Naombeni msaada wanasheria tafadhali

WEWE DADA NI MBISHI...UNATOA MAELEZO MACHACHE ALAFU UNASHAURIWA KWA JINSI ULIVYOELEZA WEWE UNALETA UBISHI...

ENDELEA NA UPUMBAVU WAKO...
 
Kila la kheri mkuu, nenda kituo cha polisi utoe maelezo yote kwa ufasaha ya mchakato wote. Utapewa mtu wa kufatilia hiyo kesi naamini huyo jamaa atapatikana tu na muafaka wa hilo deni lako utafikiwa.
asante sana kwa ushauri jamaa. Mungu akubariki
 
Pole sana mkuu, hii ndio dunia.

  1. Kesi uliyomshtaki hao ndugu iliisha lini? na je ilikuwa ni hukumu ama uamuzi (decree or ruling)?
  2. Ilikuwa ni kesi ya nini (madai, jinai nk)?
  3. Maandishi mliyoandikishana na ndugu, walitamka chochote kuhusu ndugu yao? kama kutaja jina kamilifu la huyo mtoro

Google the Doctrine of Estoppel, itakusaidia dhidi ya hao ndugu hata kama ni kwenye rufaa
kesi iliisha mwaka Jana na tukaendelea kufuatilia nje ya mahakama kuona kama wanaweza hata kufanya kama tulivyokubaliana lakini ilishindikana, hapa kati nilipitia changamoto za kiafya nikasitisha michakato nijitibu kwanza. Ilitoka hukumu ila sijui tofauti za hayo maneno ya kisheria mkuu.
 
Kama utaweza na hutojali, nitumie nakala ya hukumu DM, unaweza kuyawekea vivuli majina yaliyotumika kama hutapenda yafahamike
 
Nitatoa story kwa ufupi ilivyokua, nilimkopea mtu pesa kwenye kikundi zaidi ya milioni kumi, baadae akakimbia na ndugu zake wakaahidi kulipa kwa kusema kuwa Mimi nilipe huko kikundini then wao watalipa ila tuwape muda. Nikajilipia lile deni na tukawapa mwaka mzima walipe. Mwaka ukakata siku ya makubaliano ikafika hawakulipa.

Tukaenda mahakamani wakakataa kuwa siwadai wao ila ndugu yao na hawajui alipo nadhani na rushwa ikatembea wakashinda kesi kwa point kuwa wao si wadaiwa halisi.

Je, naweza kumfungulia huyo aliyetoroka kesi ya wizi wa kuaminika na nikawabana ndugu zake wamfichue alipo coz wanamficha?

Naombeni ushauri wowote au msaada. Nipo Arusha

Nilitamani utuambie ni kitu gani kilichowekwa dhamana wakati wa kukopa? Nyumba,Gari,Shamba au nini?
 
asante kwa moyo wako mkuu. Niliifuatilia sana hati ya hukumu ikawa napigwa tarehe tuu hadi nilivyoanza kuumwa na kusitisha ufuatiliaji
 
aliweka shamba lenye nyumba ambayo haijaisha kumbe akazunguka na kuiuza na kukimbia kwahiyo alikua na hati mbili moja aliyotupa na moja aliyouzia
 
Asanteni wote mnaoendelea kujali, natamani ningepata mwanasheria wa kunisaidia au mtu yeyote mwenye nafasi ya kufanya hivyo.nipo arusha
 
asante kwa moyo wako mkuu. Niliifuatilia sana hati ya hukumu ikawa napigwa tarehe tuu hadi nilivyoanza kuumwa na kusitisha ufuatiliaji
Sasa unatakiwa kufuatilia hiyo nakala ya hukumu. Kufuatilia ni kwa kuandika barua ya kuomba kupewa nakala hiyo sio kwenda tu na kuongea na makarani, weka vitu kwenye maandishi.

Kwa ulivyokuja kuomba ushauri hapa, tafsiri ni kuwa unahitaji msaada kupata fedha yako, itakulazimu kuwa serious ili uweze kupata msaada huo unaouhitaji.

Tafuta nyaraka zote kwa ukamilifu (mkataba wa udhamini wa mkopo ambao mara nyingi ndio mkataba wenyewe wa mkopo, hati mliyoandikishana na hao ndugu, nakala ya hukumu na chochote kile unachofikiri kina msaada kwako).

Hapo utaweza kusaidiwa au kushauriwa kwa usahihi.
 
kwahiyo mkuu naweza kurudi mahakamani na kuomba hivyo vyote? Kwasababu Yale maandishi yalibaki huko je naweza kupewa lile file?
 
Huyi mtu uliyemkopea aliacha picha, vitambulisho vyovyote kama hakuacha tafuta wakili mzuri uwabane hao ndugu zake
 
Nitatoa story kwa ufupi ilivyokua, nilimkopea mtu pesa kwenye kikundi zaidi ya milioni kumi, baadae akakimbia na ndugu zake wakaahidi kulipa kwa kusema kuwa Mimi nilipe huko kikundini then wao watalipa ila tuwape muda. Nikajilipia lile deni na tukawapa mwaka mzima walipe. Mwaka ukakata siku ya makubaliano ikafika hawakulipa.

Tukaenda mahakamani wakakataa kuwa siwadai wao ila ndugu yao na hawajui alipo nadhani na rushwa ikatembea wakashinda kesi kwa point kuwa wao si wadaiwa halisi.

Je, naweza kumfungulia huyo aliyetoroka kesi ya wizi wa kuaminika na nikawabana ndugu zake wamfichue alipo coz wanamficha?

Naombeni ushauri wowote au msaada. Nipo Arusha

Unamkopesha mtu 10 milion bila hata ya kuwa na dhamana kitu chake chochote.. utakua tajiri sana mana haiingii akilini kabisa how do you even start?? Siku hizi mtu ukimkopesha inatakiwa umkopeshe hela ambayo hata asipokulipa haitakuumiza wala kukupunguzia kitu kama alitaka 10 milion ungempa hata laki nyngne akaombe kwengne hata asingerudisha wala isingekusumbua
 
Kila la kheri mkuu, nenda kituo cha polisi utoe maelezo yote kwa ufasaha ya mchakato wote. Utapewa mtu wa kufatilia hiyo kesi naamini huyo jamaa atapatikana tu na muafaka wa hilo deni lako utafikiwa.
Hiyo ni kesi ya madai, polisi hawahusiki kwa sasa.
 
Pole sana mkuu, hii ndio dunia.

  1. Kesi uliyomshtaki hao ndugu iliisha lini? na je ilikuwa ni hukumu ama uamuzi (decree or ruling)?
  2. Ilikuwa ni kesi ya nini (madai, jinai nk)?
  3. Maandishi mliyoandikishana na ndugu, walitamka chochote kuhusu ndugu yao? kama kutaja jina kamilifu la huyo mtoro

Google the Doctrine of Estoppel, itakusaidia dhidi ya hao ndugu hata kama ni kwenye rufaa
Estoppel haifanyi kazi katika mazingira haya, mshauri vizuri.
 
Nilichokiona kwa dada mtoa post; dada si mjuzi wa mambo ya sheria kabisa na alikuwa amemwamini sana huyo mdaiwa na pengine ndugu zake ni watu wanaofahamiana nae sana.

Dada katika maisha yake hajawai kukutana na watu close wanaoweza kumgeuka.

Nakushauri dadangu tumia watu ambao hao ndugu wa mhalifu hawawezi kugundua kama una ukaribu nao ili kuweza kupata contacts za huyo mwizi/tapeli.
Kama baadhi ya ndugu ni wanaume(mfano wanakunywa pombe bar) Tenga hata laki ya kumnunua barmaid mzuri ili amnase mmoja wao na akutafutie mawasiliano ya mhalifu.

10m ni hela nyingi.
 
Back
Top Bottom