA UTAKAPOUJUA UKWELI.
  MIMI NINA MSHIKAJI WANGU ANA HIYO TABIA NAMBA ZA VIMADA WAKE ANASEVU MAJINA YA WASHIKAJI ZAKE, WIFE AKIONA INAITA UTASIKIA ''MUME WANGU NJOO SHEMEJI EMMANUEL ANAPIGA SIMU'' KUMBE HAPO ANAPIGA HALIMA
  fanya uchunguzi kwanza kabla ya kulivua pendo ukaja juuuta bure
   
 11. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  wasiwasi wa huyo mrembo tu wala mchumbake sio shoga, aache mapepe na papara, atajuta huyo hasipokuwa makini
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Hii kali Mr anachibwa kisamvu...ama kweli kuna wanaume wanaibisha sana ...dada kuwa makini na huyo jamaa!
   
 13. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #13
  Aug 27, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mhh! utata mtupu hapo... kwani gwaride analichezaje? Kama yuko fiti ujue ni uzushi tu...
   
 14. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #14
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  imenikata maini kabisa.....
   
 15. B

  Bao3 JF-Expert Member

  #15
  Aug 27, 2009
  Joined: Aug 7, 2009
  Messages: 318
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kwani wao kuitana wapenzi imehalalishwa na nani? Yaweza pia kua dalili ya kusagana, who knows?
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  Aug 27, 2009
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  eehh.........
   
 17. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #17
  Aug 27, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kikubwa Mwanamtama ambacho hujatuambia vizuri ni hizo tabia za kishoga ulizoziona! Lakini kama basis yako kubwa ni hiyo message basi naungana na Sipo kukutoa hofu. Kwa kawaida wapiganaji wengi huweka majina ya wanawake kwenye simu wale ambao wife/mchumba anawajua na ambao hawana madhara mfano dada, jirani, mfanyakazi mwenza nk. Lakini akiwa na kitu yake ingine hata kama ni ya zamani huwa haweki jina isipokuwa anatumia majina ya marafiki zake mfano utakuta Juma, Juma2, Juma3.......hapo jua kuwa hiyo Juma3 ni totoz....sio Juma real
   
 18. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #18
  Aug 27, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0

  Kuhalalishwa kunatokana na malezi ya kike na ya kiume kuwa tofauti kwa namna wanavyohusiana.Ni kawaida wanawake kuitana shoga, mpenzi n.k na haileti dhana ya kusagana!
  Jamii inakubali misemo hii baina ya wanawake..naamini ipo pia misemo mahususi kwa wanaume.Misemo hii hutumika pia kwa mfano mama kuwaita wanawe wa kike na wakiume mpenzi..ni namna ya kuonyesha upendo wa kimama kwa wana.Sijui kama baba anaweza kuwaita wanawe mpenzi japo katika lugha za kigeni ni kawaida.Nakumbuka niliwahi kuanzisha thread kuuliza hili huko nyuma.Nitastaajabu sana kumsikia Mr. wangu akimwita mwanaume mwenzake " mpenzi"
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Aug 27, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Naona hii story ni story ya kubumba tupate cha kuongea hapa. huyo bwanake siyo shoga hata dakima moja, ila waume zetu wanapenda kusave namba za wadada wengine kwa majina ya marafiki zao. Chunguza vizuri mumeo ana demu mwingine aliyesevu namba kama jina la rafiki yake. Kama siyo uzushi mwache huyo bwanako haraka sana
   
 20. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #20
  Aug 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Jamani mnashindwa kunielewa kote huko nimechunguza kwa kweli Mr anatabia za kishoga mwanzoni sikuwa namfatilia sana. Kuna siku niliisha mkuta anajaribu sidiria zangu, tight na hata Gstring zangu nikamuuliza vipi mzee akasema anampango wa kuninulia kwa hiyo anajaribu. Sijui kama ni kawaida kwa wanaume wengine kutumia perfume na mafuta ya mwenza wako, kadri siku zinavyozidi kwenda naona tabia nyingi za kike anazo huyu mzee. Hilo la kumuita rafikie mpenzi nadhani ni zaidi ya hapo....siku nikitoka naye tukurudi nyumbani storiz zake ni kusifia wanaume wenzake....
   
Loading...