Naombeni msaada wa mawazo kwa wafugaji wa kuku wa nyama

ijoz

JF-Expert Member
Apr 16, 2012
731
714
Wazoefu wa ufugaji wa kuku wa nyama habarini za kazi.
Naomba mnisaidie ufafanuzi kwenye masuala haya ambayo nimekosa majawabu ya hakika.
1. Kuna tofauti gani ya gharama ya ufugaji na pia ubora wa nyama ya kuku ambao ni pure broilers ukilinganisha na ile ya machotara kama SASSO ambao utaamua kuwafuga kisasa kama wa nyama ndani ya wiki kumi?
2. Nimeshawafuga SASSO kama broilers, kwa kutumia chakula cha silverlands, lakini nataka kutumia mchanganyiko wa formula maalum ambazo wazoefu mmekuwa mkielezea humu ndani. Ila nilipoenda kwenye maduka ya Slverlands, waliniambia kuwa, naweza kutumia mchanganyiko kwa formula maalum (ambayo wao nao wanachanganya na kuuza) kwa kuongeza na chakula chao (broilers pellets) mfuko wao mmoja wa kilo hamsini,na debe kumi za pumba pamoja na hiyo mchanganyiko wao, Je, naweza kutumia mbinu mbadala bila kutumia hicho chakula chao ambacho kwa kweli kinagharama?
3.
Kuna madhara gani ya kutumia mchanganyiko huo (pengine ukuaji au chochote) ukilinganisha na hiyo broiler pellets?
Natanguliza shukrani kwa majibu yenu ambayo ni msaada
 
Na Jingine, (Kwa maana tu ya kufahamu), kuku wa nyama akipewa layers mash au kuku wa kienyeji akipewa chakula cha kuku wa nyama kuna madhara gani?
 
Back
Top Bottom