Naombeni msaada wa mawazo jinsi ya kumsaidia ndugu yangu aliyejiingiza kwenye biashara ya rupia

pakamwam

JF-Expert Member
May 28, 2013
516
651
habari za mchana .

moja kwa moja kwenye maada. Nina ndugu yangu ambaye alikuwa naendelea vizuri sana kimaisha. alifanikiwa kujenga nyumba ya ghorofa moja na nyumba nzuri Mbeya, Arusha na Dar es salaam. Ni mtu mwenye mke msomi ambaye naye ni mfanya kazi pia

Cha ajabu kaka yangu kaacha kazi ghafra na kujiingiza kwenye biashara ya kutafuta hela ya zamani kama rupia na hela za mjerumani.
Kaka kaacha familia na hata hajui kitu kuhusu ada za watoto mpaka tumeamua kuwatoa shule za kati yaani english medium na kuwapeleka shule za serikali za kawaida na sasa kajiingiza kwenye madeni kiasi cha kufikia hata kuuza nyumba baadhi na gari.
Najaribu kumshauri aachane na biashara hiyo anakomaa kuwa ni maisha yake so tumuache
Wasi wasi wangu ni juu ya watoto maana hata upendo wake umepungua kwa watoto. Huyu kaka yangu inaonyesha kuna mtu kadhibiti akili yake asilimia 100 kiasi kwamba hata akimwambia atoe kafara watoto anaweza.

huwa mara nyingine anakuja na vitu vya ajabu sana ambavyo naona hata aibu kuvisema na anapewa masharti makali mno

mimi naona ni utapeli wa kiasi kikubwa na ushirikina. Huu ni Mtazamo wangu.

Naombeni msaada wenu na uzoefu wenu kwenye hili wana jukwaa. ninaamini kwa uwingi wetu hapa hakuna la kushindikana.

mnisamehe kama sijajieleza vizuri ila nahitaji msaada wenu sana maana kuna maisha ya watoto watano na mimi ni mdogo mtu huu mzigo ni mzito kama kaka atakufa. Napenda nimuone anafanikiwa na nikiri tu hata mimi kaniasaidia sana. Nahisi kwa dhati kabisa nina deni la kumsaidia hasa kipindi hiki na ahata akifa nawajibika kwa watoto moja kwa moja ambao bado ni wadogo na wengie hata shule bado. lakini sijui hata mahali pa kuanzaia maana ukimfuatilia anakuwa mkali sana

amefikia mahali pa kuuza hata vifaa visivyozidi milioni moja kitu ambacho sijawahi kukiona toka utoto wetu. ni msomi aliyezunguka nchi nyingi ikiwemo ulaya na amerika na hata unapomwambia anakwambia yeye anaijua dunia kwa hiyo tumuache

asanteni sana
 
Na mimi nasubiri tiba nina mtu wangu wa karibu anaangamia na hizi mambo, ila kikubwa nilichokiona kwake ni kutaka kufanikiwa kwa shortcut, na akili zao zinakua kama zimeganda hivi yan haelewi la mnadi swala wala la muadhini anachowaza wapi akatafte, huyu wangu akisikia kuna mercury mwanza haijalishi yu tayari kwenda nasubiri tiba na mie
 
Inasadikika ni hazina zilizoachwa na wajerumani kipindi cha utawala wao,ni nyingi sana katika hazina hizo kuna stove, pas ya mkaa ambayo huweki mkaa unaweka juani unapiga pasi, kuna jambia vitu vingi tu ukiangalia kwa kawaida unaona kabisa ni changa la macho, mimi wangu alikuja na hizo rupia, kuna sarafu imeandikwa 20 heller bado zote zikawa feki sasa hivi kajikita kwenye kutafta mercury, ni mtihani usiombe umkjte ndugu yako
Ningeelewa hiyo rupia na pesa za ujerumani ni nini, ningeweza kuchangia vzr
 
Huyo kaka yako tafuta ndugu ambao ni wazee kwakee ongea nao kuhusu hiyo ishuu.. Wewe hapo hakuelewii aisee.. Mtafute na mtu ambae alipoteza muda wake kufanya huo upuuzi wa Kutafuta pesa na mali za wajerumani..

Sent using Jamii Forums mobile app
yaani mkuu, nilivyoleta hapa post tumetoka kuongea na mama. naye kasema kashindwa. baba naye kajitahidi anasema ameshindwa. ndio maana mpaka nimekuja kuomba ushauri hapa. tumewashirikisha hata viongozi wa kiroho lakini hawasikilizi
 
Inasadikika ni hazina zilizoachwa na wajerumani kipindi cha utawala wao,ni nyingi sana katika hazina hizo kuna syove, pas ya mkaa ambayo huweki mkaa unaweka juani unapiga pasi, kuna jambia vitu vingi tu ukiangalia kwa kawaida unaona kabisa ni changa la macho, mimi wangu alikuja na hizo rupia, kuna sarafu imeandikwa 20 heller bado zote zikawa feki sasa hivi kajikita kwenye kutafta mercury, ni mtihani usiombe umkjte ndugu yako
dah nilijua yametufika sisi peke yetu kumbe na wewe. pole sana ndugu yangu. yaani nawaza mapaka nachoka. inafikia wakati nakosa amani kabisa. yaani kachoka madeni na kuacha watoto .
 
Poleni sana;

Kaka yako ni mgonjwa anauua ugonjwa unaitwa SEARCHERS SYNDROME hauna tiba ya moja kwa moja kwani wote anaokuwa nao huwa ni wagonjwa.Huwa unatokea pale maisha ya kawaida yanapopteza msisimko.Huwa inaanza taratibu na watu wasipoundua mapema huwa mtu anafikia hatua ya kipekee.Mimi mwenyewe nimepata kuugua huo ugonjwa ila sio kwa kutafuta rupia ni kwa kutafuta madini mengine.

Ili kumsaidia kwanza lazima utake kushirikiana naye katika hilo ili ujue wato anaoshirikiana nao maana huwa wengine humshika kimazingara.Ukishawajua watamuacha ama watawashika wote.SO kuwe makini

NB.Searcher Syndrome ni mimi nimelitumia hapa kwa sababu ndivyo nilivyouita baada ya kupona
 
Inasadikika ni hazina zilizoachwa na wajerumani kipindi cha utawala wao,ni nyingi sana katika hazina hizo kuna stove, pas ya mkaa ambayo huweki mkaa unaweka juani unapiga pasi, kuna jambia vitu vingi tu ukiangalia kwa kawaida unaona kabisa ni changa la macho, mimi wangu alikuja na hizo rupia, kuna sarafu imeandikwa 20 heller bado zote zikawa feki sasa hivi kajikita kwenye kutafta mercury, ni mtihani usiombe umkjte ndugu yako
aisee, kwa maelezo yako na hiyo tabia zinazowapata baada ya kuanza kujihusisha na hayo mambo kutafuta hizo hazina, i think kuna maroho yanawavaa na kuwapumbazu wanakuwa sio wao, hapo ni maombi tu mana hiyo si hali ya kawaida
 
Afadhali ya wewe wa kwetu ni kijana mdogo tu hata familia hana lakini akilala akiamka akili yake inawaza mercury ilipo mwanzoni alipoanza kunambia hizi habar sikumpatiliza lakini imekua too much anaweza nipigia sim nimepata sufuria inabadilisha maji natafta soko namwambia niletee hiyo sufuria nione haji na akikueleza hizo mambo yan huamini, ananambia hizo mercury kupata ni kwenye miamba na sio rahisi kuna majoka joka hahaha mtihani wallah
dah nilijua yametufika sisi peke yetu kumbe na wewe. pole sana ndugu yangu. yaani nawaza mapaka nachoka. inafikia wakati nakosa amani kabisa. yaani kachoka madeni na kuacha watoto .
 
Yani wenyewe wanakwambia hizo mali zilizindikwa na damu za watu so kuzipata sio kwa urahisi me aliwahi nambia kuna wakati ukichimba mnaona nyuki hamjui wanapotokea very interesting
aisee, kwa maelezo yako na hiyo tabia zinazowapata baada ya kuanza kujihusisha na hayo mambo kutafuta hizo hazina, i think kuna maroho yanawavaa na kuwapumbazu wanakuwa sio wao, hapo ni maombi tu mana hiyo si hali ya kawaida
 
Hamna mtu wa kumbadilisha mtu yoyote zaidi ya rafiki yake wa karibu..kama rafiki yake wa karibu na yeye yupo kwenye hiyo biashara basi mshampoteza..ila kama rafiki yake wa karibu hajihusihi bas huyo ndo wakumtumia kumbadilisha..tofauti na hapo ata utumie mababu wa zamani sahau..kama mnahisi karogwa nendeni mkamkomboe ndugu yenu pia mapema..


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
yaani mkuu, nilivyoleta hapa post tumetoka kuongea na mama. naye kasema kashindwa. baba naye kajitahidi anasema ameshindwa. ndio maana mpaka nimekuja kuomba ushauri hapa. tumewashirikisha hata viongozi wa kiroho lakini hawasikilizi
Nikutanishe nae nimpe experience.
Sitasahau nilifikishwa kwa mganga nguli (Maarufu kama Otto) sumbawanga vijijini. Nikapewa fufumark, hizo mashart zilinitoa nduki, nikapelekwa kwa mzee mwingine, nikapewa mzigo, nikaambiwa isionekane na mtu na isilowane (kwa urahisi akashauri niweke kwenye kikopo cha mafuta, nikanunua babycare, nikatoa mafuta yote, nikaweka sarafu, nikarudisha mafuta.

Kufika dar, pekenyua mafuta yote sarafu haipo, kupiga simu kwa mzee, ananiambia "TATIZO ULIKULA NYAMA NJIANI, HELA IMERUDI, IPO HUKU KWANGU".

Aache kabisa upumbavu huo. Me nliambiwa hiyo fufumark ni trillion moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom