Naombeni msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naombeni msaada

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Truly, Jun 11, 2011.

 1. T

  Truly JF-Expert Member

  #1
  Jun 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  mchwa wanashambulia fremu za milango, milango yenyewe, makabati ya ukutani. Ajabu hata mchwa wenyewe siwaoni. Mwenye kujua dawa ama namna ya kukabiliana na hili tatizo anisaidie
   
 2. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #2
  Jun 11, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,738
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Nyumba imejengwa kwenye msingi wa namna gani? Kama mchwa wanatokea chini kwenye msingi na kupanda kwenye fremu, hapo kazi unayo. Inabidi utafute professionals watakaotatua hilo tatizo kwa kushughulikia mchwa walioko ardhini chini ya msingi/nyumba. Kama mchwa wanatokea nje ya nyumba yako kupitia mapaa na madirisha, hapo unaweza ukaita wataalam wa "fumigation". All in all, it is very expensive kupata permanent solution. Ndio maana wakati wa ujenzi wa nyumba, suala la mchwa inabidi lifikiriwe toka mwanzo.
   
 3. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Watu wengi kabla ya ujenzi huwa wanazimwagia mbao oil chafu
   
 4. mchakavumlasana

  mchakavumlasana JF-Expert Member

  #4
  Jun 11, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 335
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  maduka ya mbao omc dawa ya mchwa watakupa. Ila kama umeweka sakafu ya cementi toa weka tiles, mchwa hawatapata upenyo. Na kutegemea unapoishi fanya ukaguzi mara kwa mara kwenye kuta nje ya nyumba kubaini mchwa wanapopanda ukuta kuelekea madirishani au milangoni uwauwe,kama una pesa weka madirisha ya alminium(spelling cjui ipo sawa)
   
 5. T

  Truly JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Naona hao mchwa wanatokea chini maana siwaoni nachoona fremu zinakwisha tu. Sasa nitafanyaje na suala la mchwa halikufikiriwa toka mwanzo? Full mawazo maana naona nikibadilisha fremu za milango na milango hao mchwa wanaweza kurudi tena sina hakika na mimi sio mtaalamu wala sina uzoefu wowote wa ujenzi. Nyumba ni ya rafiki yangu ambae aliniachia niishi. Kuangalia iinavyoharibika sio vizuri ndio nawaza cha kufanya
   
 6. T

  Truly JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 223
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Asante kwa ushauri, nitatembelea hayo maduka ya mbao, Nyumba sio yangu na siwezi kubadilisha hivyo vitu maana sina pesa , nilizonazo ni za kubadilisha milango na fremu zake tu. Hawa mchwa kwa kweli wananikwaza maana kama nikiwa sipo kwa wiki moja ndio utakuta mistari ya udongo kwenye ukuta.
   
Loading...