Naombeni aina ya adhabu nje ya kumchapa viboko Mtoto 'Mtukutu' wa kati ya Miaka 7 hadi 9 tu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,516
108,795
Nilidhani Fimbo zangu za Kiserikali / Za Wastani ambazo ni Nne ( 4 ) pekee zingekuwa ni sehemu ya Kumbadilisha Mtoto ila nimegundua ya kwamba hizo ' Bakora ' za Kiserikali hazisaidii kabisa ' Kumuadabisha ' Mtoto hivyo sasa nataka Msaada wenu wa aina ya Adhabu ' Kali ' zaidi za Kumpa Mtoto ili hata ikitokea akiwa anakuona tu popote aanze Kujisikia ' Maumivu ' na kuwa Mpole upesi

Nitashukuru sana kama wale Askari Magereza ( MK ) na wale Polisi Jeshi ( MP ) ambao najua Elimu ya Kutoa Adhabu ni sehemu ya Maisha yenu basi mkanisaidia nazo ili ikiwezekana kuanzia leo nianze ' Kumnyoosha ' nazo Mtoto wangu ili hata akikua mkubwa ajue kuwa ' Mshua ' wake nimembadili na aje kuwa Mtoto mwema kwa Taifa letu hili la Tanzania.

Nataka tu zile Adhabu ambazo hata Wanajeshi au Wafungwa huwa wanapewa ili nianze nazo kwake huyu Mtoto na nipumzike sasa na hivi Viboko.

Nitawashukuruni!
 
Mnyime uhuru wa kile anachokipendaa sana mfano michezo anayopenda ..atanyooka ili asikukasirishe lengo kufanikiwa katika sekta yake ya kile akipendacho

Nataka Adhabu ya Kumuumiza tu Mkuu kwani nimeshachoka sasa Kumchapa Viboko hivi ambavyo naona ni kama vile vimeshamfanya awe tu Sugu.
 
Akae kichura ashike masikio au akalie ukuta huku kashika masikio yake lisaa limoja tu

Ninakushukuru sana Mkuu na nadhani kwa asubuhi hii nitaanza na hii Kwake huku nikiwa naiongeza kadri nae anavyoongeza ' Utukutu ' wake pia.
 
Mlaze chini kifudifudi mfunge mikono na mkandamize na goti shingoni kwa kwa takribani dakika 8

Mbona unanipeleka kule kule kwa Askari Dereck Chauven ambapo alimfanyia Kitu kama hiki Marehemu George Floyd Mkuu? Acha Uuwaji Mkuu!!!!!
 
' Silaaa limoja ' ndiyo Kiswahili cha wapi hiki Mkuu? Vipi umeamka nazo nini? Mnapoingia JF hakikisheni ' Gongo ' zimeshawaisheni Miilini mwenu!!!
Acha tu mkuu Jama nilizitandika balaa.
Ni lisaa limoja.

Wangu namwekaga up to 2hr za alitoka ni kuomba msamaha tu na hicho chumba hajawahi kukichungulia .

Kuna siku namweka na nyoka mdori ili kumtisha zaidi.
 
Akifanya makosa mnyime uhuru wa vile anavyopenda.
Mfano mimi nakumbuka nlikua nkiunguza maharage, au nachezea bakora zangu, alaf kwa siku hiyo habari ya kwenda kucheza na watoto wenzangu ndo inakua imeisha. Knachofata hapo naanza kutumwa kazi, mara kufagia ndani, kufua nguo zangu, kufagia uwanja, kuoga, nakaz zngne tu za ovyoovo, ilimradi tu nikose uhuru. Hiyo hali nlikua naichukia sana zaidi hata ya bakora. Kwaio ilinbdi niwe mpole sana sabab nkifnya kosa tu tayar iyo sku imeharibika na hapo mama ananiambia "skununulii chochote".

Kwa upande mwngne naona kma nlikua napata motivation pia, sabab mama alikua haachi kunletea chochote akitoka sokoni, mfno nguo, na vyakulavyakula ila akikuta nimeharib kaz, ile zawad aninyima. Kwaio nlijkuta najtaid sana niish vile anavotaka mama.
 
Adhabu za aina zote hazijawahi kumbadilisha yoyote kuwa mwema. Badala yake adhabu humtia mhusika hofu, unyonge, kutojiamini, au kuwa korofi, katili au kuvurujikiwa na mwisho kupoteza malengo.

Njia sahihi ya kumfunza yeyote(sio mtoto tu) ni kum-elekeza, kumfundisha, kumshirikisha kwa vitendo na upendo kile unachotaka afanye.
Adhabu ina nafasi yake ila sio lazima fimbo, ngumi, makofi na mateke. Sura yako na maneno/matendo unaweza kuvitumia kama adhabu tosha kwa mwanao.
Ikiwa ni lazima kutumia fimbo, basi iwe ni kwa nadra sana.
 
Mfikiche masikio hadi yawe yanawaka moto huku ukimwambia "mimi nataka haya masikio yawe yanasikia", the most safe punishment kwa watoto. Hizi adhabu nyingine utakuja kustukia siku moja uko Keko, ni mtoto wako ndiyo lakini kwa upanfde mwingine ni kama nyara ya Serikali umekabidhiwa kuitunza kwa niaba yao
 
Nakubaliana na wewe mkuu
Adhabu za aina zote hazijawahi kumbadilisha yoyote kuwa mwema. Badala yake adhabu humtia mhusika hofu, unyonge, kutojiamini, au kuwa korofi, katili au kuvurujikiwa na mwisho kupoteza malengo.

Njia sahihi ya kumfunza yeyote(sio mtoto tu) ni kum-elekeza, kumfundisha, kumshirikisha kwa vitendo na upendo kile unachotaka afanye.
Adhabu ina nafasi yake ila sio lazima fimbo, ngumi, makofi na mateke. Sura yako na maneno/matendo unaweza kuvitumia kama adhabu tosha kwa mwanao.
Ikiwa ni lazima kutumia fimbo, basi iwe ni kwa nadra sana.
 
Nataka Adhabu ya Kumuumiza tu Mkuu kwani nimeshachoka sasa Kumchapa Viboko hivi ambavyo naona ni kama vile vimeshamfanya awe tu Sugu.
Kwani anakukosea nini huyu mtoto?
Kwa nini unamuadhibu, taja makosa yake hapa?
Mama yake yupo au mumetengana?
Ni muda gani unakuwepo nyumbani kwa siku?
Ni siku gani unakuwepo Home siku nzima?
Ulisha wahi toka nae kwenda nae out ? kama unaishi mjini!
Unamleteaga zawadi?
Naomba nijibu haya maswali kabla sijakupa ushauri timilifu.
Asante
 
Majibu....

  1. Ananikosea sana kwakuwa anaipenda sana Klabu ya Yanga na hasa hasa Mchezaji aliyetulaza mapema Simba SC Bernard Morisson.
  2. Namuadhibu ili aachane na Kumshabikia huyo Mchezaji ana ajikite zaidi katika Kuwapenda Wanasiasa John Magufuli na Tundu Lissu pekee.
  3. Wanaume tusiopenda Kupandwa hovyo Vichwani huwa hatufagilii ( hatupendi ) kabisa Kuishi na ama Wake au Wapenzi Wetu Nyumba moja.
  4. Jukumu la Kujua Ratiba zangu za Kuwepo au Kutokuwepo Nyumbani ni la Mpenzi / Hawara yangu labda kama nawe unataka uongeze idadi hiyo.
  5. Ninapokuwa nimempata tu Mwanamke wa Kumlala ( Kumtindua ) huwa nakuwepo Nyumbani Siku nzima na nikitoka jua Condoms zimeniishia.
  6. Kutoka ' Out ' anatoka sana tu kwani hata hivi sasa Mimi nipo ndani ( inside ) na Yeye yuko huko nje ( Out ) anawinda Mijusi aina ya Balangulu.
  7. Nipe Kipengele cha katika Biblia au Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kinachosema ni lazima Baba awe anamletea Mtoto wake Zawadi.
 
Ok ,
Nimekusoma.
Nakusubiria Mirembe Dom au Kidongochekundu Unguja.
Endelea Kupuliza kwa bidii huo Msuba.
 
Back
Top Bottom