Naombeni msaada wenu kuhusu sheria ya mikopo kwa taasisi za kifedha

snboy

Member
Apr 5, 2014
73
95
Wanajamvi habari.

Naomba msaada wenu. Ni sheria ipi inayotoa mwongozo wa taasisi za kibenki na makampuni ya kifedha kupanga riba katika kutoa mikopo? Kuna kampuni maarufu kama Bayport ambayo Director wake kwa hapa Tanzania ni Anna Mkapa inatoza riba hadi 100%. Sheria inasemaje katika hili? Msaada wenu tafadhali
 

Kenzpuls

Senior Member
Oct 22, 2019
171
500
Beyport, platinum, fanikiwa, faidika, Macho credit, Tunakopesha Banc Abc ogopa sana
Apo wana riba za mpka 45% uku mabenk wana riba za 16% mpka 9%
Nkushauri tu achana na ao jamaa
Maana umejiingiza kwenye matatizo hawaruhusu kuuza deni lako au lifuta ata ukiwa na pesa ilo ni lako mkuu , utachelewa pata pesa kwa wakati na ukizingua wanaweza kukukata pesa ata ukimaliza mkopo wao
Uelewa wa mikopo ndo unawaua watu wengi elimu hawana
 

snboy

Member
Apr 5, 2014
73
95
Nimekuelewa mkuu. Ninachotaka kufahamu hapa ni sheria ipi inawaruhusu wao kukata hadi 45%? Je, sheria ya huduma za kifedha zinasemaje kuhusu mikopo na riba zinazokubalika kisheria?
 

Kenzpuls

Senior Member
Oct 22, 2019
171
500
Sheria ipo na inawaruhusu izo sio bank izo ni microfinance wao hawana souce of finance mfano wao wanakopa bank 2 billion wanapewa riba ya 16% sasa wao watapataje faida ikiwa kuna operating expenses kama kodi ya majengo, stationary,Mishahara, Maji so wanachofanya wanaitoa pesa iyo iyo labda 2billions wanaitoa kwa riba ya juu ili wapate faida na kuweza kulipa deni lao mahala husika so kisheria inaruhusiwa awaja jiamulia wenyewe ukisoma sheria mfano MICROFINANCE Policy ya 2000, na sheria nyingine za BOT
 

snboy

Member
Apr 5, 2014
73
95
Asante mkuu.nimekuelewa sana. Lakini nafikiri kuna mswada alipeleka Mpango bungeni kuhusu hizi microfinance. Sasa tatizo hili litaisha maana wamewekewa ukomo wa riba na mambo mengine. Let us wait
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom