Naombeni msaada wa tiba ya kuongeza damu kwa haraka kwa njia asili

Tumia juice ya rozella its so cheap nunua Yale majani yanauzwa sokoni unachemsha kama chai yakipoa unakunywa glass Mbili kwa siku, chemsha matembele na unywe yale maji yake hata njia hii ni nzr pia
Hakika hii itakusaidia sana, imejaribiwa na kuleta matokeo ambayo nimeyashuhudia kwa karibu. Siku hizi hata tea bags za Rosella hupatikana madukani haswa kwenye supermarkets. Ndani ya wiki moja matokeo utayapata. Usisahau sala kwa Mwenyezi Mungu kwani yeye ndiye aponyaye na ndiye muumbaji pasipo yeye hata utumie nini uzima haupo.
 
Naombeni msaada jamani kwa mtu anayefahamu njia bora ya asili ya kusaidia mtu kuongeza damu mwilini kwa haraka bila kutumia dawa za hospital.
Lishe bora pekee (Balanced diet) ndio itarudisha damu kwa haraka.

Hakuna mzizi au gome la mti au mboga ya majani pekee wala tunda lolote peke yake lenye uwezo wa kurudisha damu bila kula balanced diet.

Hivyo dawa pekee ya asili ya kurudisha damu ni kula mlo kamili/ balanced diet sababu kitaalamu mwili huchukua/ hutumia virutubisho kwa kiasi kile tu inachokihitaji, ziada huifadhi kwenye store yake na ziada nyingine utolewa mwilini.

Ulaji wa virutubisho vya aina moja (e.g. rosela pekee, bit root pekee, n.k.) havitakusaidia.

Pia ili mwili huweze kutengeza damu huitaji virutubisho mchanganyiko ambavyo utavipata kwenye mlo kamili pekee.

Mwisho: Dawa pekee ambayo itarudisha damu haraka ni daily NUTRITIONAL SUPPLEMENTS pekee ambayo itakua inavirutubisho vyote kwa pamoja ambavyo vinahitajika na mwili wa binadamu ili kuweza kufanya kazi zake kwa ufanisi.

NB: Unaweza ni inbox nikutajie supplement itakayo rudisha kiasi kikubwa cha damu yako kwa wk 1 tu!
 
Tengeneza juisi ya matembele unywe.
Pia beetroot wanasema inasaidia, kula hilo!
 
Maparachichi ni kiboko aisee, nilikuwa nakatabia ka kula parachichi kila siku asubuhi kabla sijala kitu chochote, hali hii ilipelekea kuwa na damu nyingi, pili ngozi yangu ilikuwa soft na yenye kuvutia sana
Mimi sifanyi chochote ila nna damu 14.7, sijui imetokana na nini?
 
Changanya tende na maziwa fresh yaliyochemshwa kunywa mara kwa mara, inatoa majibu kwa muda mfupi sana!
 
Naombeni msaada jamani kwa mtu anayefahamu njia bora ya asili ya kusaidia mtu kuongeza damu mwilini kwa haraka bila kutumia dawa za hospital.
JUISI YA SPINACH AU BEET LEAVES MAJANI MA 2 TU KWA SIKU MUDA WA SIKU 3 UTAKUWA NA DAMU YA KUTOSHA
 
nimetoka kupima damu jana nina 9.8 gldl, ni kiwango kidogo sana karibia kupata anaemia, nimeshauliwa kula vyakula vya kungeza damu. nafurahi kuona nimegoogle nikaupata uzi huu, shukrani kwa wachangiaji wote, hakika mmetusaidia!
 
Tafuta kinywaji linafugwa Ribena kizuri sana
 
Mnahangaika wee! Nunua tende ,loweka na maziwa fresh yaliyochemshwa vzuri acha yapoe kidogo, yawe na uvuguuvugu, weka tende zako kwenye chupa, weka maziwa tikisa vzuri! Kisha yachujie kwenye kikombe kunywa mfululizo hata Lita 1.5 kila siku baada ya siku tatu kapime let's mrejesho
 
Momi chukua tembele fungu 1 librend kama juice kunywa grasi yako moja kesho kapime utashangaa
 
Aisee ata mimi naangaika alafu ukichemsha matembele unapata choo laini kwl
nimetoka kupima damu jana nina 9.8 gldl, ni kiwango kidogo sana karibia kupata anaemia, nimeshauliwa kula vyakula vya kungeza damu. nafurahi kuona nimegoogle nikaupata uzi huu, shukrani kwa wachangiaji wote, hakika mmetusaidia!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom