Naombeni msaada wa kujua Technical requirement na vifaa Vyote vinavyoitajika nikiwa Nataka kufungua kituo cha Radio FM.

tafuta mkoa mwingine ila kwa dar sikushauli kwa sababu dar radio ni nyingi na frequense zimebanana sana
 
I think you should focus on real estate
maana hata Ruge na Kusaga wanafanya real estate
 
Upo Uzi humu ndani,search tu"gharama za kuanzisha Fm radio,ukiandika Radio zitakuja nyuzi nyingi
CC
Radioproducer
 
Kwa mwenye kujua naomba ushauri. Nikiwaona wenye redio stations napata raha kwasababu napenda media. Je hadi kuanza matangazo yake,kituo cha redio FM mtaji wake ni sh. Ngapi?

siyo chini ya milioni 300 mkuu,. Jipange
 
Kwa mwenye kujua naomba ushauri. Nikiwaona wenye redio stations napata raha kwasababu napenda media. Je hadi kuanza matangazo yake,kituo cha redio FM mtaji wake ni sh. Ngapi?

Mtafute bwana mmoja anajiita Radio Producer ni member humu Jf huwa ana maelezo mazuri sana kuhusu hii hoja yako, Hawa wengine fix tu, so umeona umeshaambiwa na M 300? Utafikri unataka kuanzisha TV station!! Jaribu ku-search hilo jina!
 
unahitaji
kuwa na studio yenye basic studio equipments kama mics hasa
condenser,digital au analogue mixer ya njia nane na kuendelea, computer
angalao mbili na gadgets nyingine kidogo za sound production, ila
kikubwa kinachokula pesa ni Transmitter angalao ya 1kw na antenna yake
na limiter, vyote vinaweza cost around 40m ingawa kuna vifaa used pia,
cha msingi budget yako ndio itasaidia unataka kuwa na radio ya ukubwa na
standard ipi! pata ushauri wa engeneers pale ITV au TBC hasa linapokuja
swala la aina ya Transmitter inayofaa kwani hiyo ndio radio, hakikisha unanunua ambayo ni imara na hata ikipata hitilafu marekebisho yake hayasumbui!
 
Kwa mwenye kujua naomba ushauri. Nikiwaona wenye redio stations napata raha kwasababu napenda media. Je hadi kuanza matangazo yake,kituo cha redio FM mtaji wake ni sh. Ngapi?

Mkuu sijui kuunganisha uzi wenye maelezo unayoyataka, ila kuna uzi ulianzishwa na Radio producer unasema kuanzisha radio station. Hebu jatibu ku-search huo uzi hapa jamvini utaupata na utapata contacts za huyo jamaa.
 
Kwa mwenye kujua naomba ushauri. Nikiwaona wenye redio stations napata raha kwasababu napenda media. Je hadi kuanza matangazo yake,kituo cha redio FM mtaji wake ni sh. Ngapi?
Thread yenye majibu yako ipo hapa jf nenda new post utaiona hapo.
 
Radio producer aliwahi kuandika hivi....
Wadau,
Mara kwa mara napenda kutoa fursa hizi za pekee kwa wale wanaopenda kuwekeza katika biashara ya radio. Katika msimu huu wa sikukuu napenda kuwaletea ofa ya kipekee mno kutoka kampuni yetu ya Radio Consult.

Kwanza kabisa napenda kutoa hatua za kufuata unapotaka kuanzisha kituo cha radio kama ifuatavyo:-


Baseline Survey
Strategic Plan
Feasibility Study
TCRA license application
Purchase of equipments
Installations of studios and transmission sites
Planning and scheduling (review from Feasibility Study)
Trainings for selected staffs (ABC for studio operations, troubleshooting, programmes management, presenting skills, branding for GT radio, management, marketing etc



Hizi hapo juu ndiyo hatua za kuanza na kuzingatia! Nisingependa kufafanua zaidi hapa ila kwa yule anayehitaji huduma hizi tunaweza kuwasiliana!

Jambo la mwisho napenda kushare studio package (Vifaa vya radio iliyokamili kwa studio 2 na transmitter ya kurushia matangazo.
Kwa kifupi tu kuna studio mbili ya on air na kuandalia vipindi, kuna simu za studioni computer 3, transmitter ya watts 300 na antena zake, yaani iko kamili kamili ni kufunga tu na kwenda hewani!)

Gharama ya packege hii yote ni Tshs 25,000,000/= milioni ishirini na tano bila gharama za kodi+bandari na usafirishaji.

Kwa maelezo na msaada zaidi tembelea Radio Consult Company Limited au tuandikie email: consultancy@radiotz.com)

Karibuni!
 
Kwa mwenye kujua naomba ushauri. Nikiwaona wenye redio stations napata raha kwasababu napenda media. Je hadi kuanza matangazo yake,kituo cha redio FM mtaji wake ni sh. Ngapi?

Ndugu Xperience
Leo hii jumapili duh nilikuwa mbali sana, nimeingia nimekuta thread yako na kwa msaada wa taarifa za members humu.

Kuanzisha radio ni sawa na ujenzi wa nyumba, mara nyingi sana unategemeana na nyumba ya aina gani wewe unataka kuanzisha/radio ya namna gani wewe unataka kuanzisha.

Mfano rahisi kuna radio zinazosikika kwa covarage ya wilaya tu gharama zake zipo chini mno, kwa makadirio yasiyo rasmi, Mfano kama vifaa vinaweza kugharimu si zaidi ya TZS30,000,000/= milioni thelathini. Ada za leseni+frequency+application fee za TCRA hazitazidi milion 7. Gharama za studio (matengenezo)+consultation fee+installations fee haziwezi zidi m6.

Hivyo kwa haraka haraka unapata kama m43 hivi.

Kwa radio ya mkoa (kitaalamu TCRA wanaita Reginal coverage) katika gharama zote hapo juu inaweza kuongezeka m25.


Tahadhari: Makadirio haya ni makisio tu ukitaka uhalisia kabisa wa project hii fuata hatua zifuatazo:-

1. Lazima kufanya fieasibility study (ambayo ndiyo itatoa total fixed budget ya project yako nzima)
Lakini pia itakupa complete package ya documents zote za kusubmit TCRA.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa email: consultancy@radiotz.com copy to: lucnews@yahoo.com
Tunakusihi kuwahi huduma ili kupata huduma mapema kwasasa kuna ordering nyingi na mpaka hapa nakuandikia ni busy busy na project za watu.

Karibu sana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom